PRINCE CROWN
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 5,210
- 4,182
Ni kweli Azam TV n moto Wa kuotea mbali. Wamesajili majembe yote.Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa (azam media) kwa kuwa hewani siku nzima ya leo katika kutujuza yanayoendelea dodoma,tofauti na vyombo vingine vya habari, na ihi inatoa picha kwamba kipindi cha kampeni azam media itawashinda vyombo vingine kwa utoaji bora wa habari kwa kina,
Na hata inasikitisha vituo vya TV kama ITV, Channel ten, StarTv ni vikongwe sana lakini utangazi ni style ile ileisiyobadilika!
Binafsi, nilitegemea vituo kama ITV viwe na channel kama ITV News, ITV Sports nk
Cheki Azam wamekuja juzi tu lakini wanawa overtake wakongwe!
Kwa kweli jamaa wako vizuri sana hawa Azam media. Kule kuna watu wa kazi tuu. Natumaini wakati wa uchaguzi mkuu watatuletea matangazo yaliyo bora zaidi. big up Tido na time yako.