tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Pangani ambaye pia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Aweso amepokea fomu hiyo leo, Agosti 26, 2025, kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Pangani, Juma Bwela, katika hafla iliyohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi na wajumbe wa CCM waliomsindikiza.
Akizungumza na wanahabari baada ya kuchukua fomu, Aweso amewaomba wanachama na wananchi wa Pangani kuendelea kujitokeza kwa wingi kusaka kura za CCM, akisisitiza kuwa mchakato wa uchaguzi bado unaendelea na ushindi wa chama hicho ni heshima kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aweso amesema moja ya changamoto kubwa iliyokuwa inakwamisha maendeleo ya Pangani kwa miaka mingi ni barabara ya Tanga–Pangani–Saadani–Bagamoyo, lakini chini ya uongozi wa Rais Samia changamoto hiyo imeanza kutatuliwa kwa barabara na daraja kuanza kujengwa. Amesisitiza kuwa utekelezaji huo ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya serikali kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi.
“Hakuna demokrasia ya kupata viongozi zaidi ya uchaguzi, kwahiyo niwaombe ndugu zangu wa Chama Cha Mapinduzi na Wanapangani, hatujamaliza uchaguzi, twendeni tukazisake kura za CCM, kura za heshima kwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan”, ameeleza Aweso.
Kwa upande wao, wajumbe wa CCM Pangani na wananchi waliohudhuria wameeleza dhamira yao ya kuendelea kumpa kura Aweso, wakimtaja kama kiongozi mchapakazi na mwenye dira ya maendeleo, wakibainisha mchango wake katika sekta ya maji, elimu, na mikopo kwa wanawake, vijana na wenye uhitaji maalumu