Awamu ya tano: Ni mwendo wa Kijeshi

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Wakuu wa Mikoa, Makatibu wakuu, Ma-RAS wengi Wanajeshi wastaafu, Polisi.
3.jpg

SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kuteua wakuu wa mikoa wapya, mtaalamu wa sayansi ya siasa, Profesa Mwesiga Baregu, ameibuka na kusema kuwa kuwapo kwa wanajeshi wengi wastaafu katika uteuzi huo inadhihirisha wazi kuna dalili za utawala wa kijeshi nchini.

Profesa Baregu amesema kuwa wanajeshi huwa hawana hulka ya kidemokrasia.

“Kitu kimoja kinachojitokeza kwenye uteuzi huu ni kuwepo kwa wanajeshi wastaafu, na mimi ninavyoelewa wanajeshi huwa hawana hulka za kidemokrasia. Hii inaonyesha wazi kwamba utawala huu ni wa kijeshi,” alisema.

Profesa Baregu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema haileti picha nzuri kuwapo kwa wanajeshi wengi katika utawala kwa sababu tawala za mikoa na wilaya ni saula la kiraia na demokrasia zaidi.

Alisema rasimu ya katiba ambayo yeye alikuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ilipendekeza kupitia upya tawala za mikoa na kupunguza idadi yake.

“Kutokana na hilo, mamlaka ya wananchi inamezwa kwa sababu wakuu wa mikoa na wilaya ni wengi na kunakuwepo na mgongano mkubwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ali, alisema uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya ni wa rais na wanaoteuliwa ni watu mchanganyiko.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Ruco), Profesa Gaudence Mpangala, alisema kila anapoingia kiongozi mpya anaunda timu ambayo anaona ataendana nayo.
 
kwa nchi ilipofikia yuko sahihi maana hata raia walitamani kuongozwa kijeshi ili kurudisha nidhamu,
maana wanajeshi hawana longolongo.

Ni kweli unachosema, lakini tupime tija yao. Hivi ni kweli hakuna vijana wa kuongoza nchi hii tena wengine wala hawajawahi kuajiriwa zaidi ya kusubiri kuongozwa na wazee tena walostaafu? Wana lipi jipya katika dunia ya sasa zaidi ya kuja kuleta siasa za vitisho? Hapo tutakuwa tunajiandaa na Tanzania ya viwanda ama Tanzania ya kijeshi? Hivi kweli tumeishiwa kiasi cha kungoja kuongozwa na wanajeshi waliopigana vita mara ya mwisho mwaka 79-80 vita ya Uganda. Kibaya zaidi unaongozwa na mwanajeshi ambaye hajawahi kufanya jambo lolote la maendeleo zaidi ya kufanya mazoezi ya kijeshi, kuchukua mshahara na kusubiri vita!! Nilitarajia kama kweli tuna nia ya dhati ya kuleta mapinduzi ya viwanda tungewapa nafasi wataalamu wa kilimo na biashara, ili kuongoza mikoa yetu kwa ajili ya kuleta changamoto za maendeleo na sio kusubiri watu watakaokuja kusimamia usafi na kupambana na wapinzani huku tukijinasibu kuwa Tanzania ya viwanda.

Nasema katika vitu Magufuli anachemsha ni uteuzi wa hawa jamaa, kumbukeni jeshi letu halina jambo lolote kubwa la kimaendeleo linafanya zaidi ya mambo ya kivita na kutoa msaada wakati wa maafa, sasa kwa mtu aliyekaa miaka 30 ambaye hajasimamia mradi wowote wa maendeleo unategemea kubadilika kifikra hapo ama kuleta fikra mpya tena akiwa na miaka zaidi ya 60? Halafu kuna watu wanasema eti wengi wao wamepewa sehemu za mipakani kimkakati zaidi kuhusu masuala ya ulinzi, hii ni hoja dhaifu kwani bado jeshi lipo na lina vijana na sio kutegemea hao wazee walioweka viinua mgongo vyao mfukoni. Na ndio maana hata waisilamu wanapata kichefuchefu kwani wanaona waopewa vyeo hawana na tija kabisa. Vichekesho vingine jamani hata ni aibu.

cc: Stroke
 
Back
Top Bottom