"Azimio la JamiiForums-2015"

samsonp

Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
41
Reaction score
8
"Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe
tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena".

Katika utafiti wangu kwa muda wa miezi sita, hatimaye nimegundua kwamba, hakuna kipindi chochote tangu kuzaliwa taifa la Tanganyika 1961 na baadae Tanzania 1964 ambapo vijana wamefahamu wajibu wao katika Taifa lao la Tanzania. Vijana ni kundi kubwa ambalo linafikia karibu asilimia 70 ya watanzania wote. Ni nguvu kazi ya taifa inayokumbwa na changamoto lukuki.

Sio siri tena kwamba vijana ndio kundi pekee lililoshikilia ufunguo wa maendeleo ya namna yote ile Tanzania, kwa sababu hiyo, natangaza "AZIMIO LA JamiiForums".

Ndugu zangu awali nilipendekeza azimio ligawanyike katika maeneo makuu matano. Ni ukweli usiopingika kwamba wengi kwa sasa umri wetu ni kati ya miaka 18-35, kwa hiyo ifikapo mwaka 2050 watoto wetu na hata wajukuu tutahitaji waanze kula matunda ya kazi yetu katika taifa lao, kwa maana hiyo niligawanya katika makundi yafuatayo;

1. Tanzania ya 2050.
2.Mifumo shirikishi.
3.Maazimio ya vijana.
4.Mtandao wa vijana.
5.Hitimisho.

Ndugu wanajamiiForums, sasa ni kipindi cha kutoa maoni yenu tuliweke vipi Azimio letu ili tuweze kulikamilisha na tuanze kufumua huu mfumo wa kinyonyaji katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

TOA MAONI KWA KILA KITU; MUUNDO, JINA, NA MAMBO MENGINE YOTE...

KARIBUNI KWA MAONI KATIKA Azimio la JamiiForums..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…