Baada ya Dege feki, rada feki, R'Mond feki, sasa uwanja feki

emedichi

Member
Mar 1, 2008
46
6
Mkandarasi alaumu uongozi wa U/Taifa

2008-04-17 10:01:14
By Jimmy Charles


Mkandarasi aliyepewa kazi ya kuufanyia ukarabati uwanja wa zamani wa Taifa ameutupia lawama uongozi wa uwanja huo kuwa wao ndio chanzo cha matatizo ya sasa ya uwanja huo.

Akizungumza na Nipashe jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya EKIKA iliyofanya kazi hiyo, Joseph Mushi, alisema kuwa wao hawahusiki na suala la miundombinu ya uwanjani hapo, ambapo kazi yao ilikuwa ni kutengeneza sakafu ya uwanja huo.

Mushi alisema kuwa anashangazwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa kampuni yao imeshindwa kuutengeneza uwanja huo, ambapo lawama zote zinapaswa kutupiwa uongozi wa uwanja kwa kuukataa ushauri wao juu ya kutanua mifereji ya uwanjani hapo.

``Nashindwa kuwaelewa tunatupiwa lawama kwa sababu gani, sisi kama EKIKA hatuhusiki na suala la mifereji kazi yetu ilikuwa ni kutengeneza sehemu ya kuweka nyasi bandia na ndio kazi tuliyoitekeleza, hayo mengine hayatuhusu,``alisema Mushi.

Alisema kuwa wakati wanafanya ukarabati wao walijaribu kuushauri uongozi wa uwanja kutanua mifereji yake ili kusafirisha maji kwa urahisi kitu ambacho hakikufanyika na badala yake mifereji iliachwa vile vile.

Mushi aliongeza kuwa watakuwa tayari kuifanya kazi ya kutanua mifereji endapo watapewa tenda upya ya kufanya kazi hiyo kama walivyopewa kazi ya kusawazisha uwanja.

Aidha, alisema katika kuondoa malumbano ni vema uongozi wa uwanja ukakaa pamoja na uongozi wa EKIKA ili kujadiliana jinsi ya kulitatua tatizo hilo kitaalamu.

Kwa upande wake Meneja wa uwanja huo, Charles Masanja, alisema kuwa suala zima la ubovu wa uwanja huo ameliacha mikononi mwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA),ambao ndio waliogharamia ukarabati huo.

Uwanja huo ambao mara baada ya kuwekwa nyasi bandia ulielezwa kuwa utaweza kutumika katika hali zote kitu ambacho ni tofauti kutokana na mara kwa mara kushindwa kutumika kufuatia sehemu kubwa ya uwanja kujaa maji pale mvua inaponyesha.
 
Mbona na hilo ji-uwanja jipya halitumiki? Au ndio yale yale.

Mwewe uwanja mpya umejengwa kwa ajili ya makumbusho ya taifa. kazi yake ni kwa watanzania kwenda kuungalia then basi.

Ulijengwa wakati wa mzee Ben, na kilikuwa ni kijimradi cha kifisadi na ndio jambo pekee rais wetu aliyepita analojivunia na ndicho kitu kitakachotusaidia kumkumbuka.
 
Maskini Tanzania,tutaamka lini? kila kitu kibovu hata cha mabilioni,kila mmoja anakula kwake, tutapona kweli? imefika wakati watanzania tuongee ama sivyo patachimbika, Uwanja huo kweli ni museum kila mtanzania akapige picha
 
Inadaiwa hata hiyo kampuni ya KAJIMA iliyopaswa kujenga Kilwa Road, sio hao Wa-japan wanaohusika kwa sasa. Shoddy workmanships zimeanza kujitokeza kutokana na mvua zinazoendelea. Inadaiwa kazi zote zinafanywa na ma-sub contractors tu kwa kutumia vifaa vya Kajima! Kama ndivyo, kutajengwa barabara ya maana?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom