Ryan Herman
Member
- Jul 26, 2019
- 42
- 46
Kila tarehe ya 12 August ni siku ya vijana kimataifa. Kuna mambo mengi ambayo vijana kama nguvu ya taifa na mabadiliko hupitia.
1. Ukosefu wa ajira. Je ni nini kifanyike kuwakwamua vijana kwenye janga hili? Jambo la kusema vijana wajiajiri je ni kweli kuna mazingira wezeshi ya vijana kujiajiri? Kujiajiri ni kuwa na kiasi cha fedha cha kuanza nacho.
Pia wapo wanaomba ajira sehemu mbalimbali na kuambiwa wawe na uzoefu(experience) ya miaka3 na zaidi. Huu uzoefu wanapata wapi ilihali ndio wametoka vyuoni au hata ngazi yoyote ya elimu.
2. Ukuaji wa matumizi ya mitandao ya kijamii. Ni kweli vijana wananufaika na mitandao ya kijamii au ndio kuharibikiwa?
Mitandao ya kijamii husaidia kujifunza mambo mapya hivyo elimu zaidi inahitajika kwa vijana kuhusu matumiz chanya ya mitandao ya kijamii.
3. Afya na elimu.
Hivi ni vitu viwili muhimu kwa vijana kujua au kivipata kama huduma. Vijana wanapaswa kujua afya zao hususani magonjwa yanayoweza kuwaathiri katika ukuaji wao. Elimu juu ya magonjwa inahitajika zaidi hasa magonjwa ya zinaa na yale yanayoweza kuepukika kwa kufata ushauri wa wataalamu.
Elimu ya ujuzi pia inahitajika sio kumaliza elimu za makaratasi na kukaa tu.
4. Matumizi ya madawa ya kulevya.
Hili ni tatizo kubwa kwa vijana ila wanapata msaada gani kuhakikisha wanaweza kukwepa hili tatizo? Kuanzia ngazi ya familia mpaka jamii vijana wasaidiwe kujua matatizo na athari za madawa ya kulevya.
Mambo ni mengi ya kuzungumza na maswali ya kujiuliza kuhusu vijana.
#Happy International Youth Day