Azam Media na TFF wamekuwa na mchango mkubwa wa kuvuruga soka letu na hii dhambi hawatoikwepa

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,844
43,314
Wana jf wasalaam.
Toka mwanzo wa saktata la card tatu za mchezaji wa kagera nimekuwa nikijiuliza ni nani walikuwa wana dhamana ya kuhakikisha wanaondoa utata kwenye swala hili? Lakini jibu lilikuja haraka kwamba ni TTF na Azam media...
Kuna maswali mengi watu hujiuliza ikiwa Azam media hawana uwezo wa kuonesha game zote za ligi kuu kwanini wapewe wao pekee dhamana ya kuonesha mechi zote na wanashindwa kuonesha mechi zot? Nilitegemea kuona makampuni zaidi ya kipewa tenda ya kuonesha ligi na wagawane match za kuonesha na hili ndio lingekuwa suluhu la maneno oooh match haikuoneshwa oooh match haikurekodiwa...

Katika hili mimi ndio naona pengine TFF ya malinzi inafanya makosa yanayopelekea kulivuruga soka letu na ninategemea kuwe na uwajibikaji maana ni wazi hili swala limefanywa kwa msalai yao binafsi....kulikuwa hakuna sababu ya kumpa mtu mmoja tenda ya kuonesha mpira ikiwa hatoonesha match zote.....kwanini asingelipewa mwingine? je ni yeye pekee aliomba tenda?

Leo sakata la card limefanya mpira wetu kuvurugika kabisa na kuzua sintofahamu wakati tulitegemea watu kama Azam media na TFF ndio wangelimaliza lakini wameshindwa hadi wanaanza kuita mchezaji aliyepewa kadi.

TFF lazima wabadilike maana tunako elekea ni watu kususa kuingia uwanjani kabisa au timu kususia kushiriki kwa sababu ya uzembe wao wa wazi wazi....

Wasalaam
 
Tulia mechi ya Kagera na African Lyon alikuwa kwenye ratiba yao Africa Lyon waliiomba Kagera wacheze nao kutoka na na hali ya uchumi
 
hoja hapa kwanini match haikuoneshwa ikiwa walikubaliwa ombi lao na walipewa referees na kila kitu?
 
wewe ndio utakuwa mtu wa KWANZA duniani kutoa ushauri kuwa Ligi ionyeshwe na Satellite Television Service Provider wawili ndani ya nchi moja..

Sijui mwenzetu umeona wapi suala kama hili likifanyika.

Ukizingatia umaarufu wa ligi na hali ya kiuchumi nchini.
 
Tulia mechi ya Kagera na African Lyon alikuwa kwenye ratiba yao Africa Lyon waliiomba Kagera wacheze nao kutoka na na hali ya uchumi
Mkataba wa Azam na TFF unasema Azam TV lazima aonyeshe mechi zote,ni mechi ngapi ambazo zilihairishwa na bado zilionyeshwa na Azam TV
 
Hapo wawalamikie zaidi TFF, kwasababu wao ndio wanatakiwa kusimamia na kuhakisha AZAM anaonesha hizo match!!!
 
Kwa sasa uwezo wa Azam kuonyesha mechi zote za Ligi kuu hawana.

Production Cost ziko juu mno! DSTV wenyewe wameiacha Ligi ya Nigeria, Ghana na Kenya. Production cost ziko juu mno ukizingatia ni kuna baadhi ya mechi ambazo hazina uwezo wa kuingizia azam pesa ya kutosha kwa muda wa Game itakapo kuwa hewani.
 
Hapo wawalamikie zaidi TFF, kwasababu wao ndio wanatakiwa kusimamia na kuhakisha AZAM anaonesha hizo match!!!
Mkuu ndani ya miaka hii ya usoni usije kutegemea kama Game zote za VPL zitarushwa hewani.

Mfano:

DSTV hawajawahi kurusha game zote za SPL (Afrika Ya Kusini).

DSTV hawajawahi kurusha game zote za KPL (Kenya).

DSTV hawajawahi kurusha game zote za GPL (Ghana).

DSTV hawajawahi kurusha game zote za NPFL (Nigeria).

Hata kama wangrkuwapo hapa Bongo wasingerusha game zisizo na msisimko. Hivyo usitarajie Azam hata kama wakibanwa vipi kama wataweza kurusha game zote.
 
Asantee sana, point noted
 
Mkataba wa Azam na TFF unasema Azam TV lazima aonyeshe mechi zote,ni mechi ngapi ambazo zilihairishwa na bado zilionyeshwa na Azam TV
Unajua kwenye hii mikataba ya waafrika kuna muda unatakiwa usizingatie kilakitu.

Hivi kwa akili zetu za kawaida unawezaje kudhani kuwa Azam (na miundombinu yao yote) wanaweza kutimiza hiko kipengele?

Mfano:

Chanel ambazo azam anaweza kurusha game ni.

Azam One
Azam Two
Azam sports HD
Pengine na ZBC & Extra Chanel.

Kwa weekend ya kawaida kama jumamosi ambapo azam anataka kuonyesha
LaLiga,
VPL,
Uganda Premier League , na
Rwanda Premier League....

Inawezekanaje akapata nafasi ya angalau ya saa moja na nusu kuonyesha game ya Ruvu Shooting - MbaoFC ikiwa hapo hapo Ligi nyingine zina mechi takribani zisizopungua 3..?

Laliga 3
VPL 8 (hapa ndio mnataka zionyeshwe zote)
RPL 3
UPL 3

Jumla Mechi 17. Je swali la kujiuliza kwenye mazingira haya anawezaje kuonyesha mechi zote 17 katika kipindi cha masaa 5 ( saa 9 mchan - saa 2 kamili).

Note: Haya ni mahesabu ya siku moja tu (mathalanu Jumamosi).

Mleta mada naona hauwa anajua hili, bila shaka atakuwa ameng'amua jambo hapa!
 
Wana jf wasalaam.
Toka mwanzo wa saktata la card tatu za mchezaji wa kagera nimekuwa nikijiuliza ni nani walikuwa wana dhamana ya kuhakikisha wanaondoa utata kwenye swala hili? Lakini jibu lilikuja haraka kwamba ni TTF na Azam media...
Kuna maswali mengi watu hujiuliza ikiwa Azam media hawana uwezo wa kuonesha game zote za ligi kuu kwanini wapewe wao pekee dhamana ya kuonesha mechi zote na wanashindwa kuonesha mechi zot? Nilitegemea kuona makampuni zaidi ya kipewa tenda ya kuonesha ligi na wagawane match za kuonesha na hili ndio lingekuwa suluhu la maneno oooh match haikuoneshwa oooh match haikurekodiwa...

Katika hili mimi ndio naona pengine TFF ya malinzi inafanya makosa yanayopelekea kulivuruga soka letu na ninategemea kuwe na uwajibikaji maana ni wazi hili swala limefanywa kwa msalai yao binafsi....kulikuwa hakuna sababu ya kumpa mtu mmoja tenda ya kuonesha mpira ikiwa hatoonesha match zote.....kwanini asingelipewa mwingine? je ni yeye pekee aliomba tenda?

Leo sakata la card limefanya mpira wetu kuvurugika kabisa na kuzua sintofahamu wakati tulitegemea watu kama Azam media na TFF ndio wangelimaliza lakini wameshindwa hadi wanaanza kuita mchezaji aliyepewa kadi.

TFF lazima wabadilike maana tunako elekea ni watu kususa kuingia uwanjani kabisa au timu kususia kushiriki kwa sababu ya uzembe wao wa wazi wazi....

Wasalaam
Nan asuse simba ama yanga...? Be serious bana...kwa sasa hatuwaogop tena tunaomba washushwe daraja wote.. Simba na yanga

Sent from my E2303 using JamiiForums mobile app
 
Unajua kwenye hii mikataba ya waafrika kuna muda unatakiwa usizingatie kilakitu.

Hivi kwa akili zetu za kawaida unawezaje kudhani kuwa Azam (na miundombinu yao yote) wanaweza kutimiza hiko kipengele?

Mfano:

Chanel ambazo azam anaweza kurusha game ni.

Azam One
Azam Two
Azam sports HD
Pengine na ZBC & Extra Chanel.

Kwa weekend ya kawaida kama jumamosi ambapo azam anataka kuonyesha
LaLiga,
VPL,
Uganda Premier League , na
Rwanda Premier League....

Inawezekanaje akapata nafasi ya angalau ya saa moja na nusu kuonyesha game ya Ruvu Shooting - MbaoFC ikiwa hapo hapo Ligi nyingine zina mechi takribani zisizopungua 3..?

Laliga 3
VPL 8 (hapa ndio mnataka zionyeshwe zote)
RPL 3
UPL 3

Jumla Mechi 17. Je swali la kujiuliza kwenye mazingira haya anawezaje kuonyesha mechi zote 17 katika kipindi cha masaa 5 ( saa 9 mchan - saa 2 kamili).

Note: Haya ni mahesabu ya siku moja tu (mathalanu Jumamosi).

Mleta mada naona hauwa anajua hili, bila shaka atakuwa ameng'amua jambo hapa!
Sababu ya game ya Kagera kutoonyeshwa wanadai haikuwa kwenye ratiba sio hizo sababu unazoandika wewe,ni mechi ngapi hazikuwa kwenye ratiba na zimeonyeshwa ?

Hatujasema mechi zote zionyeshwe live,baadhi ya mechi zinaweza kuonyeshwa recorded,hivi unajua kuonyeshwa kwa ligi kwenye TV kumepunguza idadi kubwa ya watu kwenda uwanjani

Mkataba wa Azam na TFF hauna uhusiano na kuonyesha LaLiga hizo ni deal tofauti kabisa
 
Kwahiyo matatizo ya soka nchini yataisha ikiwa mechi zote zitaonyeshwa live?

Nadhani umeshindwa kutengeneza vema mawazo maana mpira wetu una mapungufu kibao. Kuna mapungufu ya kiuamuzi, miundombinu, menejimenti za timu, vyama vya soka na mlezi wao TFF.

Sasa unapokazia kwenye kuonyesha mechi live sijui inawezaje kuondoa tatizo la upangaji wa matokeo (kama ilivyokuwa kwa kina Geita) au vipi kuonyesha mechi live kunaweza ondoa tatizo la uamuzi wa utata ilhali tunaona uamuzi tata ukitokea hata ulaya hadi wanafikiri watumieje teknolojia.

Mechi nyingi tu hazijarushwa live na Azam ila nadhani haya yote yamekuja baada ya kuhusisha Timu kubwa.

Unaweza kujiuliza, kwanini pingamizi la timu ya Polisi dhidi ya Simba lilitupwa na kamati ya saa 72 kwa kigezo kuwa hawakulipa ada ya pingamizi hilo ilhali Simba dhidi ya Kagera kwanza wamepeleka pingamizi nje ya muda tena bila ada lakini kamati ileile imetoa maamuzi ya kuibeba Simba?

Azam Media hawahusiki hata kidogo, bali mfumo madhubuti ndio unahitajika
 
hivi unajua kuonyeshwa kwa ligi kwenye TV kumepunguza idadi kubwa ya watu kwenda uwanjani?

Hili sio tatizo kwakuwa hata tukisema mechi zisionyeshwe badge timu kama Mtibwa Sugar haina uwezo wa kuingiza zaidi ya Mil 100/= kwa msimu mzima..
 
Sure kaka, azam wanachagua mechi za kuonyesha, wapewe tu DSTV wana wana nia kweli
 
Sababu ya game ya Kagera kutoonyeshwa wanadai haikuwa kwenye ratiba sio hizo sababu unazoandika wewe,ni mechi ngapi hazikuwa kwenye ratiba na zimeonyeshwa ?

Game kama ile kamwe haiwezi kuwekwa kwenye ratiba kwa taarifa rasmi

Bali pale Azam huwa wana Emergency matches. Hizo ni zile ambazo zinaonyeshwa panapopatikana na nafasi ya Airtime na unyeti wa match yenyewe...
 
Back
Top Bottom