Azam Tv mnakera sana kwa hili

Director D

Senior Member
Feb 24, 2016
192
229
Kama umewahi kuangalia mechi za ligi kuu ya Tanzania Bara (VPL) kupitia Azam Tv kuna kitu huwa kinanikera sana hawa jamaa (waendesha matangazo ya mpira kutoka Azam Tv) hufanya pale timu yao Azam Fc inapocheza na timu yoyote pinzani inapotokea Azam ikafungwa goli hata siku moja hawa jamaa huwa hawarudii kuonyesha hilo tukio (goal) lilivyofungwa ila wao

Azam wakifunga tena goli likiwa zuri hurudiwa hata zaidi ya mara tano kama kuna wadau wa mpira wetu wa kibongo na ni wafuatiliaji wazuri watakuwa wamewahi kuliona hili.

Najiuliza Ikiwa Azam TV ndio walipewa mkataba wa kuonyesha ligi, kwa nini wanafanya hili, kama ni hofu ya kuogopa kuonyesha udhaifu wao wanapokosea hapo wanafeli kwa kuwa hata wenzetu walioendelea kisoka hawafanyi upuuzi kama huu.

Azam TV Badilikeni wadau tumeshagundua michezo yenu.
 
Wanakera sana hawa jamaa msimu ujao hii tenda wapewe watu wengine, watangazaji wa AZAMU wengi hawana ROHO ngumu hata jana mm sio simba ila jamaa alishika kabisa ila hawakurudia tuone tena wanakuja kutuonesha boko alivyokosa goli, yaani ukiwasikiliza unatamani uvunje Tv
 
Back
Top Bottom