Azam TV na Ndondo Cup, maamuzi ya nani?

Rio Tinto

JF-Expert Member
Sep 18, 2014
777
451
Wakuu,

Mwaka jana nilifanya maamuzi magumu ya kuweka kando kinga'amuzi changu cha DSTV na kuchukua AZAM TV nikiamini itakata kiu yangu ya Soka maana mimi kwenye TV huwa naangalia vitu viwili tu; Taarifa ya Habari na Soka... Lakini toka nimejiunga nao nimeishia kuwa disappointed.

Mwanzo walikua na Vision nzuri ila walipoanza kuokota watu ambao sio professional na wasio na vision wamepoteza mwelekeo kabisa na msumari wa mwisho wa kaburi la Azam Tv ni maamuzi yao kuonyesha michuano ya uchawi na uswahili uswahili NDONDO CUP, yaani aliyewashauri amewaingiza mkenge especially wakati huu ambao kiu ya wadau wengi wa soka ni EURO 2016 na COPA AMERICA....

Kiufupi nimeamini wa mbele siku zote ni wa mbele, DSTV wataendelea ku dominate the market kwa sababu tunaendekeza uswahili uswahili kwenye mambo yanayohitaji professionalism.

Anayetaka kinga'amuzi changu cha AZAM TV ani PM maana nakitoa bure kabisa..
 
Tule Ice cream na juice na chapati za Azam...chezea DSTV wewe....utakula maandazi bila chai.......wajipange....
 
Toka awali niliamua kutohamia Azam. Nimeendelea kubaki na Dstv yangu. Pole sana mkuu.
 
Una lako Jambo sio bure! Azam umetoa mwanga sana hapa Tanzania. Mbio za Magari mambo kedekede wewe umeona Ndondo cup tu? Au umeumia Azam kushirikiana na Clouds? Ukweli ubaki ukweli fitina hazijengi, na wewe unacholeta hapa ni fitina hata dini zote hazipendi.
 
Yan hawa azam bure kabisa wabakie kwenye game zao zao quran tu mana ukizaliwa nguruwe hupaswi kuomba mabawa wa nchi kavu haendi angani
 
Yan hawa azam bure kabisa wabakie kwenye game zao zao quran tu mana ukizaliwa nguruwe hupaswi kuomba mabawa wa nchi kavu haendi angani

Duu umefika hadi kwenye dini mjomba!!..yaani mtu awekeze pesa zake kwenye biashara zake we unakereka??..mbona simple tu mjomba huridhiki na huduma zao nenda dstv wala huna sababu ya kukwaza imani za watu!!.
 
Duuuuuuuuuuu kuonyesha ndondo cup ndo uswahili na uchawi?????
Unataka kuniambia Euro na Copa america ni michuano ya utakatifu na uzungu eeeeeee????
Ulikuwa na lengo zuri sana la kuanzisha huu uzi but umechemka kupanga na kichagua maneno yako.......Punguza jazba then edit post yako
 
Wakuu,

Mwaka jana nilifanya maamuzi magumu ya kuweka kando kinga'amuzi changu cha DSTV na kuchukua AZAM TV nikiamini itakata kiu yangu ya Soka maana mimi kwenye TV huwa naangalia vitu viwili tu; Taarifa ya Habari na Soka... Lakini toka nimejiunga nao nimeishia kuwa disappointed.

Mwanzo walikua na Vision nzuri ila walipoanza kuokota watu ambao sio professional na wasio na vision wamepoteza mwelekeo kabisa na msumari wa mwisho wa kaburi la Azam Tv ni maamuzi yao kuonyesha michuano ya uchawi na uswahili uswahili NDONDO CUP, yaani aliyewashauri amewaingiza mkenge especially wakati huu ambao kiu ya wadau wengi wa soka ni EURO 2016 na COPA AMERICA....

Kiufupi nimeamini wa mbele siku zote ni wa mbele, DSTV wataendelea ku dominate the market kwa sababu tunaendekeza uswahili uswahili kwenye mambo yanayohitaji professionalism.

Anayetaka kinga'amuzi changu cha AZAM TV ani PM maana nakitoa bure kabisa..
Naounga mkono hoja na japo mie Ndondo Cup pia naipenda
 
Azam Media ndio kampuni bora kabisa kifedha,kiuweledi,kimkakati,kimtazamo na mengineyo kuhusiana na Television hapa Afrika Mashariki na Kati.
Ndondo cup inawadhamini na ndio waliyopelekea leo uione na kuifahamu hiyo Ndondo.
Nawe waweza kwenda na fungu lako kisha wakaonyesha kile utakacho hapo kwako.
 
Sijaona waliposhindwa. Azam Tv wako vizuri sana, na kwa umri wao wa miaka mitatu hivi wameonyesha wanaweza kufika mbali sana na kuuchallenge utawala wa Dstv ambayo bei yake ni kubwa sana kwa mwananchi wa kawaida
 
Una lako Jambo sio bure! Azam umetoa mwanga sana hapa Tanzania. Mbio za Magari mambo kedekede wewe umeona Ndondo cup tu? Au umeumia Azam kushirikiana na Clouds? Ukweli ubaki ukweli fitina hazijengi, na wewe unacholeta hapa ni fitina hata dini zote hazipendi.
Kanyela Mumo naona umekunya kabisa.
 
Wabongo bhana vya bure vitawaua sasa unaringanisha Azam na Dstv wap na wapi hivj unadhani Azam akipata highlights za epl utaoneshwa mpira kwa 25000 upuuuzi huu thread closed
 
Najuta mkuu nasubiri mwezi nane nichukue DSTV sitaki stress tena
Wenye pesa hawatoi mapovu, kula ugali na dagaa ukalale, acha kutupigia kelele unatuamsha. Tumepumzika tunawaza kuongeza pesa zaidi. Sawa mtoto wa mama kula kulala?
 
Back
Top Bottom