Doctor Mama Amon
Platinum Member
- Mar 30, 2018
- 2,311
- 3,512
AZIMIO LA KAGERA: SABABU KUU YA KUMKUMBUKA RUGE
Sikuwahi kukutana uso kwa uso na hayati Ruge Mutahaba wakati wa uhai wake. Lakini, nimekutana na mawazo yake mengi. Hata hivyo, mawazo yanayonifanya nione sababu ya kumkumbuka milele ni “AZIMIO LA KAGERA.”
Ni Azimio lililozaliwa mwaka 2017 kutokana na “Makongamano ya FURSA na Mkutano wa Kilele cha Makongamano ya FURSA mwaka 2017 chini ya Uratibu wa Jukwaa la “FURSA Consultancy” likiwa chini ya Uongozi wa Ruge Mutahaba, wakati wa uhai wake.
Nimepata nakala ya azimio hili kutoka kwa rafiki yangu na naliweka hapa bila kuhaririwa. Na kwa sababu hii tu, nasema bila kigugumizi kwamba,
“RUGE MUTAHABA ANAYO HAKI YA KUPUMZIKA MAHALI ANAKOSTAHILI KULINGANA NA ALIVYOCHAGUA WAKATI AKIWA HAI.”
===================================================
1. UTANGULIZI
1.1 Dira, Dhima na Tunu za Azimio la Kagera
Azimio la Kagera ni tamko linaloonyesha dira ya vijana wa Tanzania iliyozaliwa Bukoba, Kagera katika mkutano wa kilele cha makongamano ya fursa kwa vijana uliofanyika tarehe 16-17 Disemba, 2017, chini ya mwavuli wa Jukwaa la Fursa. Dira, dhima na tunu zinazoongoza Azimio la Kagera ni kama ifuatavyo:
1.2 Chimbuko la Azimio la Kagera
Azimio la Kagera ni matokeo ya miaka 5 ya Kongamano la Fursa ambalo limekuwa likifanyika nchini. Lengo la makombamano hayo lilikuwa ni kushirikiana na vijana katika kuzitafutia majawabu changamoto zinazowakabili na kuwarudisha nyuma katika jitihada zao za kujikomboa kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Kwa miaka 5 mfululizo, Kongamano la Fursa limefanyika katika mikoa yote nchini likiibua fursa mbalimbali zilizoko katika mikoa na kitaifa, na kuhamasishana kuzichangamkia fursa hizo. Maudhui ya makongamano hayo yalikuwa yafuatayo:
Katika wito wake, Mheshimiwa Rais aliwaomba waandaaji wa Kongamano la Fursa kusaidia kuhamasisha vijana kushiriki katika Mapinduzi ya Kiuchumi katika kufanikisha azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda na kuifikisha nchi yetu kwenye uchumi wa kati. Kufuatia wito huo, na kwa kuzingatia kuwa wito huo aliutoa akiwa mkoani Kagera, iliamuliwa kuwa Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Fursa lifanyike mkoani Kagera na ndipo lilipozaliwa Azimio la Kagera.
1.3 Ushiriki na Ushirikishwaji
Azimio la Kagera ni matokeo ya ushiriki na ushirikishwaji mpana wa vijana na wadau mbalimbali kutoka nyanja mbalimbali kote nchini kupitia Kongamano la Fursa. Katika kipindi cha miaka 5, kupitia makongamano 90, Kongamano la Fursa limeweza kuwafikia ana kwa ana vijana wajasiriamali wapatao 250,000 na vijana wengine milioni 3 kupitia televisheni, radio na mitandao ya jamii kila mwaka.
2. MALENGO, KANUNI NA NGUZO ZA AZIMIO LA KAGERA
2.1 Malengo ya Azimio la Kagera
Malengo mahususi ya Azimio la Kagera ni pamoja na:
Kuhamasisha ushiriki wa vijana katika shughuli halali za kijamii na kiuchumi katika maeneo walipo;
Kushawishi mabadiliko ya fikra, dhana na mitazamo inayozuia vijana kuchangamkia na kutumia fursa zilizopo;
Kupashana habari na taarifa juu ya fursa zilizopo na zijazo ndani na nje ya nchi ili kuandaa mazingira na utayari wa kunufaika nazo;
Kushirikiana kwa kubadilishana taarifa, maarifa na uzoefu na kujengeana uwezo ili kuchochea ukuaji wa biashara na vipaji; na
Kuunganisha sauti kudai mageuzi makubwa katika uchumi wetu yenye lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa vijana ikiwemo uwepo wa miundombinu wezeshi kwa biashara, urahisi wa kupatikana kwa mitaji, unafuu na urahisi wa kulipa kodi, ada na tozo, na uwepo wa sera na sheria rafiki kwa vijana hususani wajasiriamali wa wadogo na kati.
2.2 Kanuni za Azimio la Kagera
Azimio la Kagera linaongozwa na kanuni kuu tatu muhimu zenye kuchagiza Mapinduzi ya Fikra na Mageuzi ya Kiuchumi. Kanuni hizo ni kuanzia sokoni, ubunifu na ujasiriajamii. Zinafafanuliwa hapa chini.
2.2.1 Kanuni ya Kuanzia Sokoni
Dhana ya kuanzia sokoni inahimiza kuacha kufanya biashara kwa mazoea na badala yake kuenzi matumizi mazuri ya utafiti na taarifa juu ya hali ya soko na mahitaji kabla ya uamuzi wa kuanzisha shughuli ya kipato na biashara. Matumizi mazuri ya teknolojia ya habari na mawasiliano ni nyenzo muhimu ya kupata taarifa za soko na kuyahudumia mahitaji hayo kwa ubunifu na kujitofautisha.
2.2.2 Kanuni ya Ubunifu
Dhana ya Ubunifu inasisitiza kwamba, badala ya kuigiza biashara za jirani zetu, yafaa kubuni mbinu na bidhaa mpya kwa lengo la kuongeza urefu wa mnyororo wa thamani wa bidhaa au huduma ya mwingine ambaye ametangulia sokoni. Yaani, kama ambavyo tunaongeza njia kwa kufyeka vichaka na mapori mapya badala ya kupitia njia ile ile waliyopitia wenzetu, ni vivyo hivyo kwa ubunifu katika biashara.
Kuna tofauti ya msingi kati ya ubunifu wa kuigiza na ubunifu wa kuunda kitu kipya. Katika ubunifu wa kuigiza, mbinu za kutatua tatizo zinazotumika huazimwa kutoka kwa majirani zetu. Na kwa upande mwingine, katika ubunifu wa kuunda kitu kipya, mbinu za kutatua tatizo zinazotumika huundwa kwa mara ya kwanza, kwa maana kuwa, hazipatikani mahali pengine popote duniani.
2.2.3 Kanuni ya Ujasiria-jamii
Ujasiriajamii ni mchakato wa kufungamanisha nguvu za serikali, soko na jamii katika namna ambayo inatoa uhuru zaidi kwa watendaji walio katika asasi za kiraia kubeba majukumu ya huduma za kijamii ambazo hapo awali zilikuwa zinatolewa na serikali, na hivyo watendaji walio katika asasi za kiraia kupata fursa ya kujiongezea kipato kwa njia hiyo. Huduma hizo ni pamoja na usafi wa mazingira, kutunza watoto wadogo, kusomba taka ngumu, kutunza mazingira, kusambaza maji safi na salama, na kuendesha hudumza wa vituo vya watoto wa chekechea.
2.3 Nguzo za Azimio la Kagera
Azimio la Kagera limesimama juu ya nguzo tano ambazo zitawezesha kufanikiwa kwa utekelezwa wa Azimio hili. Nguzo hizi nne ni: uimara wa taasisi za malezi ya kijamii, matumizi ya tekinolojia ya kisasa, ubora wa nguvu kazi, ujenzi wa uwezo wa mtu mmoja mmoja, mabadiliko katika mtazamo wa maisha.
2.3.1 Taasisi imara
Taasisi kama familia, shule, dini zina mchango wa pekee na zinapaswa kutimiza wajibu wao kikamilifu. Kwa upande mwingine, taasisi za Serikali zina wajibu wa kuwezesha vijana kutimiza ndoto zetu na wajibu wetu kwa taifa. Tunadai mabadiliko katika uendeshaji wa taasisi za Serikali ili ziwe wezeshi na sio kikwazo. Tunataka Taasisi zinazofungua milango badala ya kujenga kuta, Taasisi zinazotufuata badala ya kutukimbia, Taasisi ambazo kipaumbele chake ni kutoa huduma badala ya kuadhibu na Taasisi zinazojivunia kulea biashara badala ya kufurahia kuzifungia.
2.3.2 Tekinolojia ya kisasa
Kwa wastani, tayari dunia inaendelea kushuhudia mabadiliko makubwa na ya haraka kutokana na matumizi ya tekinolojia momboleo. Kwa mujibu wa historia ya dunia, ujio wa uchumi wa viwanda ni zao la mapinduzi ya viwanda yaliyopitia katika hatua nne mpaka sasa. Kuna mapinduzi ya kwanza mpaka mapinduzi ya nne.
Kwa ufupi, kila zama za mapinduzi ya viwanda ni kipindi cha historia ya wanadamu ambamo kulitokea mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa sababu ya ugunduzi maalum wa kiteknolojia.
2.3.2.1 Mapinduzi ya Kwanza ya Viwanda, 1765-1870
Mapinduzi ya kwanza ya viwanda kilikuwa ni kipindi ambamo makaa ya mawe, maji na injini za mvuke wa maji vilitumika kama vyanzo vya nishati ya kuendesha uzalishaji kimakanika. Katika mtindo huu mpya wa uzalishaji nafasi ya kilimo ilichukuliwa na karakana na viwanda kama mfumo mpya wa kiuchumi katika jamii. Mapinduzi haya yalitokea kati ya 1765 na 1870 huko Ulaya na Amerika. Katika kipindi hiki, jamii za wakulima na vijiji viligeuka kuwa viwanda na miji. Viwanda vya chuma na kusokota nguo, pamoja na injini ya kutumia mvuke wa maji, vilikuwa ni uti wa mgongo wa uchumi katika kipindi hiki.
2.3.2.2 Mapinduzi ya Pili ya Viwanda, 1870-1914
Mapinduzi ya pili ya viwanda kilikuwa ni kipindi ambamo umeme, gesi na mafuta vilikuwa ni vyanzo vikuu vya nishati iliyotumika kuendesha uzalishaji kimakanika. Nishati hizi zilichochea kubuniwa kwa injini inayofanya kazi kwa kuunguza mafuta na gesi na hivyo kuboresha uzalishaji.
Katika ulaya na Amerika mapinduzi haya yalitokea kati ya mwaka 1870 na 1914, muda mfupi kabla ya vita kuu ya pili ya dunia. Kilikuwa ni kipindi cha maendeleo ya viwanda vya awali na upanuzi wa viwanda vipya, vikiwemo viwanda vya chuma, na uhandisi wa kikemia uliozalisha nyuzi na vifaa vya plastiki bandia, rangi na pembejeo za kilimo.
Mageuzi makubwa ya kiteknolojia katika kipindi hiki yalihusisha simu ya upepeo, simu ya waya na balbu za umeme. Aidha, miundombinu ya usafiri iliboreshwa kutokana na kubuniwa kwa magari na ndege mwanzoni mwa karne ya 20.
Ugunduzi wote huu uliwezekana kutokana na kuelekeza nguvu katika utafiti na kuwekeza mitaji iliyosimamiwa kwa kutumia modeli modeli mpya za utawala na uongozi wa uchumi wa viwanda.
2.3.2.3 Mapinduzi ya Tatu ya Viwanda, 1969-leo
Mapinduzi ya tatu ya viwanda, au Mapinduzi ya Kidigitali, ni kipindi ambamo vifaa vya kielektroniki na kompyuta vinatumika kuendesha mitambo ya uzalishaji badala ya binadamu, na ambamo nishati ya nyuklia inatumika kama chanzo kipya cha nguvu za kuendesha mitambo kimakanika.
Hiki ni kipindi ambamo kuna maendeleo ya kuteknolojia yanayoendana na kuachana na matumizi ya vifaa vya elektroniki vya kianalogia kwenda kwenye vifaa vya elektroniki vya kidigitali. Huko Ulaya na Marekani, kipindi hiki kilianza tangu 1969, kikaimarika katika miaka ya 1980 baada ya kompyuta ya mezani kugunduliwa, na sasa kinaendelea.
Katika kipindi hiki, ugunduzi wa kiteknolojia ni pamoja na kompyuta ya mezani, intaneti, na kufungamana kwa kompyuta na mawasiliano ya simu. Mapinduzi haya yaliambatana na kubuniwa kwa vifaa vya kielektroniki kama vile transista na maikrochipu.
Kwa sababu ya udogo wake, vifaa hivi vya kielektroniki vimesaidia katika kutengenezwa kwa vyombo vya kielektroniki vinavyosaidia katika kufungua milango ya utafiti katika anga la mbali na bayotekinolojia. Viwandani, vifaa hivi vya kielektroniki vimewezesha sehemu kubwa ya kazi za mikono kufanywa kwa kutumia mashine kama vile automatoni na roboti.
2.3.2.4 Mapinduzi ya Nne ya Viwanda
Na mapinduzi ya nne ya viwanda yanaanzia kwenye mapinduzi ya tatu, yaani mapinduzi ya kidijitali. Ni mapinduzi yanayohusisha matumizi ya mbinu mpya za kupenyeza tekinolojia katika jamii na pia ndani ya mwili wa binadamu. Kuna ugunduzi kama vile matumizi mapana ya roboti, matumizi ya akili bandia, nano-teknolojia, bayo-tekinolojia na magari yanayojiendesha bila dereva.
Kwa ujumla, katika “Zama za Kompyuta” maarifa na stadi zinazohusiana na masomo ya “Sayansi, Teknolojia, Elimu ya Uhandisi na Mahesabu,” au “STEM” kwa kifupi, ni nyenzo muhimu kwa ajili ya kuwafanya vijana wa kike na kiume kuwa sehemu ya uchumi wa viwanda.
2.3.3 Nuvu kazi bora
Nchi yetu bado inayo changamoto kubwa ya upungufu wa nguvu kazi yenye maarifa, weledi na mtazamo unaowiana na mabadiliko ya kifikra na kiuchumi tunayoyataka. Vijana tunaamini kuwa ili kuzikabili changamoto zilizo mbele yetu, mageuzi na uwekezaji mkubwa katika mfumo wa elimu na mafunzo yanahitajika. Sambamba na hilo, tunaamini kuwa lazima kama taifa tufanye uwekezaji wa kutosha kwenye Nyanja za sayansi, tekinolojia, uhandisi na mahesabu na utafiti ili kuwandaa vijana kuzikabili changamoto za kiuchumi na kijamii kwenye karne ya ishirini na moja.
2.3.4 Mitazamo mipya
Dunia inabadilika kwa kasi inayotulazimisha kubadili mitazamo yetu. Ndani ya karne mbili pekee tayari tumepitia katika zama nne za mapinduzi ya viwanda. Zamani, nchi yetu ilikuwa ni ya wakulima na wafanyakazi pekee. Lakini leo, Tanzania ni nchi ya wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wabunifu, wasanii, wavumbuzi na wanamichezo. Aidha, mitazamo tuliyonayo juu ya tekinolojia, mifumo ya uchumi, fursa, ajira, ujira na mafanikio ni vikwazo dhidi ya ukombozi wetu. Ili twende mbele, hatuna budi kuachana na tabia za kulalamika, kutamani mafanikio ya haraka, kutegemea miujiza na kubagua kazi. Ni wakati sasa wa kuwa na fikra na mitazamo chanya, kuona fursa kwenye vikwazo, funzo kwenye kukosea na matumaini kwenye kukata tamaa.
2.3.5 Ubora wa sera za uwezeshaji
Tunaweza kusema bila kupepesa macho kuwa wajibu wa kwanza wa kulitekeleza Azimio la Kagera ni wetu sisi vijana. Hata hivyo, serikali na wadau wengine pia watahusika kwa yale mambo yanayoangukia katika wajibu wao. Hivyo, wajibu na majukumu ya utekelezaji wa Azimio la Kagera ni kama ifuatavyo:
3.1 Wajibu wa Vijana
Azimio la Kagera litatekelezwa na wadau wote chini ya uratibu wa Kamati ya Kitaifa ya Fursa itakayokuwa na jukumu la kuandaa, kusimamia, kufuatilia na kuratibu Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Azimio la Kagera. Utekelezaji wa Azimio la Kagera na Mkakati wake vitafanyiwa tathmini kila mwaka kupitia Jukwaa la Fursa katika ngazi za mikoa na Taifa.
5. HITIMISHO
Vijana wa Tanzania tunacho kila tunachohitaji kututoa hapa tulipo kutufikisha kwenye maisha yaliyo bora zaidi, kwenye Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati. Tunachohitaji ni kukusanya pamoja nia, ari, uthubutu wetuchini ya Azimio la Kagera, kwa kufanikisha Mapinduzi ya Fikra na Kiuchumi katika nchi yetu.
Tunao wajibu mabegani mwetu wa kukabidhi vizazi baada yetu, Tanzania iliyo bora zaidi kuliko ile tunayoipokea kutoka kwa vizazi kabla yetu. Wajibu huu ni wetu, hakuna badala yetu.
6. SHUKRANI
Awali ya yote, Jukwa na Fursa la Kitaifa tunawashukuru vijana wote waliojitokeza katika mikutano ya Fursa na kuelezea uzoefu na changamoto zao. Uzoefu waliotupatia, changamoto walizoziainisha na mapendekezo waliyoyatoa ndio vilivyowezesha kuandaliwa na kukamilika kwa Azimio la Kagera.
Pili, tunawashukuru viongozi wetu kuanzia ngazi ya serikali za mitaa hadi serikali kuu nchi nzima. Wameshirikiana nasi kuwaleta vijana pamoja, kutuhakikishia usalama na amani kwenye mikutano yetu na kuitikia wito kila tulipowaita kuongea na vijana wenu. Kwa upekee kabisa tunawashukuru Marais wote wa awamu mbili za maisha ya miaka mitano ya Fursa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyezindua Semina za Fursa mwaka 2014 na Rais John Pombe Magufuli aliyetupa changamoto ya kuwa na Mkutano wa Kilele wa Fursa akiwa ziarani mkoa wa Kagera.
Mwisho, ni shukrani kwa taasisi zote zilizoshiriki Makongamano ya Fursa. Hizi ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Benki ya Letshego na Wizara ya Afya na Clouds Media Group waliotoa michango yao ya kitaalamu, kifedha na kiuwezeshaji katika kufanikisha Mkutano wa kilele cha Fursa unafanyika na kuwezesha ujumbe wa Fursa kuwafikia vijana kokote walipo.
Tungeweza kuwataja wote, lakini ukurasa huu hautoshi kubeba uzito wa shukrani zetu kwa kila mmoja wenu mmoja mmoja. Kwa pamoja tunasema asanteni sana.
RUGE MUTAHABA
MWENYEKITI NA MWANZILISHI WA JUKWKAA LA FURSA,
BUKOBA,
DISEMBA 2017.

- DIRA: Vijana wenye maisha bora, walio na mabadiliko ya kifikra na wenye utayari wa kushiriki katika mageuzi ya uchumi wa viwanda.
- DHIMA: Kuwaamsha vijana ili waweze kupigania maisha bora kwa kujinufaisha na fursa za kiuchumi zitakazowasaidia kupandisha viwango vya ubora wa maisha yao, kujenga taasisi zinazoweza kuwajengea heshima na kuwapa matumaini, na kuwaongezea uhuru wa kuchagua.
- TUNU: Maisha bora, ongezeko la kipato, lishe bora, tiba nzuri, elimu bora, heshima, matumaini, hadhi ya ubindamu, uhuru wa kuchagua, taarifa sahihi.
1.2 Chimbuko la Azimio la Kagera
Azimio la Kagera ni matokeo ya miaka 5 ya Kongamano la Fursa ambalo limekuwa likifanyika nchini. Lengo la makombamano hayo lilikuwa ni kushirikiana na vijana katika kuzitafutia majawabu changamoto zinazowakabili na kuwarudisha nyuma katika jitihada zao za kujikomboa kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Kwa miaka 5 mfululizo, Kongamano la Fursa limefanyika katika mikoa yote nchini likiibua fursa mbalimbali zilizoko katika mikoa na kitaifa, na kuhamasishana kuzichangamkia fursa hizo. Maudhui ya makongamano hayo yalikuwa yafuatayo:
- 2013: Jitathmini, Jiamini, Jiongeze
- 2014: Kamata Fursa twenzetu
- 2015: Fursa 10
- 2016: Ongeza Thamani
- 2017: Anzia Sokoni
Katika wito wake, Mheshimiwa Rais aliwaomba waandaaji wa Kongamano la Fursa kusaidia kuhamasisha vijana kushiriki katika Mapinduzi ya Kiuchumi katika kufanikisha azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda na kuifikisha nchi yetu kwenye uchumi wa kati. Kufuatia wito huo, na kwa kuzingatia kuwa wito huo aliutoa akiwa mkoani Kagera, iliamuliwa kuwa Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Fursa lifanyike mkoani Kagera na ndipo lilipozaliwa Azimio la Kagera.
1.3 Ushiriki na Ushirikishwaji
Azimio la Kagera ni matokeo ya ushiriki na ushirikishwaji mpana wa vijana na wadau mbalimbali kutoka nyanja mbalimbali kote nchini kupitia Kongamano la Fursa. Katika kipindi cha miaka 5, kupitia makongamano 90, Kongamano la Fursa limeweza kuwafikia ana kwa ana vijana wajasiriamali wapatao 250,000 na vijana wengine milioni 3 kupitia televisheni, radio na mitandao ya jamii kila mwaka.
2. MALENGO, KANUNI NA NGUZO ZA AZIMIO LA KAGERA
2.1 Malengo ya Azimio la Kagera
Malengo mahususi ya Azimio la Kagera ni pamoja na:
Kuhamasisha ushiriki wa vijana katika shughuli halali za kijamii na kiuchumi katika maeneo walipo;
Kushawishi mabadiliko ya fikra, dhana na mitazamo inayozuia vijana kuchangamkia na kutumia fursa zilizopo;
Kupashana habari na taarifa juu ya fursa zilizopo na zijazo ndani na nje ya nchi ili kuandaa mazingira na utayari wa kunufaika nazo;
Kushirikiana kwa kubadilishana taarifa, maarifa na uzoefu na kujengeana uwezo ili kuchochea ukuaji wa biashara na vipaji; na
Kuunganisha sauti kudai mageuzi makubwa katika uchumi wetu yenye lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa vijana ikiwemo uwepo wa miundombinu wezeshi kwa biashara, urahisi wa kupatikana kwa mitaji, unafuu na urahisi wa kulipa kodi, ada na tozo, na uwepo wa sera na sheria rafiki kwa vijana hususani wajasiriamali wa wadogo na kati.
2.2 Kanuni za Azimio la Kagera
Azimio la Kagera linaongozwa na kanuni kuu tatu muhimu zenye kuchagiza Mapinduzi ya Fikra na Mageuzi ya Kiuchumi. Kanuni hizo ni kuanzia sokoni, ubunifu na ujasiriajamii. Zinafafanuliwa hapa chini.
2.2.1 Kanuni ya Kuanzia Sokoni
Dhana ya kuanzia sokoni inahimiza kuacha kufanya biashara kwa mazoea na badala yake kuenzi matumizi mazuri ya utafiti na taarifa juu ya hali ya soko na mahitaji kabla ya uamuzi wa kuanzisha shughuli ya kipato na biashara. Matumizi mazuri ya teknolojia ya habari na mawasiliano ni nyenzo muhimu ya kupata taarifa za soko na kuyahudumia mahitaji hayo kwa ubunifu na kujitofautisha.
2.2.2 Kanuni ya Ubunifu
Dhana ya Ubunifu inasisitiza kwamba, badala ya kuigiza biashara za jirani zetu, yafaa kubuni mbinu na bidhaa mpya kwa lengo la kuongeza urefu wa mnyororo wa thamani wa bidhaa au huduma ya mwingine ambaye ametangulia sokoni. Yaani, kama ambavyo tunaongeza njia kwa kufyeka vichaka na mapori mapya badala ya kupitia njia ile ile waliyopitia wenzetu, ni vivyo hivyo kwa ubunifu katika biashara.
Kuna tofauti ya msingi kati ya ubunifu wa kuigiza na ubunifu wa kuunda kitu kipya. Katika ubunifu wa kuigiza, mbinu za kutatua tatizo zinazotumika huazimwa kutoka kwa majirani zetu. Na kwa upande mwingine, katika ubunifu wa kuunda kitu kipya, mbinu za kutatua tatizo zinazotumika huundwa kwa mara ya kwanza, kwa maana kuwa, hazipatikani mahali pengine popote duniani.
2.2.3 Kanuni ya Ujasiria-jamii
Ujasiriajamii ni mchakato wa kufungamanisha nguvu za serikali, soko na jamii katika namna ambayo inatoa uhuru zaidi kwa watendaji walio katika asasi za kiraia kubeba majukumu ya huduma za kijamii ambazo hapo awali zilikuwa zinatolewa na serikali, na hivyo watendaji walio katika asasi za kiraia kupata fursa ya kujiongezea kipato kwa njia hiyo. Huduma hizo ni pamoja na usafi wa mazingira, kutunza watoto wadogo, kusomba taka ngumu, kutunza mazingira, kusambaza maji safi na salama, na kuendesha hudumza wa vituo vya watoto wa chekechea.
2.3 Nguzo za Azimio la Kagera
Azimio la Kagera limesimama juu ya nguzo tano ambazo zitawezesha kufanikiwa kwa utekelezwa wa Azimio hili. Nguzo hizi nne ni: uimara wa taasisi za malezi ya kijamii, matumizi ya tekinolojia ya kisasa, ubora wa nguvu kazi, ujenzi wa uwezo wa mtu mmoja mmoja, mabadiliko katika mtazamo wa maisha.
2.3.1 Taasisi imara
Taasisi kama familia, shule, dini zina mchango wa pekee na zinapaswa kutimiza wajibu wao kikamilifu. Kwa upande mwingine, taasisi za Serikali zina wajibu wa kuwezesha vijana kutimiza ndoto zetu na wajibu wetu kwa taifa. Tunadai mabadiliko katika uendeshaji wa taasisi za Serikali ili ziwe wezeshi na sio kikwazo. Tunataka Taasisi zinazofungua milango badala ya kujenga kuta, Taasisi zinazotufuata badala ya kutukimbia, Taasisi ambazo kipaumbele chake ni kutoa huduma badala ya kuadhibu na Taasisi zinazojivunia kulea biashara badala ya kufurahia kuzifungia.
2.3.2 Tekinolojia ya kisasa
Kwa wastani, tayari dunia inaendelea kushuhudia mabadiliko makubwa na ya haraka kutokana na matumizi ya tekinolojia momboleo. Kwa mujibu wa historia ya dunia, ujio wa uchumi wa viwanda ni zao la mapinduzi ya viwanda yaliyopitia katika hatua nne mpaka sasa. Kuna mapinduzi ya kwanza mpaka mapinduzi ya nne.
Kwa ufupi, kila zama za mapinduzi ya viwanda ni kipindi cha historia ya wanadamu ambamo kulitokea mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa sababu ya ugunduzi maalum wa kiteknolojia.
2.3.2.1 Mapinduzi ya Kwanza ya Viwanda, 1765-1870
Mapinduzi ya kwanza ya viwanda kilikuwa ni kipindi ambamo makaa ya mawe, maji na injini za mvuke wa maji vilitumika kama vyanzo vya nishati ya kuendesha uzalishaji kimakanika. Katika mtindo huu mpya wa uzalishaji nafasi ya kilimo ilichukuliwa na karakana na viwanda kama mfumo mpya wa kiuchumi katika jamii. Mapinduzi haya yalitokea kati ya 1765 na 1870 huko Ulaya na Amerika. Katika kipindi hiki, jamii za wakulima na vijiji viligeuka kuwa viwanda na miji. Viwanda vya chuma na kusokota nguo, pamoja na injini ya kutumia mvuke wa maji, vilikuwa ni uti wa mgongo wa uchumi katika kipindi hiki.
2.3.2.2 Mapinduzi ya Pili ya Viwanda, 1870-1914
Mapinduzi ya pili ya viwanda kilikuwa ni kipindi ambamo umeme, gesi na mafuta vilikuwa ni vyanzo vikuu vya nishati iliyotumika kuendesha uzalishaji kimakanika. Nishati hizi zilichochea kubuniwa kwa injini inayofanya kazi kwa kuunguza mafuta na gesi na hivyo kuboresha uzalishaji.
Katika ulaya na Amerika mapinduzi haya yalitokea kati ya mwaka 1870 na 1914, muda mfupi kabla ya vita kuu ya pili ya dunia. Kilikuwa ni kipindi cha maendeleo ya viwanda vya awali na upanuzi wa viwanda vipya, vikiwemo viwanda vya chuma, na uhandisi wa kikemia uliozalisha nyuzi na vifaa vya plastiki bandia, rangi na pembejeo za kilimo.
Mageuzi makubwa ya kiteknolojia katika kipindi hiki yalihusisha simu ya upepeo, simu ya waya na balbu za umeme. Aidha, miundombinu ya usafiri iliboreshwa kutokana na kubuniwa kwa magari na ndege mwanzoni mwa karne ya 20.
Ugunduzi wote huu uliwezekana kutokana na kuelekeza nguvu katika utafiti na kuwekeza mitaji iliyosimamiwa kwa kutumia modeli modeli mpya za utawala na uongozi wa uchumi wa viwanda.
2.3.2.3 Mapinduzi ya Tatu ya Viwanda, 1969-leo
Mapinduzi ya tatu ya viwanda, au Mapinduzi ya Kidigitali, ni kipindi ambamo vifaa vya kielektroniki na kompyuta vinatumika kuendesha mitambo ya uzalishaji badala ya binadamu, na ambamo nishati ya nyuklia inatumika kama chanzo kipya cha nguvu za kuendesha mitambo kimakanika.
Hiki ni kipindi ambamo kuna maendeleo ya kuteknolojia yanayoendana na kuachana na matumizi ya vifaa vya elektroniki vya kianalogia kwenda kwenye vifaa vya elektroniki vya kidigitali. Huko Ulaya na Marekani, kipindi hiki kilianza tangu 1969, kikaimarika katika miaka ya 1980 baada ya kompyuta ya mezani kugunduliwa, na sasa kinaendelea.
Katika kipindi hiki, ugunduzi wa kiteknolojia ni pamoja na kompyuta ya mezani, intaneti, na kufungamana kwa kompyuta na mawasiliano ya simu. Mapinduzi haya yaliambatana na kubuniwa kwa vifaa vya kielektroniki kama vile transista na maikrochipu.
Kwa sababu ya udogo wake, vifaa hivi vya kielektroniki vimesaidia katika kutengenezwa kwa vyombo vya kielektroniki vinavyosaidia katika kufungua milango ya utafiti katika anga la mbali na bayotekinolojia. Viwandani, vifaa hivi vya kielektroniki vimewezesha sehemu kubwa ya kazi za mikono kufanywa kwa kutumia mashine kama vile automatoni na roboti.
2.3.2.4 Mapinduzi ya Nne ya Viwanda
Na mapinduzi ya nne ya viwanda yanaanzia kwenye mapinduzi ya tatu, yaani mapinduzi ya kidijitali. Ni mapinduzi yanayohusisha matumizi ya mbinu mpya za kupenyeza tekinolojia katika jamii na pia ndani ya mwili wa binadamu. Kuna ugunduzi kama vile matumizi mapana ya roboti, matumizi ya akili bandia, nano-teknolojia, bayo-tekinolojia na magari yanayojiendesha bila dereva.
Kwa ujumla, katika “Zama za Kompyuta” maarifa na stadi zinazohusiana na masomo ya “Sayansi, Teknolojia, Elimu ya Uhandisi na Mahesabu,” au “STEM” kwa kifupi, ni nyenzo muhimu kwa ajili ya kuwafanya vijana wa kike na kiume kuwa sehemu ya uchumi wa viwanda.
2.3.3 Nuvu kazi bora
Nchi yetu bado inayo changamoto kubwa ya upungufu wa nguvu kazi yenye maarifa, weledi na mtazamo unaowiana na mabadiliko ya kifikra na kiuchumi tunayoyataka. Vijana tunaamini kuwa ili kuzikabili changamoto zilizo mbele yetu, mageuzi na uwekezaji mkubwa katika mfumo wa elimu na mafunzo yanahitajika. Sambamba na hilo, tunaamini kuwa lazima kama taifa tufanye uwekezaji wa kutosha kwenye Nyanja za sayansi, tekinolojia, uhandisi na mahesabu na utafiti ili kuwandaa vijana kuzikabili changamoto za kiuchumi na kijamii kwenye karne ya ishirini na moja.
2.3.4 Mitazamo mipya
Dunia inabadilika kwa kasi inayotulazimisha kubadili mitazamo yetu. Ndani ya karne mbili pekee tayari tumepitia katika zama nne za mapinduzi ya viwanda. Zamani, nchi yetu ilikuwa ni ya wakulima na wafanyakazi pekee. Lakini leo, Tanzania ni nchi ya wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wabunifu, wasanii, wavumbuzi na wanamichezo. Aidha, mitazamo tuliyonayo juu ya tekinolojia, mifumo ya uchumi, fursa, ajira, ujira na mafanikio ni vikwazo dhidi ya ukombozi wetu. Ili twende mbele, hatuna budi kuachana na tabia za kulalamika, kutamani mafanikio ya haraka, kutegemea miujiza na kubagua kazi. Ni wakati sasa wa kuwa na fikra na mitazamo chanya, kuona fursa kwenye vikwazo, funzo kwenye kukosea na matumaini kwenye kukata tamaa.
2.3.5 Ubora wa sera za uwezeshaji
- Sera huzaa sheria na huweka miongozo mbalimbali inayoathiri mwenendo wa uchumi kwa ujumla. Sera huumba na kuua fursa. Kwa ajili hiyo, Mapinduzi ya Fikra na Mageuzi ya Kiuchumi hayawezi kukamilika bila kuwapo mabadiliko ya sera ambazo ni kikwazo kwa ustawi wa vijana katika sekta za biashara, sanaa, ubunifu, uvumbuzi na michezo.
- Hivyo, hatuna budi kuunganisha nguvu zetu kudai kuwepo kwa mazingira mazuri ya kisera. Tunataka sera wezeshi zinazotoa urahisi kwa vijana kuanzisha biashara, kuifikia mitaji, kuondoa vikwazo vya kukua kwa biashara ndogo na kati, na kurahisisha ufanyaji wa biashara ya ndani na nje.
Tunaweza kusema bila kupepesa macho kuwa wajibu wa kwanza wa kulitekeleza Azimio la Kagera ni wetu sisi vijana. Hata hivyo, serikali na wadau wengine pia watahusika kwa yale mambo yanayoangukia katika wajibu wao. Hivyo, wajibu na majukumu ya utekelezaji wa Azimio la Kagera ni kama ifuatavyo:
3.1 Wajibu wa Vijana
- Kusaka na kuchangamkia fursa na maarifa kwa kadri ya uwezo wetu, na kuhakikisha hatumuachi kijana yoyote nyuma yetu katika safari ya Tanzania ya Uchumi wa Kati na Viwanda;
- Kutumia vizuri fursa ya TEHAMA kwa kubadilishana taarifa juu ya fursa zilizopo na kupunguza gharama za uendeshaji biashara.
- Kutanua na kurefusha mnyororo wa fursa kwa kuondokana na tabia ya kuigana na kuhujumiana, na badala yake kujenga utamaduni wa kushirikiana kwa kuungishana, na kwenda hatua moja zaidi ya pale ambapo ubunifu wa mwenzetu inaishia;
- Kutii na kufuata sheria na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kujiingiza katika shughuli halali za kiuchumi na kuwa mfano wa kuigwa kwa vizazi vijavyo; na
- Kulitangaza Azimio la Kagera na kulitumia kuunganisha nguvu za vijana wote kudai mageuzi ya kiuchumi, na mazingira mazuri ya kisera, kisheria na kitaasisi yatakayowezesha vijana kushiriki kikamilifu, katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na hatimaye uchumi wa kati.
- Kulitumia Azimio la Kagera kama rejea ya mijadala yetu ya kijamii na kitaifa kuhusu masuala ya kiuchumi, kuamsha ari na kutatua changamoto za vijana.
- Kuweka mazingira wezeshi ya kisera, kisheria na kitaasisi yanayochochea ustawi wa vijana na kuwawezesha kufikia kilele cha ndoto zao katika nyanja zote za maisha yao;
- Kuwajengea vijana uwezo kwa kupata stadi muhimu za kiuongozi, biashara na kitaasisi ili waweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya dunia;
- Kuhakikisha taarifa za kidunia kuhusu fursa za elimu, uendelezaji vipaji, biashara na uchumi zipatikanazo nchini;
- Kuchochea upatikanaji wa mitaji kwa vijana, kwa ajili ya biashara ndogo na kati, kwa kuweka sera zinazoshawishi taasisi za fedha za umma na sekta binafsi kukopesha vijana kwa masharti nafuu; na
- Kufanyia mapitio Sera, Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma na kuelekeza kuwa walau asilimia 30 ya manunuzi ya bidhaa na huduma yanayofanywa na serikali yatokane na biashara ndogo na za kati zinazomilikiwa na vijana.
- Kuunga mkono Azimio la Kagera kwa kuwekeza katika kubadili mtazamo wa kuwachukulia vijana kama soko badala ya kuwachukulia kama hazina ya sekta binafsi ya nchi yetu;
- Kuwekeza katika sekta ya uvumbuzi, ubunifu, sanaa na michezo ili kuendeleza na kuvuna mtaji wa vipaji miongoni mwa vijana, na kuwawezesha vijana kutafsiri vipaji vyao kutoka kuwa majaliwa na kuwa fursa za kibiashara;
- Kutoa fursa za mafunzo ya vitendo kwa vijana wabunifu, wasanii na wafanyabiashara ndogo na kati ili kuwajengea uwezo, ujuzi na maarifa ya kukuza shughuli na biashara zao;
- Kutenga na kufanya manunuzi yasiyopungua walau asilimia 30 ya bidhaa na huduma kutoka kwa wazalishaji, watoa huduma na wagavi vijana, ikiwa ni sehemu ya sera ya Uwajibikaji wa Makapuni kwa Jamii; na
- Kuandaa na kushiriki katika Tuzo ya Azimio la Kagera itakayotolewa kwa makampuni na taasisi zenye kutoa mchango mkubwa katika kusaidia utekelezwaji wa Azimio la Kagera.