Asalaam aleykum...........! Bwana Yesu asifiwe........! Tumsifu Yesu Kristo............! ndugu wana jf, nipende kuwapongeza wote waliofanikiwa kupata wapenzi WA KWELI humu jf, hata hivyo ninatoa pole zangu kwa wale ambao kwa namna moja ama nyingine waliangukia pua pamoja na kuleta mabandiko humu ila bado wanasubiria aliye wa bahati kwao kuwa ipo siku ataliona na kulifikiria bandiko. Sijawasahau pia wale ambao baada ya kutambiana sana kwa kuchat waliishia kutimua mbio siku ya kuonana baada ya kukutana na kinyume cha matarajio yao, Mwenyezi mungu awabariki nyote kabisa!!!!!!!.
^^^^^^^^
Niliwahi kuleta bandiko langu hapa jf nikitafuta mwenzi wa maisha ili nitakapomaliza ka degree kangu mwezi ujao nisirud kazini kwangu bila mwandani, nikatiririka sifa na vigezo. Nawashukuru wote ambao baada ya kuona bandiko waliweza kunitafuta na tukafika tulipofikia. Kuna wengine walitaka tu kutest zali ili wapime spidi ya maji na walipopata findings zao, walichukua uamuzi, wengine walitumbukia wakaoga na wengine waliahirisha kuoga, wakavaa nguo na kuondoka zao.
&&&&&&&&&&
Baada ya kupima niliamua kuendelea na mmoja kwa kuzingatia vigezo nilivyoona kwake (Niliamua kuwaambia wengine wote wanisamehe kwa kuwa, tayari nimepata na nisingependa kuwapotezea muda). Katika harakati za kumfahamu vilivyo, niliamua kujifanya ---- pamoja na kuelezana likes and dislikes! Hapo niligundua mambo yafuatayo kwa mtarajiwa wangu ambaye kwa bahati mbaya hatukufanikiwa kukutana uso kwa uso.
$$$$$$$$$$$$$
Mwenzangu huyo kumbe ni THE GREAT THINKER KWELI ambaye kwa bahati mbaya hakuonesha kujua kuwa mimi pia natumia akili na pia nina uwezo wa kufanya ex-ante evaluation kama waitavyo wenzetu. Nilisikitishwa na kitendo cha kunipiga tarehe kila nikimwabia tuonane (nadhani alitaka kujiridhisha zaidi) niligundua kuwa labda ratiba yake ni ndefu na huenda kwenye list, jina langu lipo mbali kidogo, Naomba kupitia jf nimjulishe kuwa the appointment of meeting for marriage purposes has officially expired today 20[SUP]th[/SUP] June 2013 9:08pm. Hata hivyo, tutaendelea kuwa marafiki wa karibu kwa ushauri wa hapa na pale kwa maana maisha hayaishi leo.
:director:USHAURI.
Ninawaomba ! wana jf wote, wake kwa waume, kama bado hujawa tayari kuoa ama kuolewa, plz usianzishe uhusiano wa aina yoyote hapa, kwa ufupi usitafute mtu humu, UNAJITIA MIKOSI BURE, Kuna wengine wanatafuta wachumba ili hali wakiwa bado katika uhusiano na watu wao, naomba mtambue kuwa ukitofautiana na mwenzi wako, suluhisho si kutafuta mtu mwingine, kaeni muyamalize maisha yaende.
Kwa wale wanaotafuta kwa ajiri ya kugegedana au kampani tu, kuweni wazi kwa maana mtapata watu kwa ajiri hiyo,
MSIWAUMIZE WADADA WA WATU ROHO ZAO KWA KUWADANGANYA, maana wengi wanaotafuta humu, ni wale ambao wamepata misukosuko katika mapenzi na wanataka kutuliza roho zao kwa kupata Great thinkers, ukimuumiza mtu wa namna hii, adhabu yako ni kubwa mbinguni.
Mwenyezi Mungu awalinde wote waliopigwa vibuti, naomba msilipe visasi, ni maoni yangu.
Wasalaam
:disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::disapointed::smash::smash::smash::smash::smash::smash::smash::smash::smash::smash: