Azam TV inapeta, wengine wanachechemea

Azam TV inapeta, wengine wanachechemea

Sungurawembe

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
414
Reaction score
55
Wakuu habari zenu
Jana nimekuta mtu mmoja anatafuta king'amuzi cha Azam TV wakati ana kingine startimes sikupata jibu leo nimepata, pamoja na CCM kutangaza kumtambulisha mgombea mteule wao leo, Ni azam two pekee imerusha matangazo ya papo (LIVE) kutoka Mbagala Zhakeem. Media nyingine wapo na mambo yao tu kama hawajui wateja wao wanakimbia kwani katika local channel Azamtv haimo huwezi kuwapata bila king'amuzi chao. Ni muda wa kumpa hongera Tido Muhando kwa ubunifu wake hakika ataipaisha sana media hiyo.
 
Incase hukujua,
Hawaoneshi bure!!
 
Miaka mitano ijayo Azam atakuwa levels nyingine.
Aboreshe na aangalie wateja wake wanataka nini na kuwatimizia.
 
Pia wamepata haki ya kuonesha la liga
Mkuu hii ilikuwapo kwenye Channel baadhi ila kama wamepata haki ya moja kwa moja ni wazo zuri pia.

Nasubiria Manchester United na Liverpool ambazo wameingia nazo mkataba,ila sijui kama mechi zao zitakuwa zikionyeshwa.
Wacha tusubirie msimu uanze tuone
 
Azam TV hongereni sana, angalau napata faraja kuona Chanel ya nyumbani ikiwa Na viwango vya kimataifa, Bravo!
 
Imagine live coverage inaongozwa na Charles Hillary, Taji Liundi na Kamuntu , huku Tido akiwa pembeni kufatilia viwango ..... wanatisha sana Azam tv .....

Hata habari zao ni live kweli kweli ... mahojiano katikati .....kwenda live hata na maripota wa mikoani ......safi sana ...
 
Zanzibar Spices

Nyuzi zinazohusu azam TV lazima uwepo..

Hahahah,mkuu unajua chanzo cha mie kukubali Azam,ni pale Nilipohama Simba Rasmi na kuwa AZAM FC.
Baada ya blaablaa za simba na AZAM kufanya vizuri nikawa shabiki mkubwa saana wa AZAM Team yenye malengo.
Hata hapa home nina jezi almost matoleo yoote ya AZAM TEAM,tena huwa nikija Dar naenda kununua pale AZAM COMPLEX.

So,kuanzia muda huo,nimekuwa nafuatilia kila wanachofanya kwenye products zao za TEAM na TV.

Mie nina Startime na pia ZANZIBAR CABLE,ila nimeviweka chini nimepandisha AZAM tangu walipoanza huduma,wiki ya mwanzo tu mie nikawa nimenunua Dekoda yao,hadi sasa sijuti kuwa na AZAM Dekoda.

Napendelea saana kufuata kitu chenye mabadiliko yanayoonekana na sio yanayoandikwa kwenye Magazeti.

Mfano ni kama AZAM Team inafanya yao bila kuwa na ushabiki wa magazeti,Simba na Yanga wao kila siku ni kuletea wachina wa Kilosa eti wapima uwanja,ebbo

Ukienda kwenye AZAM Tv kule unakuta almsot kila Mwezi ni sapraiz za ajabu na maendeleo ya kasi sana kwenye tasnia ya habari.

Sasa Mabadiliko haya ndio mie nataka kuyaona na sio ya kuandika magazetini kila siku wakati uhalisia hakuna.

Ndio maana mkuu unaniona saana kwenye nyuzi za AZAM,maana ni shabiki wa AZAM Team na AZAM TV kwa ujumla.
 
Ni ukweli mtupu. Hata Mimi nikipata kahela mwisho wa mwezi naondoa huu uchafu niliofunga naweka azam. Kweli wanastahili pongezi siwezi kila uchao kuanzalia habari kwa jirani hadi naonekana kero!! Mko wapi akina Charles Hilary?? Safi sana
 
Hahahah,mkuu unajua chanzo cha mie kukubali Azam,ni pale Nilipohama Simba Rasmi na kuwa AZAM FC.
Baada ya blaablaa za simba na AZAM kufanya vizuri nikawa shabiki mkubwa saana wa AZAM Team yenye malengo.
Hata hapa home nina jezi almost matoleo yoote ya AZAM TEAM,tena huwa nikija Dar naenda kununua pale AZAM COMPLEX.

So,kuanzia muda huo,nimekuwa nafuatilia kila wanachofanya kwenye products zao za TEAM na TV.

Mie nina Startime na pia ZANZIBAR CABLE,ila nimeviweka chini nimepandisha AZAM tangu walipoanza huduma,wiki ya mwanzo tu mie nikawa nimenunua Dekoda yao,hadi sasa sijuti kuwa na AZAM Dekoda.

Napendelea saana kufuata kitu chenye mabadiliko yanayoonekana na sio yanayoandikwa kwenye Magazeti.

Mfano ni kama AZAM Team inafanya yao bila kuwa na ushabiki wa magazeti,Simba na Yanga wao kila siku ni kuletea wachina wa Kilosa eti wapima uwanja,ebbo

Ukienda kwenye AZAM Tv kule unakuta almsot kila Mwezi ni sapraiz za ajabu na maendeleo ya kasi sana kwenye tasnia ya habari.

Sasa Mabadiliko haya ndio mie nataka kuyaona na sio ya kuandika magazetini kila siku wakati uhalisia hakuna.

Ndio maana mkuu unaniona saana kwenye nyuzi za AZAM,maana ni shabiki wa AZAM Team na AZAM TV kwa ujumla.

Zanzibar Species
Nimekusoma vilivyo...pamoja sana..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom