Azam Tv hamtendi haki katika kuonesha mpira

moodykabwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
625
602
NA MOODY KABWE

Yale aliokuwa anayasema mwenyekiti wa YANGA AFRICA BW YUSUFU MANJI

Nimeaza kuyaona leo nlikuwa natazama mpira kati ya MTIBWA SUKARI vs AZAMFC MAARUFU MAKONTENA FC

Kiukweli sikuvutiwa na namna mpira unavyoneshwa katika kituo hicho na si leo tu ila leo imezidi sana na ukichanganya na malalamiko ya wadau wa soka inajizihirisha zahiri kuwa ule ubora wa ligi tuliotegemea kuuona katika runinga hatuone sasa na hii ni moja ya timu moja tu ikicheza na timu nyingine


Leo mtibwa alikuwa anacheza na azamfc maarufu makontena fc

Mechi hii ilikuwa inarushwa live na kituo cha michezo AzamTv
Ila cha kushangaza nipale Timu yao inapofanya makosa yale mabaya ya kimchezo hayaoneshwi huonesha mazuri tu tena hurudia mara tatu mda mwingine mara 6 mpaka 7

Ila mpinzani wake akifanya vibaya basi mabaya yake huoneshwa na kuchagizwa na mtangazaji wao Hasany Mvula kwa maneno ya kubeza huku akiisifia zaidi Timu yake ya azamfc maarugu makontena fc

Nini kimenifanya niandike haya
Kwanza
Nawapongeza mtibwa wameojesha

Upinzani mzuri wa soka

Kwa waliotazama mpira kati ya MTIBWA vs AZAMFC maarufu MAKONTENA FC
wameshuhudia wenyewe

Tukio alilofanya nditi halikurudiwi katika Tv yao ila goli.la Boco lilirudiwa zaidi ya mara 6 kiuhalisia tu ninamna gani uonevu bado upo ndani ya AzamTv katika kuonesha mpira live

Kitu kingine kinachokera kuangalia mpira katika Tv hii ni hawa wachambuzi wao Edo kumwembe vs Jeffu Lea

Hawa jamaa kama Azamfc maarufu Makontena Fc inacheza na timu nyingine hutawaona wakiwapatia watazamaji usawa wa uchambuzi wa Timu zote zinazocheza wataichambua tu azamfc maarufu makontena fc sasa hapa ndiyo unajiuliza hii timu nyingine inayocheza na timu yao haina nafasi ya kujadiliwa au nashauri tu kama kwa mfano Toto Africa ancheza na mwadui fc bas wawatafute wachezaji wa zamani wa Timu hizo wachambue timu zao na wao huku wao wakiwepo kama wachambuzi wa soka sasa ila sio wao kuwepo peke yao kuzicbambua hizo timu kwasababu wanaelemea upande mmoja ili Watupatie laza sisi watazamaji basi wa Runinga tunaonunua vocha kwa ajili ya vingamuzi vyao ili Tupate laza ya mpira

Na huyu hasani mvula Anakera sana anaacha kutangaza mpira kwenda na matukio.ya mpira kazi yake kuisifia tu azamfc

Na kusahau majukumu yake ya kutangaza mchezo wa mpira

Ki uhalisia maneno ya mipasho mengi sana kama sio muandishi wa habari au mtangazaji wa mpira hata mtoto wa darasa la saba ukimuweka pale azamtv atangaze mpira hataongea mipasho kama anayosema mvula akitangaza mpira

USHAURI WANGU KWA AZAMTV

1) Badilisheni mfumo wenu wa kuegemea Timu yenu wakati muonesha mpira ili muendani na soko la wadau wa mchezo wa mpira

2) Huyu mvula hana sifa ya kutangaza mpira katika Tv ana mipasho sana kuliko uhalisia wa soka lenyewe na kurushia vijembe wachezaji wa timu nyingine

3) Azafc na AzamTv tunajua baba mmoja sasa basi kwakua mliwaaminisha watanzania kuwa mnaleta mapinduzi ya soka bas tuonesheni utofauti wa soka kueni na balanzi wakati wa mechi kama ni makosa basi yaoneshe pande zote na kama ni mazuri basi yaoneshwe pande zote japo ni kituo cha nyumbani tutakuja kukichoka tu kwa mfumo huu

4) kwa wachambuzi wenu wa kituo cha michezo wawe wana michezo wasichambue timu moja tu mtazamaji aliekaa katika runinga anajifunza nini sasa ndiyo maana katika mabanda umiza mpira ukiwa oftaimu watu huendelea na story zao.hawataki hata kuwasikiliza


Naomba niishie hapo kama mtavutiwa wadau karibuni kwa kuchangia
Asanteni
By moody kabwe
 
umeongea points ambazo mimi nimezikubali, kiukweli ningekuwa muajiri wa Azam TV ningefukuza watangazaji wengi akiwemo Mvulla, sio siri Mvulla level yake ni redio au TV za wilayani na si Azam, kwa hali hii Azam TV wasubiri sana wana watangazaji wengi zero ambao wanaondoa mpaka sifa nzuri ya akina Charles Hilary

Ni mimi @Malezo kukuletea habari hii
 
Hizo lawama tu! Tanzania kuna tatizo la uhaba mkubwa wa watangaza mpira wenye ubora unaokidhi mabadiliko ya utangazaji duniani. Kwenye uchambuzi wa mpira pia kuna tatizo kama hilo. Hao unaowaona ndo wamejitokeza na azam imewachukua. Kama kuna unayemjua anatangaza na kuchambua mpira kisasa kwa kiswahili kama wale jamaa wa sky sports mshawishi akaonane na tido uone kama atanyimwa kazi. We hushangai kwanini supesport wanapotangaza kwa kiswahili wanawatumia wakenya wakati kiswahili bongo ndo nyumbani?
 
Unakumbuka suala la Nyosso lilioneshwa pale tu Nyosso alipomtia dole Bocco ilhali tukio lilianza kwa Sure Boy kumfanyia kitu Nyosso.
 
Nazani waliotazama mpira jana wa mapinduzi cup wamejionea wenyewe
 
Mvula hafai kurtangaza mpira nafuu hata Nurdin Suleiman anabalance, Huyu mvula kazi kuiponda team pinzani na wachezaji wake
 
Mvula hafai kurtangaza mpira nafuu hata Nurdin Suleiman anabalance, Huyu mvula kazi kuiponda team pinzani na wachezaji wake
Uko sahihi kwa Nurdin...Hana mahaba ya kipuuzi...

Ila hao Hassan Mvula na Twalib Omary ndo hovyo kabisa....Wao ni kuponda timu pinzani na Azam FC
 
Back
Top Bottom