Azam Tv vifurushi vyenu havieleweki

vngenge

JF-Expert Member
Apr 19, 2011
539
270
Katika matangazo yenu ya mabadiliko ya bei za vifurushi mmeonesha kifurushi cha Azam plus ni Tsh 23000. Ndani ya kifurushi hicho inaonekana clouds plus ni kati ya channel zilizomo. Lakini unapolipia hiyo channel haionekani, huu ni ulaghai. Simu zenu huduma kwa wateja haziiti.
 
Mimi nililipia tarehe 30 mwezi wa nane 15000/= lakini kufikia tarehe 11 mwezi wa tisa wamekata.... Simu yao sio tu haipatikani hata kuita haiiti.

Hawa jamaa nilikuwa nawaamini sana...lakini sasa hivi duh.!
 
kinachopendwa sana huwa na tabia ya kuringa sana.Azam acheni maringo huu wakt wa sasa ni wakiushindani,kaeni chonjo..tunaotumia AZAM kwa sasa,tulikuwa tukitumia ving'amuzi vingine hivyo muwe makini,acheni midenguo wakt wa sasa..kama hotel zinageuzwa kuwa hosteli mjue huwa wakati si wa maringo..ni hayo tu.
 
Nililipa Tsh 15,000 tarehe 04/09/2017
Account 212985419406
TransID 491424027713
Reference 0188463471
Receipt 11208116
Channel hazikupatikana.
Nilipiga simu huduma kwa wateja hazipatikani.
Baadae nikaenda kwa wakala wao nikajibiwa kuwa malipo ni 18,000 hivyo niongeze 3,000 ili kuibust ile 15,000.
Baada ya malipo hayo kufanyika hakuna cha channels wala Radio,cha ajabu salio linasoma 3,000/=.
Baadae nikarudi kwa wakala,alichofanya ni kuwatumia ujumbe wa barua pepe juu ya malipo na kuambatanisha email ili nipatiwe mrejesho.
Nimesubili lakini sioni mrejesho wowote,nilichofanya ni kuongea na mtandao wa simu ulipofanyika mhamala wa 15,000/ nilihakikishiwa kuwa malipo yalikwisha pokelewa nna Azam TV.
 
hicho cha Clouds plus hata ulipe kifurushi cha 28,000 hupati???? lazima uilipie kivyake kwa 3,000!! huu si uhuni??
Heeee. Ndio maana hivyo kina bei yake mana mi pia nalipia hicho cha 28 lakini siipati hiyo clouds plus.

Ila huu ni usanii wa hali ya juu.
 
Mimi nililipia tarehe 30 mwezi wa nane 15000/= lakini kufikia tarehe 11 mwezi wa tisa wamekata.... Simu yao sio tu haipatikani hata kuita haiiti.

Hawa jamaa nilikuwa nawaamini sana...lakini sasa hivi duh.!
Wamelewa wingi wa wateja sio bure.
 
Katika matangazo yenu ya mabadiliko ya bei za vifurushi mmeonesha kifurushi cha Azam plus ni Tsh 23000. Ndani ya kifurushi hicho inaonekana clouds plus ni kati ya channel zilizomo. Lakini unapolipia hiyo channel haionekani, huu ni ulaghai. Simu zenu huduma kwa wateja haziiti.
kifurushi cha clouds plus kiilipoanza kilikuwa ni kama kinaoneshwa kama channel za nyumbani nyingine (nilivyoelewa mimi) ghafla msimu wa fiesta ulipoanza kikaanza kulipiwa kipekee - sh.3,000 ndio ukipate. Najaribu kuwaza mwenyewe, ndivyo kitakavyokuwa siku zote au msimu wa fiesta ukiisha kitarudishwa kama awali?
 
0764700222 hii huduma kwa wateja azam tv inapatikana ila pia ni vizuri ukilipia kupitia simu yako maana kuna wakati nililipia kwa wakala 28,000/= kumbe wakala kalipia cha 23,000/= nilikuja kugundua baadaye ila alinirudishia 5,000/=
 
AZAM TV ni wezi na matapeli wakubwa sasa. Ni bora uwe na DSTV tuu hata ukilipia 40000 haitakuuma, coz utapata huduma consistent siyo ubabaishaji.

Mwenyew nawahama soon mbweha hao
 
Back
Top Bottom