kalisheshe
JF-Expert Member
- Mar 19, 2020
- 2,469
- 5,059
Happy,
Ulinipenda kutoka moyoni. Zaidi ya Mara 4 nilikwambia sikutaki lakini nilirudi mwenyewe ukanipokea tena. Nilikusaliti Mara 3 na rafiki zako uliishia kulia na kunisamehe
Happy hukuwahi kuniomba pesa kila nilipokupa pesa ulikataa na kuniambia hujanipendea pesa. Tofauti na vijizawadi vidogovidogo Happy hukuwahi kuchukua hata 100/= yangu.
Happy ulinipa mapenzi Kama hutonipa tena. Naukumbuka uzuri wako niliojifanya siuoni.
Happy naikumbuka vizuri ile siku unalia kifuani kwangu ukiniuliza kwanini nakufanyia hivyo! Au kwakua unanipenda?
Naukumbuka vizuri ufundi wako kupika Happy
Ni miaka miwili tokea nikuache umeolewa una mtoto mmoja. Mwenzako nimepita katika mahusiano 10 ambayo sijabahatika kumpata wa kufanana na wewe zaidi ya magumegume yaliyoishia kunifanya nikukumbuke.
Nafikiria kilichonifanya nikuache ila sikumbuki ni nini.
I really miss u Happy ingawa umeolewa. Kwa hakika jamaa ako amepata Mke
Bado nakupenda Happy
Ushauri: Wanaume tuache kuwanyanyasa wanaotupenda