Baa la njaa; Kila mtu abebe msalaba wake,hatutaletewa chakula na serikali,tushikamane watoto,wajane

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Ni wazi kwamba daraja la kuunganisha wananchi na serikali katika baa la njaa limevunjika rasmi,tumepewa ujumbe kwamba hatutaletewa chakula na serikali,na kila mtu "atajiju"

Kilio changu ni kwa watoto,akina mama,vikongwe na yatima.

Kwa kuwa tuliowapa kazi ya kuratibu mambo yetu kwa niaba yetu,yaani serikali(social contract) wamesema wao haliwahusu,natoa wito kwa jamii,usiipite familia ya mjane bila kuisaidia,utabarikiwa.

Usiipite familia ya masikini,japo mara moja kwa wiki,isabahi,kama una mia tano ya unga,upatie,utabarikiwa.

Usiipite Nyumba ambayo unaamini kuna mzee kikongwe anaishi humo,kama una hela ya dagaa na unga,MPE,utabarikiwa.

Kwa kuwa Tanzania ilikuwepo hata kabla ya serikali kuwepo,zikaundwa serikali,zikatukuta,tuhakikishe asiwepo mmoja wetu ambaye tumbo lake litakauka kwa kukosa chakula mpaka kumtesa na kumpoteza.

Kinachofata ni ku-redraft our social contract
 
Hakuna Chakula cha Msaada lakin Serikal imenunua Tani elf 90 za Mahindi kwny ghala zake!
 
Back
Top Bottom