Hii habari ni ya muda kidogo, japo humu imeingia leo na sasa Mabele alishaanza kufanya mazoezi show ya mwisho aliifanya 2009 huko Paris tena akiwa bado anaumwa.
Niliifuatilia hii habari miaka kadhaa iliyopita, ni hivi huyu jamaa alipoanzisha group la Loketo walikuwa share na Diblo Dibala kama wamiliki!!
Ulipofika muda wa mgao wa faida Diblo
inasemekana akamdhulumu Mabele akachikichia mapato yote na kumuacha mchizi Mabele na visenti tuu hali iliyopelekea kupata stress na mwisho wa siku stroke!!
Sasa mtu kesha broke na stroke juu, mke kajionea mauza uza akasepa! Jamaa kajiuguza kwa shida sana mpaka kupata msaada wa serikali yake.
Ila mpaka dakika za mwisho kulikuwa na amsha amsha ya wasanii nguli wa dance lile la miaka 90 wafanye show wampe msaada, na yeye pia alikuwa ana courage atapona aimbe apate pesa tena. Sikufuatilia baada yaa hapo
Miongoni mwa habari ilowahi kuniumiza aiseee namkubali sana Mabele toka enzi za albam yao ya Extra Ball, ila favourite song yangu ni Choc a Distance!! Mpaka muda huu nikiingia mahali lazima niudunde kidogo.
Kweli maisha hayana formula na kama!! Mabele leo wakutegemea watu wamsaidie, siamini mtu hataaa