AZIMIO LA SONGEA - MADAI MANNE [4] KWA SERKALI

Cannibal OX

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
3,095
3,476
AZIMIO LA SONGEA - MADAI MANNE [4] KWA SERKALI

Mkutanoni Songea|Septemba 9, 2007

Azimio la Songea ni vuguvugu la kudai demokrasia katika maliasili (movement for resources democracy) iliyolenga kukuza Demokrasia nchini ili kuwaelimisha na kuhamasisha Watanzania kuujiuliza na kuuliza namna maliasili yao inatumika na kuendeshwa ikiwa pamoja na uwazi wa mikataba inayohusiana na maliasili hizo.

Azimio la Songea lina madai makuu 4;

1. Usisainiwe mkataba wa madini mwingine wowote ule mpya hadi pale jopo la wabunge, wanasheria na wataalamu wa madini na uchimbaji watakapo husishwa kupitia upya mikataba inayotumika sasa.

2. Vifungu vyote vya sharia ya uwekezaji vitega uchumi, sharia ya kodi ya maapto na sharia ya madini ( TIC Act of 1997, Income Tax Act of 2004 and Mining Act of 1998), vinavyotoa vivutio vya kikodi na kukosesha nchi mapato kutoka kwenye sekta ya madini lazima virekebishwe kwa kufutwa kabisa.

3. Serkali imiliki sio chini ya asilimia 25 ya hisa katika makampuni ya madini ikiwemo hisa za lazima zitokanazo na uwepo wa rasilimali hapa nchini kwetu (Golden Share).

4. Mrahaba unaotozwa kwa kampuni za madini ugawanywe kwa namna ambayo theluthi moja ibakie kwa Halmashauri za Wilaya zenye migodi, theluthi nyingine kwa Shirika la Madini la Taifa na theluthi iliyobakia kwa Mkoa ambao una mgodi au madini yamechimbwa.

*Mara baada ya ndugu Zitto Kabwe kumaliza ziara ya kuzunguuka nchi nzima kwa kumalizia Songea ambako lilitolewa azimio (Azimio la Songea); Mwaka huo huo (2007) Raia waliunda Tume ikiongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani. . Tume hiyo ikatoa taarifa kwa na ilichukua mapendekezo karibia yoote ya Azimio la Songea na kuyatumia. Hii ni hoja iliyowasilishwa na ndugu Zitto Kabwe kujadili taarifa ya kamti ya Bomani.

Zitto Kabwe.
 
Back
Top Bottom