Baada ya CUF kinafuata kifo cha CCM mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya CUF kinafuata kifo cha CCM mara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgeni wenu, Mar 2, 2012.

 1. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wana JF kama mnakumbuka majuzi niliwaambia kuhusu anguko la CUF mkoani Mara na wengine wakabeza na sasa limetokea,
  Habari kutoka Chanzo cha kuaminika sasa ni kufuatia kifo cha CCM (musoma mjini)mara baada ya kuletwa katibu mpya wa CCM ambaye anatajwa kuwa ni kibaraka wa Mgombea Urais(2015) .

  Katibu huyo akishirikiana na mbunge wa viti maalum(Rose kirigini) wamekuwa na mikakati ya kupanga safu upya ya wagombea wapya wa CCM ili kumpa nafasi kubwa mgombea wa Urais wa 2015 kwa tkt ya CCM.

  Mkakati uliyowekwa ni kuhakikisha Makongoro Nyerere anatoka kabisa katika Siasa za Mara kwa kuwa amekuwa mwiba kwa Mgombea huyo,na Nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa mwenyekiti wa vijana wa CCM (UVCCM)mkoa wa Mara ndugu Marwa Mathayo, pia Mkakati wa pili ni Kuhakikisha Mkurugugenzi wa Manisapaa ya Musoma aliyetajwa kwa jina moja tu la Mshana anaundiwa Zengwe ili aondoke kwani alikataliwa na madiwani wa CHADEMA kutoa fedha za kulipa posho za vikao vya CCM nae akakubaliana na madiwani wa CHADEMA musoma mjini ambayo imetafsirika ni kukwaza mipango maalum ya CHAMA tawala.

  Pia Njama hizi zinamuhusisha mkuu wa wilaya ya Musoma kapten mstaafu G ngatuni maana yeye ameahidiwa ukuu wa mkoa ifikapo 2015 au uwaziri kama akigombea Ubunge.

  Wana CCM wameahidi kama njama zao zitafanikiwa bac wapo tyr kuachana na siasa Uchwara na kuacha Chama kife kwani badala ya kupigania maslahi ya nchi sasa wanapigania maslahi ya Watu.

  Kwa Upande wake Makongoro Nyerere anathibitisha kutetea kiti hicho huku akitamba kuwabwaga vibaya wapinzani wake huku akisema anazijua njama zoote zilizopangwa na jinsi ya kukabiliana nazo kisayansi.

  Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Manispaa yeye simu yake alipoulizwa na mpasha habari hakuwa tyr kusema njama hizo ila alikiri kuombwa fedha za kuwalipa wajumbe katika vikao vya kamati ya siasa ya wilaya na aligoma kwa kuwa fedha hizo ni za maendeleo na sio posho za vikao vya chama na akasema yupo tayari hata kuafukuzwa kazi kwa kuitetea nchi yake na sio maslahi ya watu.

  Kwa Upande wa Rose Kirigini yeye anasema yupo kuelimisha wana mara kuhusu katiba mpya na sio mipango ya kumtoa mwenyekiti wa mkoa japo amekiri kuwa mwanyekiti huyo hana mvuto tena kwa wana CCM mausoma mjini kutokana kuacha Jimbo la Musoma mjini kwenda kwa Wapinzani(CHADEMA)na ameahidi kurudisha jimbo hilo kama atapewa nafasi ya Kugombea
  Pia kwa sasa nafasi ya mwenyekiti ni vizuri apewe kijana.

  Wakati huohuo aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa huo ndugu Chambiri nae amehakikisha kugombea kiti hicho iwapo Gachuma atagombea huku akilaani na kutabiri kifo cha CCM mara kama Makongoro ataendelea kuundiwa fitna na viongozi wa chama na Serikali kwani Makongoro ni mkweli nje na ndani ya chama na ni mwenye siasa za kutomuogopa wala kumuonea mtu.

  Pia kwa kitendo cha Chama tama tawala kuomba fedha za maendeleo kwa ajili ya posho za vikao vya kupanga safu ni kijipalia makaa kwa wananchi wenye kiu ya maendeleo,"kama tukiendelea hivi hiki chama tunakiua"alisema kwa Uchungu."Ndio maana tangu CHADEMA waingie madarakani kasi ya maendeleo ni kubwa mno kuliko awali sisi kama nchi tuangalie maendeleo kuliko vikao vya vyama"alisema CHAMBIRI

  MY take: kumbe safu za urais zinaanzia kujipanga kwenye chama tawala? Kwa nini wasipange kwa wananchi kwa kutatua kero kwanza?
   
 2. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi Mimi najua CCM ilishakufa kabla ya CUF. Bi mdogo na Bi mkubwa wote wataachika 2015
   
 3. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ipo ICU
   
 4. m

  mubi JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Udini unaiua ccm, wanaoitetea ccm, ni masheikh wanasema serikali ya mfumo kristo lazima ipingwe. Mpinga kristo yeyote hawezi kuingia kwenye ufalme wa mbingu. Kwa ccm kukumbatia hilo anguko lao limethibitishwa na baba mbinguni.

  Mwalimu nyerere alitamka serikali ya tanzania haina dini. Lakini ccm ya leo inasema serikali ina mfumo kristo lazima ipingwe , basi ndiyo wajue sasa kristo ni mkombozi ataiteketeza ccm , mbele ya macho yetu.

  Mungu awe nasi watanzania wote atupatie viongozi waadilifu, nitafunga kwa wiki moja kutubu na kuomba msamaha kwa mungu atusamehe wana ccm kwa dhambi hiyo. Si vizuri kumkata kristo ili tutawale.
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Changia bila jazba ya dini
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wewe pia mdini
   
 7. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Safari ni hatua, wachafu wote hawana nafasi 2015..... Wawe ccm, cuf ama vibaraka wengine wowote. Mabadiliko 2015 ni muhimu na ya lazima
   
 8. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Umenena vyema kaka
   
 9. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Jana Mtatiro kajitutumua Bunda
   
Loading...