Baada ya Dhiki Faraja... Tumvumilieni Rais Magufuli

Baada ya Dhiki Faraja... Tumvumilieni Rais Magufuli

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,181
Tuacheni na tabia ya kuangushana na kupondana. Kiukweli Serikali ya Mheshimiwa Magufuli imewaamsha Watanzania na tumeona japo kwa miaka michache hii aliyokuwepo madarakani, bila ya kumeng'enya maneno. Rais Magufuli ameiinua Tanzania katika uhalisia wa uongozi na ni namna gani kiongozi anatakiwa awe, kwenye uongozi ameweka udugu, ujamaa, urafiki karibu lakini kwenye maamuzi ameuweka unasaba huo pembeni.

Kuna mambo madogo na makubwa yametokea na yanatokea na pia hatuondoi tegemeo kwamba yatatokea na ameonekana kukaa kimya au kuyafumbia macho, mfano lupotea kwa watu kama Bisanane kupigwa risasi Tundu Lissu huwenda uchunguzi bado unaendelea kwa kina, rais hawezi au ameonelea asijibu tuhuma, awachie wakuu wa upelelezi na waziri wao. Kwa hili kama wa kumsakama ni waziri wa ulinzi na wakuu wa upelelezi, na jibu linajulikana litakuwa upepelezi unaendelea na haujakamilika.

Sasa Shida na mazila tunayokutana nayo katika kuijenga Tanzania mupya ni mambo ya mpito,jamani mmesahu kama inasemwa Mji wa ajabu au mkongwe wa Zanzibar haukujengwa kwa siku moja aka Roma ya Africa.

Sasa ndio tukasema msitegemee mmelala mkiamka Magufuli amewezesha kila kitu mtakuwa hamna tofauti na wale aliowashtukia Ndugai pale bungeni.

Tanzania ya Nyerere sio hii ya Magufuli, uchumi umekuwa kila mtu sasa anamiliki smart phone 24hrs hakosi mtandaoni halafu mnasema akuna maendeleo, hivi mkisikia maendeleo mnafikiri ni kitu gani inawezekana hamujaelimika na hayo yanayoitwa maendeleo,kwa ufupi hayajengwi wala hayaji kwa siku au muda mfupi.
 
Tanzania tunaelemewa na ufinyu wa kufahamu angalia majibu yenu hapo,mmoja nimemtia sana huruma,mwengine anauliza mambo ya ndege,hivi hajaona hata moja,huyu anaulizia smart phone ni maendeleo, jamani kumbe wapo wengi wenye matatizo ya ubongo, hata aliekuwa hana jembe leo akipata uwezo akanunua jembe basi hayo ni maendeleo yake na ndio hivyo hivyo kwenye simu, bodaboda bajaji na vyombo vingine.

Zama hizo nyumba zenye simu ndani zilikuwa unazihesabu mtaani na sehemu nyengi mtaa mzima hamna mwenye simu.leo hii ndugu zanguni kila mtu anamiliki simu haijalishi ni ya aina gani, hivi ni wangapi wakimiliki simu sa mkononi wakati wa Mwalimu Nyerere kama ni ngumu nipe japo kwa ujumla wa asilimia! Ndio nimesema wengi hamuelewi maana halisi ya maendeleo mnafikiri yanakuja kama mawimbi ya maji.
 
Sasa ili mpate kuumbuka hebu elezeni nyinyi manyigu mwitu nini maendeleo, kwa mnavyofahamu huwenda hamuelewagi mnachoandika au hamuelewi kabisaaa maana ya maendeleo ndio ikawa mnapiga makelele,kama umeona mwizi anapapatua dirisha lako

Tulieni mje na hoja ya kwamba maendeleo tunayoyasema ni haya na yale.lakini unakurupuka eti GB kwa elfu tatu ukija kwangu utatoa elfu tano kama hutaki undoka na hamna kupatana.
 
Yaani tumvumilie mtu aliyeshindwa kuajiri, kupandisha madaraja, mishahara kulipa wastaafu kwa miaka mitano, aliyevuruga uchumi na kusababisha maelfu ya biashara kufungwa, kukimbiza wawekezaji, kuharibu mahusiano ya kimataifa, aliyeongeza umaskini wa watanzania maradufu , ndio tumvumilie labda wewe na familia yako.
 
hivi ni wangapi wakimiliki simu sa mkononi wakati wa Mwalimu Nyerere kama ni ngumu nipe japo kwa ujumla wa asilimia !
Ukisikia na kuuthibitisha ukweli kuwa baadhi ya members humu hawana uelewa ndo huu. Simu za mkononi zilianza kutumika Tanzania mwaka gani na Mwl alifariki mwaka gani? Hata kama ni ushabiki hapa umejidhalilisha kwa hoja hii. Pole sana mkuu!
 
Zile ndege nyingine 11 mpya kwa cash( keshi)

Zimefikia wapi sisi tulioko Chato tunataka ndege zetu bwana na maflai ova tunataka pia.
 
Ukisikia na kuuthibitisha ukweli kuwa baadhi ya members humu hawana uelewa ndo huu. Simu za mkononi zilianza kutumika Tanzania mwaka gani na Mwl alifariki mwaka gani? Hata kama ni ushabiki hapa umejidhalilisha kwa hoja hii. Pole sana mkuu!
Mnapoambiwa mna utindia wa ufahamu mnabisha,waTanzania tutumie akili zetu vizuri,hivi Mwalimu aliacha Uraisi na alipofariki ni miaka mingapi vile tokea October 14, 1999,imefikia miaka 22 kwa leo .

Kwa kuwasaidia wengi waliojaa upofu wa maendeleo hizi simu za mikononi zilianza kuingia mwaka 2000 habari za mtandao kwa simu mwaka 2013 mwaka 2018 miaka michache baada ya magufuli kuingia madarakani kengere ililia watu milioni 24 waliweza kutumia mitandao karibu asilimia 85 waliweza kujiunga laivu,sijui kama mlikuwa mmeshazaliwa kwenye zahanati mpya alizojenga Magu akiwa kwenye uongozi wake.

Wacheni hizo longolongo msiyafumbie macho maendeleo aliyoyaleta na kujifanya vipofu mwitu,harafu mnapoambiwa mvumilie basi tulieni tuli,

hayo ya ndege meli tireni mbona vinakuja,sasa jamani mnapoambiwa maendeleo sio kwa siku moja,hamuelewi au mnafanya makusudi kujitia uzuzu,mpaka mnaitwa mazwazwazwa.
 
Tuacheni na tabia ya kuangushana na kupondana. Kiukweli Serikali ya Mheshimiwa Magufuli imewaamsha Watanzania na tumeona japo kwa miaka michache hii aliyokuwepo madarakani, bila ya kumeng'enya maneno. Rais Magufuli ameiinua Tanzania katika uhalisia wa uongozi na ni namna gani kiongozi anatakiwa awe, kwenye uongozi ameweka udugu, ujamaa, urafiki karibu lakini kwenye maamuzi ameuweka unasaba huo pembeni....
Hivi unaongea kutoka wapi? Ni Tanzania ipi unayomaanisha? Kama Chato Ni Tanzania uko sawa!!

Ila mtu wenu ameleta umasikini kwenye kika pembe ya nchi
 
Tuacheni na tabia ya kuangushana na kupondana. Kiukweli Serikali ya Mheshimiwa Magufuli imewaamsha Watanzania na tumeona japo kwa miaka michache hii aliyokuwepo madarakani, bila ya kumeng'enya maneno. Rais Magufuli ameiinua Tanzania katika uhalisia wa uongozi na ni namna gani kiongozi anatakiwa awe, kwenye uongozi ameweka udugu, ujamaa, urafiki karibu lakini kwenye maamuzi ameuweka unasaba huo pembeni....
on your own opinion
 
Mnapoambiwa mna utindia wa ufahamu mnabisha,waTanzania tutumie akili zetu vizuri,hivi Mwalimu aliacha Uraisi na alipofariki ni miaka mingapi vile tokea October 14, 1999,imefikia miaka 22 kwa leo .....
Hayo siyo maendeleo bali Ni vitendea kazi vilivyopo. Ulitaka tumiliki smart phone mwaka 2000 wakati ilikuwa haijagunduliwa?

Mtoa mada hata ufanye nini mtu wenu Magu hauziki na hilo analijuwa ndiyo maana Oktoba 2020 hakusubiri tuhesabu kura, akaiba uchaguzi wote.

Atabakia katikka historian Kama Rais ALIYEFELI sana
 
Tuacheni na tabia ya kuangushana na kupondana. Kiukweli Serikali ya Mheshimiwa Magufuli imewaamsha Watanzania na tumeona japo kwa miaka michache hii aliyokuwepo madarakani, bila ya kumeng'enya maneno. Rais Magufuli ameiinua Tanzania katika uhalisia wa uongozi na ni namna gani kiongozi anatakiwa awe, kwenye uongozi ameweka udugu, ujamaa, urafiki karibu lakini kwenye maamuzi ameuweka unasaba huo pembeni...
Peleka Ujinga wako Chato huko
 
Back
Top Bottom