CEO wa AZAM TV.Tido Muhando anahojiwa muda huu yupo live akihojiwa na Patrick Nyembera.
Kwamba kuanzia Tarehe 10th August wataonyesha La Liga Liveeeee(Spanish League)
AZAM imepata haki miliki ya kuonyesha Mechi zoote za LA LIGA
TIDO,anasema kwamba alikutana na Uongozi wa La Liga DUBAI,na kuwaambie uwezo wa AZAM TV.
Na haikuwa kazi rahisi kupata Haki miliki kwa kuwa jopo la La Liga lazima lijue uwezo wa Kituo husika na ubora wake.
Ilichukua muda mrefu saana tangu wawasilishe maombI yao,hatimae yamekuwa
Amegusia tena kuhusu Arsenal TV,wapo kwenye mazungumzo hatua za mwisho na amesema kuna uwezekano wa kupata haki miliki ya kuonyesha mechi zao muda sio mrefu.
Manchester United na Liverpool wapo kwenye mazungumzo na yanaendelea vizuri.
Amegusia Tena Kuhusu EPL,wapo kwenye mazungumzo nao,Uongozi mkuu wa AZAM TV ulitoka na kuwafuata viongozi wa EPL UK.
TIDO anakiri kwamba nikazi kubwa zaidi kwa hili,lakini amesema watafika hatua nzuri tu.
AZAM TV ndio habari ya MJINI