Don't blame Ay (yeye ni Mlamatoke wa Mbeya, chingerezi na yeye ni maji na mafuta?) Nyimbo zake nyingi ni kiswahili kama sio "copy & paste" maneno machache tu ya Kizungu!. Ipo hivyo hata kwa wasinii wengine duniani, ili mradi unafikish ujumbe kwa lugha ile ambayo wengine wanakuelewa.
Hata Mwana FA nae anaonekana anatumia muda mwingi kufikiri kwa kiswahili ili aweze kujibu swali kwa kiingereza. Hili ndo tatizo la kuendekeza lugha za kigeni, akili inaumia mmo pale unapotakiwa kujibu kitaalamu.
Unaweza kuona hata majibu wanayotoa hayana maelezo ya kitaaluma zaidi kwa kuhofia kukosea lugha ( Ona Mwana FA na pamoja na Shahada yake ya Chuo Kikuu anajibu pasipo maelezo ya kina ya kudhirisha ufahamu wake wa yale anayojibu).
Niemwangalia pia Alikiba, yeye anaulizwa kizungu anataoa majibu kiswangilishi na pia hata muulizaji nae ni Mswangilishi.
Hopeless show, sijui inasaidia nini!.