Azam tumieni njia mbadala badala ya madishi

Azam tumieni njia mbadala badala ya madishi

Egwugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,558
Reaction score
8,556
Uwekezaji wenu ni mkubwa na soko lenu vile vile ni kubwa mno. Kitu kimoja hadi sasa kimewashinda ni kuweza kuja na aina ya teknolojia ama madishi ambayo yanaweza kuhimili hari ya hewa ya hapa Tz. Madishi yenu yana ubora hafifu sana hasa nyakati kama hizi kukiwa na mawingu kidogo tu ama mvua basi utakuta picha hazionekani tena hadi kabisa.

Hebu chukulia maeneo kama kanda ya ziwa na haswa (Kagera) ambako mvua zinanyesha miezi 7/12 maana yake nini? Si kuliwa pesa bure kweli? kila siku mtu unakutana na maneno "access denied ama no signal", why so? Kwa kampuni yenye jina kubwa kama yenu huu ni udhaifu mkubwa sana. Na kwa uzoefu na mda mlionao katika biashara hii mlitakiwa kuwa mmeshakuja na suruhu ya hili. Katika karne hii ya tehama hakuna kinachoshindikana bwana, msilete figusu figusu za mara hivi mara vile, tumieni pesa mpate pesa ya maana.

Super sport mbona wako live all wheather na wako mbali sana, why Azam Tv just from Dar and yet everything collapses while still in Dar ...WHY?

Wateja wenu tunajitahidi kuvumilia lakini tunaumia sana. Tunashindwa hata kupata ile raha tuliyoizoea kwa vipindi vya jua na kiangazi. Hiki kipindi kuna mda mtu unatamani hata ukitupe king'amuzi chako kutokana na aina ya usumbufu mnaotupatia. Tunaamini pesa za kutatulia hili tatizo si kazi kwani makampuni yenu yako vizuri, kinachobaki ni utashi wenu juu ya jambo hili. Tufanyieni msaada wa kweli na wa haraka
 
Ile app yao ni yakisengerema sijawahi ona..wengine hatuwezi kuwa Kwenye TV muda wote..cha ajabu kukiwa na game muhimu utaona inaandika "something went wrong" wali design ya nini? Bull shit!
 
Mwenye Hio avatar hapo juu ya huyo mrembo mungu anakuona.
 
Ile app yao ni yakisengerema sijawahi ona..wengine hatuwezi kuwa Kwenye TV muda wote..cha ajabu kukiwa na game muhimu utaona inaandika "something went wrong" wali design ya nini? Bull shit!
Hakika mkuu unachokisema, sijui ndo nini ile hata haieleweki
 
Azam wanaboa sana kwa kweli, bado kidogo tu nitupe king'amuzi chao
 
Back
Top Bottom