AY kupambana na Ruge Mutahaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AY kupambana na Ruge Mutahaba

Discussion in 'Entertainment' started by Mtoto wa Kishua, Feb 2, 2011.

 1. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 818
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Msanii anayepata mafanikio ya kimataifa katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini Ambwene Yessaya aka AY amewataka wasanii kugoma kulipwa fedha kidogo kwenye maonyesho na badala yake wawe na msimamo mmoja katika kupanga viwango vya malipo yao.

  AY aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu Harakati za Kuufanya Muziki wa Kizazi kipya kuwa wa kimataifa kwenye Jukwaa la Sanaa linaofanyika kila wiki katika Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo alisema kwamba, wasanii hapa nchini wamekuwa ni wepesi kulalamika wanapolipwa malipo kidogo lakini wagumu kuchukua hatua katika kukomesha hali hiyo.

  “Wasanii wengi wanalalamika malipo kidogo kwenye maonyesho, naona hali hii wanaitaka wenyewe. Kama msanii umeweka viwango vyako vya malipo na vinatambulika lazima anayekuhitaji atakulipa tu kazi kubwa inayobaki ni kuweka juhudi na ubunifu katika kazi tunazozifanya na kwenye maonyesho” alisema AY.

  Alizidi kueleza kwamba, wasanii kwa pamoja wanao uwezo wa kukataa malipo wanayolipwa sasa kwenye maonyesho kwani wao ndiyo wenye kazi na ndiyo wanaoamua kuzitumia. Katika hili alisisitiza kwamba, ni bora msanii akubali kulala njaa kwa siku moja ili aweze kula kwa mwaka mzima badala ya ilivyo sasa ambapo wamekuwa ni wa kulilia fedha za kukidhi matatizo yao madogomadogo tu.

  “Huko Nigeria kulikuwa na mchezo kama huu wa wasanii kulipwa fedha ndogo kwenye maonyesho lakini kuna siku wasanii wote waliamua kugoma kushiriki shoo za nyumbani hadi hali itakapobadilika. Leo hii msanii wa Nigeria analipwa dola laki moja na nusu hadi laki mbili wakati hapa kwetu ni ndoto” alisisitiza AY huku akiwaomba wasanii kuwa na umoja katika hili.

  Wakati akiwasilisha mada yake, AY alitaja mambo kama uthubutu, kutengeneza kazi za sanaa zenye ubora, kujiamini, ushirikiano, kusimamia asili yetu na vitu vingine kama nguzo zitakazosaidia kuuvusha muziki wa kizazi kipya kwenye ngazi za kimataifa.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA ambaye pia ni mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Ghonche Materego alisema kwamba, Baraza lake litaendelea kuwakutanisha wasanii wa hapa nchini na wadau wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuwapa fursa ya kujifunza kutoka kwao.

  “Leo hapa tumeelezana masuala ya kujiamini, kuthubutu, kufanya kazi zenye ubora, haya yote ni ya msingi katika kukuza sanaa zetu. BASATA itaendelea kuwakutanisha wasanii na wadau wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa lengo la kukuza sanaa zetu na kutekeleza kaulimbiu ya mwaka huu ya Sanaa ni Kazi” alimalizia Materego.

  Chanzo Globalpublisherstz
   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Inauma pale msanii anapoishi maisha ya kubahatisha huku wajanja wachache wakifaidi jasho lake.
   
 3. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 818
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Tatizo ni kubwa sana kwa wasanii haswa ukizingatia magwiji kwnye biashara hii ndio wako karibu na raisi na ambao ndio wanamfanyai hadi Bedhidei na raisi kuamini kuwa Bila watu kama Ruge asinge ingia madarakani kiraisi sababu ya lile fiesta lililopigwa kwnye kampeni.
   
 4. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Acha wanyonywe mpk mavi.
  Coz ikifikaga kipindi cha uchaguzi basi wao huwaambii kitu juu ya CCM.

  Sasa acha CCM wawalipe fadhila
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kule kwenye kampeni za CCM kuna uhusiano gani madai ya AY?
   
 6. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 818
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45

  Hilo nalo neno, maana wanakua mstari wambele kupiga kampeni, wakati wanaye mpigia kampeni kaisha kamatwa na fisadi papa wa biashara ya burudani (Ruge Mutahaba) ,matokeo yake baada ya kampeni kuisha fadhila anapewa Ruge na wao wasanii kusahukika na kusota kama kawa . Nadhani ni mwanzo mzuri umeanzishwa na AY.
   
 7. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Heshima Mbele Kibunango...
  Ishu ni kuwa kwa wasanii wetu wa Kibongo walivyo mstari wa mbele pindi kampeni zinapofika then baada ya hapo wanaitwa Ikulu na jamaa kisha wanapewa Menu na kupiga nae Piacha ya pamoja ingekuwa safi sana kama Serikali hiyohiyo ya yule waliyempigia chapuo kuingilia kati na kuwasaidia wasanii hawa wawe wanalipwa vizuri kwenye Shoo na pia wangesimama imara na kuwasaidia wasanii wasinyonywe na wahindi wale wachache ambao ndio huwa wana distrubute kazi zao.

  Lakini kwa mambo kama haya huwezi kusikia CCM wametia pua zao.

  Sasa wahenga wanasema rafiki wa kweli ni yule wa shida na raha.
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wanawapromoti kimuziki hadi kimwili
   
 9. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 818
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ukifuatilia vizuri, msanii anabanwa sio moja kwa moja na Wahindi , kuna fisadi huyu Ruge, yeye yuko kwnye kila kitu, ana connection kila sehemu kuanzia kwenya makampuni makubwa ya udhamini, usambazaji, vituo vya TV,radio na Tuzo zote. yeye na uwezo wa kuhakikisha una baniwa na unapotezwa na sasa na connection hadi Ikulu. Kuna kipindi ili bumbuluka ana play list yake anayo taka nyimbo zipigwe na nyingine zisipigwe kwnye Channel 5 TV , iki ongozwa na demu wake Christine Mosha aka Seven (enzi hizo alipo kua ITV), huko kwenye MTV base na hizo awards pamoja na show zote kama Big Brother , Idol ,Tusker project fame kote ana mkono wake, ndio najiulzia huyu AY amejipanga vipi kupambana na Ruge Mutahaba?
   
 10. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ruge ni mtu hatari sana kwa mziki wa bongo flavour,ni mnyonyaji sana
   
Loading...