Azam tv

mnawaonea tu tcra. Wao wamewapa kampuni 3 tu haki ya kurusha channel za bongo mojawapo ni startimes na wenzake ambao wote wanatumia antena. Hawa wanaotumia madish mfano zuku,azam hawa hawapo kwenye huu mpango na ndo maana wanapatika mikoa yote{setellite} Hawa wengine ni lazima mkubaliane wenyewe kwa wenyewe mfano azam akubaliane na itv. Mfano mzuri ni dstv na wenyewe wanazo channel 3. Ingekuwa ni ruksa dstv wasingekubali kukosa itv nk. Huu ndo mtazamo wangu
 
AZAM,ZUKU NA DSTV hawawezi kurusha bila kibali cha wamiliki. TCRA walisisitiza juu ya hili ili watumiaji wasije kulaumu kama sasa.
kwa hiyo mvumilie mpaka watakapoamua kuziingiza huko mpate kuziona.
ni vema kutafiti kama unapenda vya nyumbani
 
AZAM,ZUKU NA DSTV hawawezi kurusha bila kibali cha wamiliki. TCRA walisisitiza juu ya hili ili watumiaji wasije kulaumu kama sasa.
kwa hiyo mvumilie mpaka watakapoamua kuziingiza huko mpate kuziona.
ni vema kutafiti kama unapenda vya nyumbani

"ni vema kutafiti kama unapenda vya nyumbani" KIVIPI?
 
Dawa ni kuwa na ving'amuzi vyote!zuku,ting,startimes,digitek,continental,dstv,azam N.K
 
Tanzania haina tofauti na danguro.sijui inaendeshwaje.tena danguro la uwanja wa fisi.
 
"ni vema kutafiti kama unapenda vya nyumbani" KIVIPI?

Wengi wakishanunua ndiyo wanaanza kulalamika channel fulani hakuna. ni vema kucheck kila kampuni ina channel gani, zikiwemo unazozihitaji, ndipo ununue.
 
Kwani local channel zina nini? au mnamiss mizengwe?

AZAM TV imenipa sababu ya kuanza tena kuangalia tv.
 
ngoja niwaulize swali nyie mnaowalaumu tcra. Mbona kwenye startimes,digitek,continental hakuna azam one?
 
Me nazuku yangu hata siwezi kutoka Nje kwani kwa zuku naridhika kabsaa.
 

mkuu nasikia azam tv wanatumia dish, kama kweli sheria haiwabani wanaotumia dish..
 

Yeah, you are right!
 
IPP media ndio wenye matatizo...mbona hata DSTV hawamo? Wanatia aibu
 

kwanini wawape kampuni tatu? Wakati Azam pia ni mzawa wa nchi hii kwanini na yeye asipewe upendeleo huo? Kuonyesha kwa dish, kuonyesha kwa antenna kuna ambaye anarusha channel zote bure au kugawa ving'amuzi free?
 
Jamani mnaotumia king'amuzi cha azam vipi upande wa soccer, tofauti na ligi ya vodacom wanaonyesha ligi gani nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…