Azam marine kuleta boat mpya hivi karibuni

Banxbanxson

Senior Member
Oct 19, 2016
119
149
Kupitia page yao ya Instagram, Kampuni ya usafirishaji Baharini ya Azam marine inayomilikiwa na Mzee Said Salim Bakhresa, imetangaza rasmi ujio wa boat yao mpya iitwayo Kilimanjaro VIII iliyopewa jina la FALCON OF THE SEA.

Boat hiyo mpya kabisa iliyotengezwa nchini Australia inatarajia kuwasili Zanzibar mwishoni mwa mwezi huu.
Wasafiri baina ya Unguja na Dar Es Salaam watafurahia boat hiyo itakayokuwa na mwendokasi zaidi kuliko boat nyingine za kampuni hiyo.

Hii ni sehemu ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Mzee Bakhresa ili kurahisisha huduma ya usafiri Baina ya Visiwani na bara.

Wahusika wa karibu wa Kampuni hiyo wanasema utengenezaji wa boat hiyo ulichukua takribani miaka miwili umegharibu Pesa za kitanzania Bilioni 47.

Hakika Mzee huyu anastahili pongezi katika ujenzi wa Taifa hili.

Tazama video hapa
 
Back
Top Bottom