RAHA KAMILI
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 203
- 83
Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila Akitoa Mada kwenye Mradi wa kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye Ujasiriamali kupitia Taasisi ya Manjano Foundation. Mafunzo hayo yalianza wiki iliyopita kwa lengo la kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania kupitia bidhaa za vipodozi vya LuvTouch Manjano. Washiriki wataweza kujisimamia na kujikita vizuri kwenye biashara ya vipodozi na kujua mbinu mbalimbali za biashara kwa lengo la kumjengea uwezo mwanamke wa Kitanzania.
Washiriki wa Mafunzo ya Usajiriliamali na Urembo yalio chini ya Manjano Foundation wakisiliza kwa makini mada mbalimbali kuhusu mafunzo hayo ya kuwapa uwezo wa kuthubutu kufanya biashara, kujisimamia na kujua mbinu mbalimbali za biashara.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Washiriki walionufaika na Mradi huo.
Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili uwezo wake ikiwa pamoja na kuisaidia jamii yake iliyomzunguka. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano.
Awamu ya Pili ya Mradi huu Ulizinduliwa na waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage mnamo tarehe 14 Februari 2017, ambapo alisema amefurahishwa sana wwa mwanamke wa Kitanzania kuzindua mradi unaowawezesha wanawake kujiongezea kipato na kujiajiri hasa kwenye sekta ndogo ya Urembo yenye fursa kubwa ya kukua.