Aussems arudia maneno kama ya Rage: Ili Simba iendelee inahitaji kuachana na Viongozi Waongo na Vilaza

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,277
17,983
IMG_20191204_103926.png

Kocha wa Simba anayeondoka ametumia maneno yanayoshabihiana na yale ya Rage kuhusu Board Members wa Simba.

Ukweli ngumu kuuficha.
******

Aliyekuwa kocha wa Simba SC, Patrick Aussems 'Uchebe' amesema ili klabu hiyo, iendelee inatakiwa kuachana na viongozi waongo na wasiokuwa na uelewa katika bodi yake ya wakurugenzi.

Aussems alisema hayo jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ambao aliutumia kuwaaga mashabiki na wachezaji wa Simba kufuatia kuondoka kwake nchini baada ya kumalizana na klabu hiyo.

Kocha huyo, Mbelgiji aliposti ujumbe huo, uliokuwa ukisomeka, "Asanteni mashabiki wa Simba. Nawatakia kila la kheri. Ili Simba ikue, lazima watimue waongo na watu wasio na elimu kwenye bodi ya wakurugenzi."

Ujumbe huo, uliendelea kwa kusomeka kuwa sasa ni muda wa kufurahia na familia yake huku akimalizia, "Kwaheri Tanzania." Kocha ameondoka akiicha Simba ikiwa katika kilele cha msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Moja ya mambo yaliyopelekea Aussems awe kipenzi cha mashabiki wa Simba ni kitendo cha timu hiyo kutamba katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita wa 2018/2019.

Huku ikiwa inashiriki kwa mara ya kwanza baada ya kukosa mashindano kwa takribani miaka mitano, Simba ikiwa chini ya Aussems iliweza kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ambapo ilitolewa kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-1 na TP Mazembe ya DR Congo.

Ilianza kwa kuitoa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1 na katika hatua ya kwanza wakaitupa nje Nkana FC ya Zambia kwa kuichapa jumla ya mabao 3-2 kisha wakatinga hatua ya makundi ambapo waliangukia katika Kundi D lililokuwa na timu za Al Ahly, AS Vita Club na JS Saoura.

Katika hatua hiyo ya makundi walimaliza wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Al Ahly wakikusanya pointi tisa baada ya kupata ushindi katika mechi tatu na kupoteza tatu kabla ya kukwaa kigingi mbele ya Mazembe katika robo fainali.

Hata hivyo baada ya kutamba msimun uliopita, mambo hayakuwa mazuri kwa Aussems msimu huu kwani walijikuta wakiondoshwa mapema na UD Songo ya Msumbiji katika raundi ya awali kwa sheria ya bao la ugenini.

Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana huko Msumbiji na katika mchezo wa marudiano hapa nchini zilifungana bao 1-1.

Kiujumla chini ya Aussems, Simba imecheza jumla ya michezo 14 ya Ligi ya Mabingwa Afrika, imepata ushindi katika mechi sita, imetoka sare mitatu na imepoteza mechi tano, huku ikiwa imefunga mabao 20 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 22.
 
Hata Kerr aliwaambia ni mbumbumbu........
 
Dah Huku chedema wanatoa boko uku simba wanazingua bora nijuvutie zangu bange tu
 
Nimesoma mahali kuwa Ausems amefunguka juu ya usajili kuwa mchezaji aliyempendekeza na akasajiliwa ni Kahata peke yake na vile vile hakutaka Okwi na Kotei waondoke na hata wabrazili hakuwapendekeza yeye na hawana uwezo wa kucheza ligi ya Afrika. Iwapo hii taarifa ni kweli na si uzushi wa mwandishi basi nafikiri Simba kuna tatizo kubwa sana. Kama pamoja na uwepo wa MO mambo ya hovyo kiasi hiki yanafanyika kwenye usajili basi tuliotegemea Simba iende anga za TP Mazambe, Alhaly, n.k. tutakuwa tunaota ndoto za mchana.

Klabu kubwa kama Simba inatakiwa iwe na timu ya watu watatu mpaka watano kwa ajili ya kufanya scouting ya wachezaji ndani na nje ya nchi ambayo itakuwa inafanya kazi kwa ukaribu na benchi la ufundi. Mwisho wa siku kocha mkuu ndiye awe mwenye uamuzi wa mwisho nani asajiliwe na sio viongozi.
 
Alimpendekeza Shiboub peke yake. Wengine wote hao ni dili za watu kula hela ya Mhindi.
Mbrazil atoke India aje Bongo? Halafu mishahara yao so haba. Watu wana percent zao humo.
 
Nyie vyura! mbona naona kama hata huyo Mkwasa mnataka kumtimua? Acheni kujadili ya Aussems bali jadilini yanayowahusu, hasa namna ya kuwapa rupia waamuzi ili waendelee kuwabeba (kama yule aliwabeba juzi dhidi ya KMC).

Jadilini pia mtawezaje kupunguza idadi ya magoli ya kufungwa kutoka 4 - 0 hadi 3 - 1 kwenye mechi ijayo ya Simba vs Yanga.
 
Back
Top Bottom