Azam media group movie mnazorusha kwa lugha ya kiswahili ni mbaya mno

Habari wana jamvi,

Niende moja kwa moja kwenye mada.Azam TV wamekuwa wanarusha movie walizo tafsiri kwa kiswahili lakini hawa jamaa wanatuonesha vimuvi vya hovyo sana mfano jana tar28/04/2018 pale azam two kimuvi kibaya balaa.

Pia tamthiliya zenu nazo ni mbaya vile vile mfano tamthiliya ya SULTAN ni mbaya inafundisha kugegeda vijakazi tu hamna lolote!!

Pia tamthiliya ya Jamai Raja huwa inatakiwa iwe nusu saa lakini nyinyi mnaonesha dk 20 tu halafu mnajaza mitangazo yenu ya hovyo!!

Swali: kwa nini hamrushi seasons za kikorea ? Pia muvi kali za mapambano hamna mpaka mturushie vimuvi vya hovyo?

Wana jf karibuni tuwape vidonge vyao hawa...
Usichikipenda ww,kuna mwenzako kinamnyima usingiza. SULTANI ni Tamthilia nziri sana. sema tu ww wakati wa kuangalia huwa unakuwa ushapata vitu vyako... hii hupelekea uione mbaya
 
Mm huwa sitegemei movie zinazorushwa kwenye ching'amuzi. Nikitaka movie nadownload movie nayoitaka naangalia.
 
Usidhani movie inachukuliwa tu na kurushwa kwenye TV, kuna makubariano ya hati miliki na kiasi cha pesa kinalipwa.
Ndiyo maana huwezi kuona wanarushwa movies mpya kwakuwa ni ghali sana kupata haki ya kuzionyesha movie hizo na kwa hayo malipo yetu ya 23,000 hawezi kumudu ukitaka kujua hilo channel ya movies ya netflix malipo yake ya bei ndogo ni 11$ kumbuka ni channel moja tu hiyo.
Sasa wasipoonyesha matangazo wakati ndiyo yanawaingizia ela zaidi TV wataiendeshaje?
Ukitaka vizuri hamia DSTV nadhani gharama zao wazijua vizuri gharama mkuu
Mie nataka kuhamia DSTV
 
Movie ya Jana ni nzuri, 30 minutes or less ilikua bomba. Nimeipenda maana ina comedy fulan hivi ndani yake.

Sultan iko Poa, Hurem (Alexander) anacheza vizuri, hata Sultan Suleyman pia na Ibrahim wake. Sema tu zile vita zao zimekaa nyepesi mno, zinaonyesha kabisa ni acting, sio nzito kama za kina Jumong.

Jamai Raja ni fupi kweli, ila matangazo ndio yanayowaweka mjini wenye TV stations. Maana wale waliotafsiri lazima walipwe pia. Namfahamu Monalisa Ivon Cherry ameigiza sauti ya Kritika, mshiko wake anaolipwa sio wa kitoto. Sasa ukipiga hesabu na wengine waliobaki ni balaa.

Tusubir tu, wanaweza kuja kutafsiri kina Jumong, Land of Wind, Man Called God, Kingdom of Wind etc. Nina uhakika wanapitia humu, Unajua hata juzi tuliwaponda kuhusu kutomchangia Msanii Majuto then baada ya kusoma wakaenda kumsaidia wakiwa na Mh. Waziri.
Atleast wewe umeongea kitu
 
Usidhani movie inachukuliwa tu na kurushwa kwenye TV, kuna makubariano ya hati miliki na kiasi cha pesa kinalipwa.
Ndiyo maana huwezi kuona wanarushwa movies mpya kwakuwa ni ghali sana kupata haki ya kuzionyesha movie hizo na kwa hayo malipo yetu ya 23,000 hawezi kumudu ukitaka kujua hilo channel ya movies ya netflix malipo yake ya bei ndogo ni 11$ kumbuka ni channel moja tu hiyo.
Sasa wasipoonyesha matangazo wakati ndiyo yanawaingizia ela zaidi TV wataiendeshaje?
Ukitaka vizuri hamia DSTV nadhani gharama zao wazijua vizuri gharama mkuu
 
Usichikipenda ww,kuna mwenzako kinamnyima usingiza. SULTANI ni Tamthilia nziri sana. sema tu ww wakati wa kuangalia huwa unakuwa ushapata vitu vyako... hii hupelekea uione mbaya
Ttz haina mapambano ila mapenzi kwa wingi
 
Back
Top Bottom