Azam Tv, kweli hii ni haki?

Azam Tv, kweli hii ni haki?

albertdaud29

New Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
4
Reaction score
8
Lini matamko yanayotolewa nchini yatakua ya uhakika? Yaani mwezi ukiisha tu lazima nilipie hata kwa steshen za ndani ya nchi.

Sasa AzamTv mtatumaliza maana hizo stesheni zilizokua bure sasa ni 500 kila siku.
 
Lini matamko yanayotolewa nchini yatakua ya uhakika? Yaani mwezi ukiisha tu lazima nilipie hata kwa steshen za ndani ya nchi.

Sasa AzamTv mtatumaliza maana hizo stesheni zilizokua bure sasa ni 500 kila siku.
Azam TV haijasajiliwa Tanzania, hivyo haibanwi Na Sheria za kuonyesha local chaneli bure....

Azam TV ni sawa tu DSTV.
 
Nilishaachana na Azam maana wana uswahili mwingi kuanzia kwenye vifurushi mpaka kila kitu
Tunapenda uzalendo lakini kiukweli hawa jamaa hawafai na huenda katika ushindani huu sio ajabu wakaondoka sokoni.
 
Eti king'amuzi kimeisha na nimeongeza pesa na kuonekana imelipwa lakini ni siku ya sita sasa stesheni hazionekani. Nimejaribu kupiga hizo namba zao za Voda na Airtel (nadhani) zinaita tu na kukatika kwa siku zote hizi. Sasa leo wakati naendelea kujaribu nakadhani nimepata bahati kumbe ni sauti imerekodiwa!!
Unajua ni nini hiyo sauti inasema!!??? ....eti; "samahani leo ni sikukuu, tupigie kesho".

Ndio nikajiuliza kama kweli media house iliyosajiliwa to deliver 27/7 services wanajibu hivi ni sahihi!???
Hawa jamaa watabaki kuwapata watu wa aina fulani tu wasioelewa wanachokitaka!
 
Azam TV haijasajiliwa Tanzania, hivyo haibanwi Na Sheria za kuonyesha local chaneli bure....

Azam TV ni sawa tu DSTV.
Lo, sikulijua hili pia.
Alafu ukiangalia hata jinsi ya kulipia wenyewe inabidi uongeze pesa zinazolingana na kifurushi husika zote wakati startimes hata ukiwa na buku mbili wanaipokea kwa proportional ya unacholipia!
Sioni wakienda mbali sana na hasa ukichukulia wanavyoifanyia promo starttimes kupitia ile channel ya PL.
 
Mbona kuna decoda zisizo za kulipia na channel kibao...
ACHANA NAO HAO WAFANYA BIASHARA TU
 
Mbona kuna decoda zisizo za kulipia na channel kibao...
ACHANA NAO HAO WAFANYA BIASHARA TU
Yaani imeniacha na maswali mengi, eti tupo sikukuu!
Ngoja naanza kufuatilia kama kweli sikukuu zote bwanakuwa hawapatikani. Na kama ni hivyo basi wafunge hata mitambo yao siku za sikukuu ili tusiwasumbue lakini nao wasitusumbue. Najiuliza kama maamuzi haya yamepitishwa na Ndugu Tiddo Mhando mtu ambaye amefanya kazi miaka mingi kwenye chombo kinachoelewa maana halisi ya 24/7.
 
Nenda Star Times Chukua Decoda Ya 20000/-
Mwezi Mmoja Offer Halafu Unalipa 6000/- Kwa Wiki Mbili
 
Back
Top Bottom