Auza mwanae alea mke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Auza mwanae alea mke

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shine, Jan 26, 2012.

 1. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Bwana mmoja nchini Saudi Arabia ameamua kumuuza mwanaye wa kiume kutokana na matatizo ya kifedha aliyonayo. Bwana huyo Saud bin Nasser Al Shahry aliweka picha ya mwanae kwenye ukurasa wa Facebook, akisema bei ya mtoto wake huyo ni dola milioni ishirini.
  Mtandao wa habari wa Press TV umesema baba huyo amedai kumuuza mwanaye ndio njia pekee ya kuondokana na maisha ya kimasikini. Biashara ya kukusanya madeni isiyo rasmi ya bwana huyo ilifungwa na mahakama hivi karibuni.
  Bwana Al Shahry amesema aliomba serikali imsaidie fedha, laki alikataliwa kwa sababu umri wake ni zaidi ya miaka thelathini na tano, umeripoti mtandao wa Mail online. Amesema akifanikiwa atatumia fedha hizo kumtunza mke wake na mwanaye mwingine wa kike.
  Na kwa taarifa yako....
  Chakula pekee kisicho oza ni asali...
  ------------------
  Tukutane wiki ijayo..... panapo majaaliwa..
  Taarifa kutoka mitandao mbalimbali ya habari duniani
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mungu atustiri.
   
Loading...