Azam TV, Yanga wapambana Dar

Azam TV, Yanga wapambana Dar

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Azam TV, Yanga walumbana Uwanja wa Taifa Dar
images

azamtv.jpg

Mpiga Picha wa Azam TV akiwajibika uwanjani
images

VIONGOZI wa Yanga nusura wazuie Kituo cha Televisheni cha Azam kuonyesha laivu mechi baina ya Yanga na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Azam TV, ambayo ilianza kurusha matangazo yake kupitia televisheni ya Taifa (TBC1) juzi Jumamosi baina ya Simba na Ruvu Shooting ilijiandaa pia kuonyesha mechi ya jana Jumapili kati ya Yanga na Mtibwa kabla ya kuzuiwa kwa muda na viongozi wa klabu ya Jangwani
Hata hivyo, Azam TV ilionyesha mechi hiyo kipindi cha pili, licha ya viongozi wa Yanga kutishia kuwa mashabiki wao wangefanya vurugu iwapo mechi hiyo ingeonyeshwa.
Mratibu wa Azam TV, Patrick Kahemele aliliambia Mwanaspoti jana Jumapili jioni kuwa walifuatwa na viongozi wawili wa Yanga (anawataja) ambao waliwazuwia wasionyeshe mechi hiyo.
¡°Walituambia (viongozi wa Yanga) kuwa kama hatutaondoa kamera zetu, wangewaambia mashabiki wafanye vurugu, na hatukutaka shari, hivyo tukalazimika kuondoa kamera zetu kwa muda,¡± alisema Kahemele.
¡°Hata hivyo baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wetu wa juu wa Azam Media, wakatuambia kuwa tuonyeshe mechi kwa sababu tupo kazini na tuna mkataba rasmi,¡± alifafanua Kahemele.
Kahemele alisema licha ya kuanza kuonyesha mchezo huo kipindi cha pili hakukuwa na vurugu zozote na wamegundua kuwa viongozi wa Yanga wamekuwa wakiwasingizia bure mashabiki wao.
Yanga wamekuwa wakigomea kusaini mkataba ambao klabu nyingine 13 zilisaini kwa ajili ya kuonyeshwa laivu kwa mechi za Ligi Kuu Bara na kituo cha Azam TV.
Wakati kila klabu ikipewa Sh100 milioni, Yanga ilisusia kiasi hicho kwa madai kuwa ni fedha ndogo na hasa ukizingatia kuwa ina mashabiki wengi nchini.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah alisema watakutana kujadili suala hilo, lakini akasisitiza kuwa Azam TV wanaruhusiwa kuonyesha mechi zote za Ligi Kuu wanazotaka.

M_SPOTI
 
Yanga waseeeeeeeeeee.............la kwani hao nani ktk nchi hii?pmbv clipendi hili litimu la ccmauaji
 
yanga wamevurugwa hizi ndiyo timu za kipuuuuuuuuuzi zinazorudisha maendeleo ya soka
 
Mtu yeyote mwenye uwezo wa kufuatilia utatuzi wa migogoro (conflict resolution) angejua haya yangetokea. Kwa sababu TFF iliahirisha tatizo badala ya kulitatua. Kuwaambia Yanga na Azam TV wamalizane ilhali kila upande una mtizamo tofauti unaozaa msimamo tofauti ni TFF kutambua kuwapo kwa tatizo (ndio, tatizo sio changamoto) lakini ikajivua kwenye wajibu wa kulitatua. Iweje mlalamikaji na mlalamikiwa wakamalizana bila ya kuwapo msuluhishi? Ni kwenye sheria ya porini tu ya mwenye nguvu mpishe ndiko hilo linakowezekana. Ndio kinachoendelea sasa hivi. TFF amekaanga mbuyu, anawaachia Azam TV na Yanga watafune!
 
Hakuna kitu kibaya kama hicho wale jamaa wanamkataba tayari . Pale yanga wakifanya fujo za kuharibu vifaa vya azam hawataweza kulipa kwani kamera moja inagarimu dola 18000 hadi dola 20000. Wakae mezani waelewane ili sisi wadau tufaidi.
 
Hakuna kitu kibaya kama hicho wale jamaa wanamkataba tayari . Pale yanga wakifanya fujo za kuharibu vifaa vya azam hawataweza kulipa kwani kamera moja inagarimu dola 18000 hadi dola 20000. Wakae mezani waelewane ili sisi wadau tufaidi.
bosi...hiyo lens tu ni dola 114,000 kwa hiyo camera na lens ni kama 150,000 usd
 
Hakuna kitu kibaya kama hicho wale jamaa wanamkataba tayari . Pale yanga wakifanya fujo za kuharibu vifaa vya azam hawataweza kulipa kwani kamera moja inagarimu dola 18000 hadi dola 20000. Wakae mezani waelewane ili sisi wadau tufaidi.
waambie washamba hao...:A S-confused1:
 
Back
Top Bottom