OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,015
- 114,360
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kutaja majina watuhumiwa wa madawa ya kulevya mengi yameibuka kumuhusu Makonda.
Hoja zilianzia bungeni kutoka kwa mbunge wa Geita Mh.Msukuma baadae Mbunge wa Rombo Mh.Selasini. Tuhuma zote zinaonyesha matumizi mabaya ya madaraka na kujilimbikizia mali.
Hivi punde yameshikiwa Bango mambo ya kutumia cheti cha mtu katika kupata elimu yake ya juu.
Watetezi wa Mh.Makonda ikiwepo Mh.Rais mwenyewe wamekuwa wakidai kwamba Makonda asichafuliwe kwa kuwa amejitoa kupambana na wauza madawa ya kulevya. Rais alisema anamuunga mkono Makonda na abashangaa watu wanamchafua kwa kuwa ni mpambanaji.
Hata mwanahabari aliyedai kutukanwa na Mh.Makonda amedai kuwa Makonda alimwambia inaonyesha katumwa na Wauza Madawa. Haya yalizungumzwa na mtuhumiwa bila kujibu tuhuma dhidi yake.
Hata mambo yananishangaza sana. Kwa lugha rahisi ni kwamba mimi nikitaja watuhumiwa wa ufisadi nakuwa nimepata kinga ya makosa yangu mengine mbele ya serikali. Kwa hiyo hata kama nitatuhumiwa kubaka nitakingwa na kuwataja mafisadi.
Pamoja na kwamba ndiyo tuhuma hizi zimekuja kukolezwa baada ya kuyataja majina ya kina Mbowe na Manji lakini ni tuhuma hizi ni nzito inabidi zifanyiwe kazi. Kukolezwa kwa tuhuma hizi ni suala ya timing tu. Kwa sisi wajumbe wa Jamiiforums hakuna jipya katika tuhuma hizi za Mh.Makonda. Kuhusu tuhuma a mali zisizoendana na kipato cha Makonda yameongelewa sana humu.Kuhusu utata wa majina ya Makonda yamesemwa sana humu tangu uteuzi wa Ukuu wa Wilaya. Kwa hiyo leo hii tuhuma hizi zimekolezwa tu.
Ombi langu kwa Magufuli na mamlaka zingine. Ni vyema mka-maintain credibility yenu ya kupambana na ufisadi na watumishi wenye vyeti feki. La sivyo mkubali kuonekana kuwa mna double standard katika vita hivyo.
Makonda ni mpambanaji,well and good.Kivipi umbanaji wake unakuwa kinga kwa makosa yake ya jinai???!!!
1.Daktari Mtwara alisimamishwa kazi kwa kusontwa tu na mama mmoja kwa kutuhumiwa kutaka hongo
2. Mh.Chenge hakupigiwa kampeni na Magufuli kwa tuhuma tu za ufisadi na matumizi mabaya ya cheo
3. Bandarini na TRA watumishi walisimamishwa kazi kwa tuhuma za kufanya ufisadi.
4.Orodha ni ndefu sana
SWALI: He Makonda yeye kateuliwa na Mungu kiasi kwamba hapa duniani hakuna wa kumshughulikia?