Naisoma360
JF-Expert Member
- Jan 23, 2015
- 821
- 491
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuufahamisha umma kuwa, Awamu ya Kwanza ya Watumishi wa Wizara kuhamia Makao- Makuu ya Nchi, Dodoma inaanza tarehe 10 Februari, 2017.
Miongoni mwa watakao hamia katika awamu hiyo ni pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara ambao ni Waziri wa Nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Naibu Makatibu Wakuu wa Nishati na Madini.
Watumishi wengine ni pamoja na Kamishna wa Madini Tanzania, Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Maafisa. Jumla ya Watumishi wanaohamia Dodoma Awamu ya Kwanza ni 47.
Aidha, kutokana na uhamisho huo, anuani ya Wizara Dodoma ni;
Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na Madini,
Barabara ya Kikuyu,
S.L.P 422,
DODOMA
Imetolewa na;
KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
9/2/2017