Aukata uume wa mbakaji na kuupeleka Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aukata uume wa mbakaji na kuupeleka Polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 31, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanamke mmoja wa nchini Bangladeshi ameukata uume wa mwanaume aliyejaribu kumbaka na kisha kukipeleka kipande cha uume wa mwanaume huyo polisi kama ushahidi.

  Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 aliukata kwa kutumia kisu uume wa mwanaume aliyejaribu kumbaka na kisha alikichukua kipande cha uume huo na kukipeleka polisi kama ushahidi.

  Mwanamke huyo ambaye ni mama wa watoto watatu alishambuliwa na mwanaume huyo wakati amelala usiku wa jumamosi kwenye kibanda chake kilichopo kwenye kitongoji cha Jhalakathi nje kidogo ya mji mkuu wa Bangladeshi, Dhaka, taarifa ya polisi ilisema.


  "Wakati alipojaribu kumbaka, mwanamke huyo alichukua kisu na kuukata uume wake na kisha alikifunga kipande hicho cha uume kwenye nailoni na kukipeleka kwenye kituo cha polisi kama ushahidi wa tukio hilo la ubakaji", alisema mkuu wa polisi Abul Khaer wakati akiongea na shirika la habari la AFP.


  Mwanamke huyo alifungua kesi polisi akisema kuwa mwanaume aliyejaribu kumbaka ambaye naye pia ana umri wa miaka 40 ambaye pia ni baba wa watoto watano, alikuwa akimsumbua sana kwa miezi sita sasa.


  Kipande cha uume wa mwanaume huyo kilihifadhiwa kwenye kituo cha polisi kama ushahidi wakati mwanaume huyo mbakaji akiwa na uume wake kibubutu alipelekwa hospitali kwa matibabu zaidi ili kunusuru maisha yake.


  "Tutamtia mbaroni wakati hali yake itakapokuwa nzuri", alisema mkuu huyo wa polisi.
   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Du!! Makubwa.
   
 3. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Monju Begum says her neighbour had been harassing her for months

  Police in southern Bangladesh say a woman cut off a man's penis during an alleged attempt to rape her and took it to a police station as evidence.
  The incident took place in Mirzapur village, Jhalakathi, about 200km (124 miles) south of the capital, Dhaka.
  Monju Begum, 40, a married mother of three, told police that neighbour Mozammel Haq Mazi forced his way into her shanty and started assaulting her

  BBC News - Bangladesh woman cuts off 'attacker's' penis
   
 4. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Du hii kali,kwa style hii lazima matukio ya ubakaji yapungue
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  safi sana...
   
 6. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  miamia
   
 7. mchakavumlasana

  mchakavumlasana JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  excellent!!
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kajichukulia sheria mkononi!!!!
   
 9. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Huyu yuko serious hataki utani. Ila wa TZ wanatabia ya kuchomekea mtu kesi wakati walikubaliana
   
 10. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Bravo! Huku bongo angeambiwa asaidie polisi na cash zingemtoka!
   
 11. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  It's well 'n good
   
 12. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  safi! sasa kile kijiti ukikikata nacho kinacheza kama vile kidole au?
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ama kweli kua uyaone................sio magorofa
   
 14. M

  Mocrana JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mmh sijaelewa kwa hiyo huyo jamaa alishamtaarifu atakuja kumbaka akatayarisha kikatio kabisa, lol
   
Loading...