Augustine Mahiga: Mwanadiplomasi anayeheshimiwa kuliko wote Tanzania

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
774
1,456
Gazeti la Rai mwema toleo la 391la February 4, 2015 limemtaja kuwa perhaps ndie mwanadiplomasia anayeheshimika kuliko wote nchini Tanzania.

Pia limesema kuwa ni moja katiya watu wachache nchini Tanzania anayefaa kuwa Rais lakini hataki wala hana nia ya kuwa Rais.

Ni Muanzilishi wa idara ya Usalama wa taifa Tanzania na ni Mkurugenzi wa Kwanza


Mfahamu zaidi: WASIFU



Augustine Philip Mahiga (born28 August 1945) is a Tanzanian diplomat. He previously served as the PermanentRepresentative of Tanzania to the United Nations, and later as the UN Special Representativeand Head of the United Nations Political Office for Somalia.

EARLYHISTORY
In 1971, he earned a Bachelor of Arts (Education) at the Universityof East Africa in Dar es Salaam, Tanzania. That same year, Mahiga completed aMasters of Arts at the University of Toronto (U of T). He also received a PhDin International Relations in 1975 from the same institution. Mahiga is marriedand has children




CURRICULUMVITAE

DR. AUGUSTINE PHILIP MAHIGA

PERSONALDATA Name:Augustine Philip Mahiga

Dateof Birth: 28 August 1945 Nationality:Tanzanian

MaritalStatus: Married

EDUCATIONQUALIFICATIONS 1975Doctor of Philosophy (PhD) in International Relations, Universityof Toronto 1971Master of Arts (M.A.), University of Toronto, 1970 Bachelor of Arts withEducation (B.A. Ed.


Honors. University of East Africa, Dar-es-Salaam

SUMMARYOF WORK EXPERIENCE
2005 -
Ambassador,Head of the Tanzania Delegation to the United Nations Security Council
2003 - Present - AmbassadorExtraordinary and Plenipotentiary,
presentPermanent Representative of the United Republic of Tanzania to the UnitedNations
2002 - 2003 UNHCR, Representative to Italy, Republic of Malta, Holy See andRepublic of San Marino.
1998 - 2002 UNHCR, Chief of Mission (Representative) in New Delhi,India.
1994 - 1998 Coordinator andDeputy Director of the Great Lakes Region of Africa Refugee Emergency Operationbased in Geneva.
1992 - 1994 UNHCR Chief ofMission (Representative) in
Monrovia, Liberia.
1993 Appointed bythe Government of the United Republic of Tanzania to the rank of Ambassadorwhile on secondment to UNHCR.
1989 - 1992 MinisterPlenipotentiary, Tanzania Permanent Mission to the United Nations in Geneva.

1977 - 1980 Director of Research andTraining, President?s Office, Dar-es-Salaam, Tanzania.
1975 - 1977 Senior Lecturer in International Affairs and Regional Cooperation, University ofDar-es-Salaam, Tanzania


PUBLICATIONS AND INTERNATIONAL CONFERENCE PAPERS

- Empowerment of Women and Millennium Development Goals in Empowerment of Women, Partners in Population and Development Publication, New York, 2004

- Forward to Refugees and the State Practices of Asylum and Care in India, 1947- 2000, Edited by Ranabir Samaddar, New Delhi, Sage Publishing, 2003

- Water Resources, Human Displacement and International Security (Paper presented to the Gorbachev Foundation Peace Conference, Rome, Italy, November 2002

- Demography Strategic Imperatives and Displacements in South Asia (Lecture delivered to the National Military Academy, New Delhi,India, 2001)


- Reconciling Refugee Protection and National Security(Paper presented to the University of Pune, Pune, India and Habitat Centre, New Delhi, India, 2001)

- Globalization and Forced Migrations (Lecture at the Press Club, Madras, India)

- International Response to the Post-Genocide Rwanda Emergency?, Reference document at Oxford University, Refugee Studies website


- Confidence Building Measures in Africa?, published by the United Nations Institute for Disarmament Research (UNIDIR)

- Pitfalls and Promises of East African Integration "TAAMULI" Journal of Political Science, University of Dar-es-Salaam

- Disarmament and Development in Africa (Paper presented to the Palme Commission Conference on Disarmament and Development, New Delhi, India,1986)

- Conflict Resolution and Security in Africa (Paper presented at a Conference on Conflict Resolution in Africa, Lome, Togo, 1989)


- Confidence Building Measures in Africa?, published by the United Nations Institute for Disarmament Research (UNIDIR)


=======

JUNI 10, 2015: Dkt. Mahiga achukua fomu kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MWANADIPLOMASIA maarufu, Balozi Dk Augustine Mahiga ametangaza nia kukiomba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumfikiria na hatimaye kupendekeza ili apate fursa ya kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania.

Dk Mahiga pamoja na nia yake amekuja na vipaumbele vyake kuwa ni kuleta umoja, amani na maadili, kupambana na rushwa na ufisadi, kukuza uchumi na kuimarisha uhusiano wa kimataifa.

Akitangaza nia jana mbele ya waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa ni haki yake, lakini pia amepata fursa ya kuielewa nchi yake, dira, uchumi, siasa na utamaduni wake na kuitangaza ndani na nje ya nchi.

“Ningependa kusimama na kugombea nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Nimetafakari muda mrefu na nikafikia muafaka wa kujitosa katika kinyanganyiro hiki, naomba nifikiriwe na hatimaye kupendekezwa na kupata fursa ya kuongoza taifa hili,” alisema.

Vipaumbele vyake

Mwanadiplomasia huyo alibainisha kuwa akichaguliwa, jambo la kwanza litakuwa kuandaa miongozo ya nchi na kutekeleza ilani ya CCM kwa nguvu zote.

Balozi Mahiga, aliyeanza hotuba yake kwa kueleza wasifu wake wa elimu na mafanikio ya kazi zake mbalimbali alizofanya ndani na nje ya nchi, alisema akipata ridhaa kipaumbele chake cha kwanza ni kuimarisha misingi ya Taifa ambayo ni umoja, amani na maadili.

Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni mkakati wa kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kipato cha kati na kukuza uchumi kwa kupambana na umaskini, kukuza kilimo, viwanda, uchukuzi, na utalii.

Dk Mahiga, ambaye kabla ya kustaafu alikuwa mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia na mkuu wa ofisi ya siasa za Somalia (UNPOS), alisema atashughulikia uboreshaji wa mfumo wa elimu, kuimarisha uhusiano na Jumuiya ya Kimataifa na kukabiliana na changamoto mpya za vitisho vya ugaidi na biashara ya dawa za kulevya.

Alifafanua kuwa kwa muda mrefu umoja wa nchi, umekuwa ukiyumbishwa na watu wachache wenye masilahi binafsi, hivyo atapambana nalo kwa karibu iwapo atapata fursa ya kuiongoza nchi baada ya kupitishwa na CCM.

“Umoja wetu ulikuwa ni nguvu pekee ya kumwondoa mkoloni, kupambana na udini, ukabila, ukanda na ndiyo uliofanikisha mapinduzi ya Zanzibar na kuanzisha Jamhuri ya Muungano Tanzania,” alisema Balozi Mahiga.

“Lakini sasa tumeanza kuona uadui, ukabila, ukanda na hata rika… mara hee wazee, mara vijana. Pia, tumeanza kuona watu wachache wanayumbisha Muungano wetu, umoja ukiyumba na amani itayumba.”

Kwa kutumia uzoefu wake katika kusuluhisha amani nchi za Afrika Magharibi na ukanda wa Maziwa Makuu, Balozi huyo alisema: “Nitasemea hilo kwa uchungu na nisingependa uvunjifu wa amani usitokee nchini.”

Alisema Tanzania inapitia katika kipindi kigumu kwa sababu za kiitikadi, hivyo njia pekee za kujinasua ni kutatua kero za Muungano, kuruhusu uwanja mpana na wa wazi wa ushiriki wa vyama vya siasa na kuimarisha taasisi za kidini, Serikali na asasi za kiraia.

“Nadhani hizi kero za Muungano zimejadiliwa na kupatiwa majawabu. Zikipatikana katika Katiba mpya zitawaridhisha Wazanzibari na watu wa Bara na kudumisha amani na umoja,” alisema.

Hata hivyo, alipoulizwa iwapo akipata urais atabadilisha Katiba Inayopendekezwa ili kutatua baadhi ya kero za Muungano zinazolalamikiwa ukiwamo Muundo wa Muungano, alijibu; “katika siasa kuna mambo mengi yanayoweza kutokea” na kwamba mchakato wa Katiba ni shughuli endelevu.

Pia, alisema iwapo atapata ridhaa hiyo, kuna ulazima wa kuufanya mfumo wa vyama vingi kuwa wa kidemokrasia zaidi. “Lazima tujifunze kuwa na utamaduni wa vyama vingi. Ushindani wa kisiasa usiwe mapambano na kuyumbisha amani na umoja,” alisema.

Kwa muda mwingi, Balozi Mahiga alikuwa akisisitiza maadili ya viongozi na nchi akisema kuwa yataimarishwa kwa kukuza uzalendo, uadilifu, uwajibikaji na ukweli. Alisema kwa kipindi kirefu maadili nchini yameanza kuporomoka, hivyo suala hilo halitakiwi lizungumziwe kirahisi, bali ni lazima livaliwe njuga
.
“Tusiogope kujikosoa, kukosolewa kuwa maadili yamemomonyoka na yanatakiwa kushughulikiwa na kuboreshwa. Jambo la haraka ni kupambana na udanganyifu, rushwa na ufisadi ambao kwa ujumla ni wizi tu,” alisema.

Alisema mapambano ya rushwa na ufisadi yanapaswa yafanyike katika chama na uchumi.

Atangaza vita dhidi ya ufisadi

“Siyo kwamba haya mambo ya uhujumu uchumi hayakuwapo, yalikuwapo tangu zamani… nakumbuka nilipokuwa Usalama wa Taifa pamoja na Marehemu (Waziri Mkuu wa zamani Edward Sokoine) tulipambana sana.

“Lakini sasa watu wachache ni wala rushwa na mafisadi, wakiachwa wanaweza kuliangamiza Taifa na ina madhara makubwa kiuchumi na kwa heshima ya Tanzania,” alisema.

Alisema kuna haja ya kufanya uratibu wa kupambana na ubadhirifu wa kisiasa ili kuliwezesha Taifa kuwa na mwelekeo mpya wa siasa usio wa kuuza au kununua kura na utu.

Balozi huyo pia aligusia suala la matumizi ya fedha kwenye uchaguzi akisema inabidi yawekewe ukomo.

“Lazima kuwe na kikomo cha kugombea nafasi mbalimbali na matumizi ya fedha. Chama kitoe fursa ya kugombea na kuchaguliwa kwa kila mtu… tusifike mahali uwezo wa kuchaguliwa ukawa mikononi mwa wenye fedha,” alisema.

“Kuwe na uwazi katika chaguzi ili usitengenezwe mwanya kati walionacho na wasionacho na matabaka siyo dhamira ya CCM.”

Kama ilivyokuwa kwa wagombea wengine waliotangulia, Balozi Mahiga alitumia muda mrefu kuzungumzia rushwa kwa kina akieleza kuwa ili kupambana na ufisadi wa kiuchumi atatangaza vita maalumu.

Alisema ufisadi ni kuliibia Taifa na vita hiyo ikitangazwa kama kampeni maalumu kama ilivyokuwa katika kuwezesha wanawake, mwelekeo imara wa taifa utapatikana.

Utekelezaji wa kukomesha ufisadi na uonevu utafanyika kwa kubadili mfumo wa Serikali na sheria ili kutoa haki kwa watu wote.

Ili kukuza uchumi, alisema: “Kuna haja ya kupambana na umaskini kwa kuwawezesha Watanzania wa kawaida kuongeza pato lao mifukoni na kumudu gharama za maisha.

“Pia, inatakiwa kuipa Serikali uwezo wa kutoa huduma muhimu kwa watu wote. Mkulima, mjasiriamali, mvuvi, mfanyakazi na wengineo ni lazima wazipate huduma bora kwa haki bila kununua.”

Alisema inatakiwa kuboresha mfumo wa kuendesha uchumi wa kuendesha soko huria na sekta binafsi ambao utatatua tatizo la ajira, masoko na uwekezaji.

Alisema iwapo sekta binafsi na serikali zitashirikiana kwa pamoja, zitafanya kazi ya kubaini mwelekeo wa Taifa wa uchumi na idadi ya watu kwa kuzingatia ongezeko la tatizo la ajira kwa vijana.

“Suala la kuwawezesha vijana liingizwe kwenye mfumo wa Serikali. Kila kiongozi ajiulize ubunifu wangu unanipeleka wapi kujibu changamoto za vijana,” alisema

Balozi Mahiga alieleza kuwa katika kilimo ataweka kipaumbele katika kutatua matatizo ya migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima au wakulima na wakulima.

Alisema kuwa baada ya hapo ataandaa mfumo madhubuti wa kukuza kilimo kwa pamoja kwa kuboresha masoko, uhifadhi wa mbegu bora, na ardhi.

Katika ukuzaji wa viwanda, Balozi huyo aliyejinasibu kuwa alichangia zaidi kuwavutia wawekezaji wa kigeni, alisema atatoa fursa kwa wazawa na wageni kuchangia maendeleo hayo.

“Tutatengeneza mazingira bora ambayo wananchi watashiriki kikamilifu katika viwanda kutokana na mitaji itakayopatikana kwenye kilimo na biashara,” alisema.

“Kwa wawekezaji wa nje tutahakikisha tunawawekea mazingira rafiki ya kuwavutia waje kuwekeza… kwa sasa bado wawekezaji hao wanalalamika kuna vikwazo vinavyowafanya wengine washindwe na kuondoka,”

Pia, alidokeza kuwa katika sekta ya uchukuzi ataweka utaratibu maalumu wenye uwiano baina ya usafiri wa reli, barabara na majini ili visiathiriane.

Alisema suala la uchukuzi linahitaji mipango madhubuti na utekelezaji na iwapo itafanywa vizuri, barabara hazitaharibika wala malori hayatakosa mizigo.

Pia, alieleza kuinua utalii kwa kutunza vivutio vyote hususan vinavyotambuliwa na Umoja wa Mataifa kama urithi, ikiwamo kuzuia ujangili wa wanyamapori.

Balozi Mahiga alisema akiridhiwa na CCM na wananchi kugombea nafasi hiyo, atahakikisha anabadili mfumo wa elimu utakaojikita katika utaalamu na ufundi ili uendane na ushindani wa soko huria.

“Tuachane na ule msemo wa kwamba nimejenga shule 20 au 30 lazima tuangalie na ubora,” alisema.

Masuala yanayompa nguvu

Pamoja na kuonekana kutokuwa maarufu kwenye siasa za ndani, Balozi Mahiga alisema ana uzoefu mkubwa kwa kuitumikia nchi ndani na nje, jambo ambalo anaamini litasaidia kumvusha katika kinyang’anyiro hicho.

“Mchango wangu siyo kitu cha kuonekana mara moja lakini ni mkubwa sana katika maendeleo ya nchi hii,” alisema ofisa huyo mwandamizi wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa. “Nikiwa katika uwakilishi wa Tanzania katika jumuiya za Kimataifa niliweza kuanzisha jukwaa la kuleta wawekezaji na watalii wengi na kuwezesha kuiweka nchi katika ramani… ni kitu ambacho hakipimiki,” alisema.

Plan B

Alipoulizwa endapo hatapitishwa na CCM kuwania urais atamuunga mkono mgombea gani, Balozi Mahiga alijibu kuwa licha ya kujitokeza makada wengi katika kinyang’anyiro hicho kwake anaona ni shule mpya.

“Kati ya wote tunaowania ni lazima atoke rais mmoja, hata viongozi wenzangu watajua kumbe kuna watu wenye uwezo wa kuongoza... kwa kuwa tunaendelea na mchakato siwezi kusema nani ntamuunga mkono… atakayepita tufanya kazi kama timu,” alisema.
 
Ifike siku Watanzania waanze kuangalia nakuthamini ubora wa KIONGOZI kwa SERA na VISION zake kwa UJENZI wa Taifa licha ya kuwa na CV nzuri.
 
Hivi vinyago tulivyonavyo hatujamaliza kuvichezea sasa unatuletea vinyago vipyavya nini? isitoshe hivi sasa vinyago vyenye uzungu mwingii na kujifunika mikaratasi kibao(vyeti) hatuna haja navyo tunataka vya hapa hapa mradi vijue nyimbo zetu na ngoma zetu!
 
watu wengi wanamponda kwa sababu wamekuwa wakifuatilia siasa za magazeti lakini jamaa yuko very smart amekuwepo toka kipindi cha marehemu Sokoine ndio watu waliokuwa wakifanya kazi kwa ufanisi na kufanya serikali ionekane inafanya kazi bila kujulikana na bahati nzuri hana scandal ni miongoni mwa watu wachache ambao kama kweli ccm itatumia mtindo wa kushawishi agombee na yeye atakuwemo hata wakina lowasa wanajua kabisa jina lake likifika kwa uadilifu na uwezo amewaacha mbali
 
watu wengi wanamponda kwa sababu wamekuwa wakifuatilia siasa za magazeti lakini jamaa yuko very smart amekuwepo toka kipindi cha marehemu Sokoine ndio watu waliokuwa wakifanya kazi kwa ufanisi na kufanya serikali ionekane inafanya kazi bila kujulikana na bahati nzuri hana scandal ni miongoni mwa watu wachache ambao kama kweli ccm itatumia mtindo wa kushawishi agombee na yeye atakuwemo hata wakina lowasa wanajua kabisa jina lake likifika kwa uadilifu na uwezo amewaacha mbali
 
Kuna wakati Bernard Membe alichemka baada ya Tanzania kupatwa na kashfa ya kuwauzia silaha waasi wa Congo.

Bernard Membe, kwa akili zake fupi, alipoulizwa swali la mtego kama ana uhakika hakuna mfanyakazi wa serikali ya Tanzania anayehusika na kashfa hii, alikataa katakata kama vile ana kurunzi inayowamulika na camera inayowarekodi wafanyakazi wote wa serikali ya Tanzania, kwa muda wote, na kisha kuhakiki nyendo zao zote.

Serikali baada ya kuona Membe kaharibu, ikampa kazi Balozi Dr. Mahiga kusawazisha mambo. Muda huo alikuwa New York kama balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

Balozi akaenda on a PR campaign kusafisha jina la Tanzania. Akasema serikali ya Tanzania haihusiki na biashara haramu ya silaha. Alipobanwa kwa mtego kuhakikisha kwamba, hata kama serikali ya Tanzania haihusiki, hakuna mfanyakazi wa serikali aliyehusika, akaweza kuruka mtego kwa kisema ni vigumu kujua nyendo zoye za watumishi wote wa serikali kwa mara moja, na kwamba uchunguzi wa serikali ukishirikisha vyombo vya kimataifa unaendelea. Baadaye kidogo balozi wa Tanzania Burundi akatolewa.

Ukiongea au kumsikiliza Dr. Mahiga hata kabla hajasema yeye ni Dr. unaona usomi. Sio kama ma Dr. fulani hata ukiambiwa huyu Dr. unapata maswali.

Mtu kama Dr. Mahiga kuwa rais ni kazi kwa sababu hajihusishi sana na mitandao ya kisiasa na kakaa sana nje ya nchi.

Hapo ndipo utaona wanaoweza urais hawasikiki sana, wanaosikika sana hawawezi.
 
Na hii habari kuwa ni jasusi mubaya na file la balali linamhusu vipi?
Yes ni huyu ndiye alie bumbulua ule mpango wa Father Tom na kina Hatty McGhee kuipindua serikali ile 1982!. Yeye ndie alikuwa PW-1 akitambulishwa kwa jina la Mr. X!. Huyu urais wa bongo kwa sasa, hauwezi kabisa!, kwa sababu rais wa 2015 tayari aliishapatikana, yupo, na tunaye, anasubiri tuu kuapishwa!, hivyo msimpotezee muda mzee wa watu!. Si mmeona jinsi tumemuajiri yule former spy chief?, atusimame mambo yetu!. Labda kama hana shughuli nyingine yoyote ya kufanya, tunaweza kumchukua awe usaidizi wa aliyepo!.

Pasco.
 
Kuna wakati Bernard Membe alichemka baada ya Tanzania kupatwa na kashfa ya kuwauzia silaha waasi wa Congo.

Bernard Membe, kwa akili zake fupi, alipoulizwa swali la mtego kama ana uhakika hakuna mfanyakazi wa serikali ya Tanzania anayehusika na kashfa hii, alikataa katakata kama vile ana kurunzi inayowamulika na vamera inayowarekodi wafanyakazi wote wa serikali ya Tanzania, kwa muda wote, na kisha kuhakiki nyendo zao zote.

Serikali baada ya kuona Membe kaharibu, ikampa kazi Balozi Dr. Mahiga kusawazisha mambo. Muda huo alikuwa New York kama balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

Balozi akaenda on a PR campaign kusafisha jina la Tanzania. Akasema serikali ya Tanzania haihusiki na biashara haramu ya silaha. Alipobanwa kwa mtego kuhakikisha kwamba, hata kama serikali ya Tanzania haihusiki, hakuna mfanyakazi wa serokali aliyehusika, akaweza kuruka mtego kwa kisema no vigumu kujua nyendo zoye za watumishi wote wa serikali kwa mara moja, na kwamba uchunguzi wa serikali ukishitikisha vyombo vya kimataifa unaendelea. Baadaye kidogo balozi wa Tanzania Burundi akatolewa.

Ukiongea au kumsikiloza Dr. Mahiga hata kabla hajasema yeyr ni Dr. unaona usomi. Sio kama ma Dr. fulani hata ukiambiwa huyu Dr. unapata maswali.

Mtu kama Dr. Mahiga kuwa rais ni kazi kwa sababu hajihusishi sana na mitandao ya kisiasa na kakaa sana nje ya nchi.

Hapo ndipo utaona wanaoweza urais hawasikiki sana, wanaosikika sana hawawezi.



Na tatizo linalotusibu watanzania watu kama hawa(Dr. Mahiga) hatuwataki, tunataka wanasiasa wetu wa siasa za majitaka ndo wachukue uraisi.
 
siasa za bongo bila local network ni ngumu, vinginevyo huyu angetufaa sana.
 
Yes ni huyu ndiye alibumbulua ule mpango wa Father Tom na kina Hatty McGhee ile 1982!. Yeye ndie alikwa PW-1 akitambulishwa kwa jina la Mr. X!. Huyu urais wa bongo hauwezi kabisa!, kwa sababu rais wa 2015 tsyari tunaye, anasubiri tuu kuapishwa, hivyo msimpotezee muda mzee wa watu!. Si mmeona tumemuajiri yule former spy chief, atusimame mambo yetu!. Labda yeye tumpe usaidizi!.

Pasco.

Hahahaha Mkuu umenena vyema sana....... Infact rais tayari kashapatikana kilichobaki ni muda wa kumwapisha....
 
Kuna wakati Bernard Membe alichemka baada ya Tanzania kupatwa na kashfa ya kuwauzia silaha waasi wa Congo.

Bernard Membe, kwa akili zake fupi, alipoulizwa swali la mtego kama ana uhakika hakuna mfanyakazi wa serikali ya Tanzania anayehusika na kashfa hii, alikataa katakata kama vile ana kurunzi inayowamulika na vamera inayowarekodi wafanyakazi wote wa serikali ya Tanzania, kwa muda wote, na kisha kuhakiki nyendo zao zote.

Serikali baada ya kuona Membe kaharibu, ikampa kazi Balozi Dr. Mahiga kusawazisha mambo. Muda huo alikuwa New York kama balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

Balozi akaenda on a PR campaign kusafisha jina la Tanzania. Akasema serikali ya Tanzania haihusiki na biashara haramu ya silaha. Alipobanwa kwa mtego kuhakikisha kwamba, hata kama serikali ya Tanzania haihusiki, hakuna mfanyakazi wa serokali aliyehusika, akaweza kuruka mtego kwa kisema no vigumu kujua nyendo zoye za watumishi wote wa serikali kwa mara moja, na kwamba uchunguzi wa serikali ukishitikisha vyombo vya kimataifa unaendelea. Baadaye kidogo balozi wa Tanzania Burundi akatolewa.

Ukiongea au kumsikiloza Dr. Mahiga hata kabla hajasema yeyr ni Dr. unaona usomi. Sio kama ma Dr. fulani hata ukiambiwa huyu Dr. unapata maswali.

Mtu kama Dr. Mahiga kuwa rais ni kazi kwa sababu hajihusishi sana na mitandao ya kisiasa na kakaa sana nje ya nchi.

Hapo ndipo utaona wanaoweza urais hawasikiki sana, wanaosikika sana hawawezi.

Niliisha kuambia uje ugombee, uliichukuliaje ushauri wangu?
 
Sawa, pamoja na VC yake nzuri, lakini umri umemtupa. Tuna Watanzania wasomi wazuriwenye umri mdog ambao watatufaa kuliko mzee huyu msomi.
 
Watanzania watakubali kuongozwa na mtu ambaye haamini kuwapo kwa mungu?

Hahaha, Usifikirie kabisa Mkuu hawatakubali,

Umenikumbusha Ideal State ya Plato, ambayo itaongozwa na Philosopher King, lakini Philosopher ana sifa mbili, moja ni kwamba Ana uwezo mkubwa sana wa kuongoza, mbili ni kwamba Hapendi kabisa Kuongoza.
 
Hahaha, Usifikirie kabisa Mkuu hawatakubali,

Umenikumbusha Ideal State ya Plato, ambayo itaongozwa na Philosopher King, lakini Philosopher ana sifa mbili, moja ni kwamba Ana uwezo mkubwa sana wa kuongoza, mbili ni kwamba Hapendi kabisa Kuongoza.

Halafu akiongozwa na Dr. JK haishi kupiga kelele.
 
Back
Top Bottom