Azam FC yamtimua kocha Omog

Azam FC yamtimua kocha Omog

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
Uongozi wa Azam FC umetangaza rasmi kuachana na kocha wake Joseph Omog baada ya kuwa nae kwa kipindi cha miezi 14.

Mwalimu huyo wa zamani wa Leopards ya Kongo anaondoka ikiwa ni siku mbili baada ya kutolewa kwenye Kombe la Klabu Bingwa Afrika kufuatia kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa El-Mereikh mjini Omdurman.

Ajira ya kocha huyo raia wa Kamerun inasitishwa sambamba na msaidizi wake Ibarahim Shikanda!

Chanzo: Azam FC

attachment.php
 
Attachments

  • azam.png
    azam.png
    196.2 KB · Views: 2,188
Mpira wa tanzania majanga matupu
 
Baada ya kudumu katika timu hiyo ya Matajiri jijini Dar es salaam kwa muda wa miezi 14. Timu ya Azam Football Club imemfukuza aliye kuwa kocha mkuu Joseph Omog.

Je hii Tabia ya kufukuza makocha kutokana na matokeo mabaya ni mzizi kwa maendeleo ya soka la Tanzania.? Hasa kwa club changa kama Azam Football Club.?
 
Azam nao wanaanza kuiga siasa za Yanga na simba
 
du...even if they are hired to be fired hii sasa sifa...
 
Wazee wa mapinduzi ya soka,hahaha siami yanga mmi,nashabikia mpira na sio pesa,
 
Attachments

  • 1425305213657.jpg
    1425305213657.jpg
    30.5 KB · Views: 400
Kocha kama kashindwa kazi lazima afukuzwe sisi tunataka maendeleo sio kelele
 
Soka la bongo katika ubora wake...Azam haiwezi kuwa na jipya sana ...viongozi wake wengi ni walewale...inatakiwa hata viongozi(Maafisa wa timu) wabadilishwe waajiriwe wataalamu hasa hata kama wa kutoka nje ya nchi waje waboreshe timu
 
Baada ya kudumu katika timu hiyo ya Matajiri jijini Dar es salaam kwa muda wa miezi 14. Timu ya Azam Football Club imemfukuza aliye kuwa kocha mkuu Joseph Omog.

Je hii Tabia ya kufukuza makocha kutokana na matokeo mabaya ni mzizi kwa maendeleo ya soka la Tanzania.? Hasa kwa club changa kama Azam Football Club.?

hata utupeleke wapi ndio wa hivi hivi..

kwa mbali namuona maximo na msaidizi wake haoooo watua azamfc

hakuna kitu kama hicho mkuu

Jambo la heri tu

sio kabisa la heri hasa kwetu sie die hard fans..
 
Kalimangonga alienda kuongeza elimu ya ukocha Uingereza. Kwa kutimuliwa kwacOmog, bila shaka Kali yuko njiani kurejea Azam.

yap hapo umenena sasa na hii ni kutokana jamaa katokea mbali sana..
 
Maemdeleo gani mkuu?

Mkuu yanga tukiwatimua makocha wanasema club bora na ya kuigwa ni azam fc lakini leo wanatimua walimu wao sasa sijui wataiga nini wale wa kuiga kutoka kwao.
ha ha ha ha ha ha ha ha ha YANGA UTAIPENDA.
 
Kalimangonga alienda kuongeza elimu ya ukocha Uingereza. Kwa kutimuliwa kwacOmog, bila shaka Kali yuko njiani kurejea Azam.

lakini hata kama kali yuko njiani kwanini wasiwe na subra ili arudipo apate mzoefu kumzoesha kazini!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom