Kifulambute
JF-Expert Member
- May 8, 2011
- 2,539
- 755
natumaini hamjambo wanajamvi wenzangu.....najua mna habari kwa nini kinaendelea kwa wenzetu Kenya kuhusu balaa la njaa linalowakumba... Juzi nimeshuhudia malori( semi trailers) kama 50 zikiwa na shehena ya mahindi kuelekea mpakani Horiri zikipeleka mahindi kenya, kwa taarifa niliyonayo serikali imepiga marufuku usafirishaji huo haramu lakini cha kushangaza polisi waliopo maeneo hayo wanaruhusu magari yapite kwa kitu kidogo wanachopokea kwa gunia moja ni Tsh 1000. sasa ninavyojua mbeleni hali kama hii ikitokea kwetu Wakenya kamwe hawawezi kuleta chakula kwetu....lazima tufe maana serikali kwa sasa wamejikita kwenye Posho, Symbion a.k.a TANESCO, itakapokuja njaa tutakimbilia kwa nanai? ....tujihadhali watanzania kwa njaa inayokuja