Azimio La Arusha; Upande Wa Pili Wa Shilingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azimio La Arusha; Upande Wa Pili Wa Shilingi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Aug 6, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280

  Ndugu zangu,

  Pichani ni ushahidi wa kilichotokea miaka ya 70 wakati wa utekelezaji wa Azimio la Arusha na sera ya Vijiji Vya Ujamaa. Mabaki haya ya makazi ya wananchi wakati huo bado yanaonekana. Picha hiyo nimeipiga asubuhi hii takribani kilomita 8 kutoka katikati ya mji wa Iringa.

  Ni juu kileleni na kandokando ya mlima wa Gangilonga. Picha hii inatukumbusha tena umuhimu wa kusimulia hata yale mabaya yaliyotokea wakati huo ili tupate ya kujifunza wakati huu nchi yetu inaadhimisha miaka 50 ya uhuru.

  Kuna maswali ya kujiuliza; Je, kulikuwa na mapungufu gani katika fikra na utekelezaji wa Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji Vya Ujamaa?

  Ninayo ya kusimulia, kwa niliyoyaona, niliyoyasoma na niliyosimuliwa. Naamini, kuwa kuna wengine humu ' Kijijini' mwetu wenye ya kusimulia; mnakaribishwa, maana, hii nayo ni historia yetu.

  Maggid,
  Iringa, Agosti 6, 2011
  0754 678 252
  http://mjengwa.blogspot.com
   
Loading...