Audio: Lema baada ya hotuba yake kukataliwa bungeni

helu

Member
Feb 28, 2015
86
124
Anasema hotuba yake haikuwa mbaya bali ilikuwa na busara ya kusaidia jeshi la polisi.

Suala la Lugumi halikuwa kwa ajili ya kuidhalilisha serikali bali kulisafisha serikali hasa IGP na Waziri Kitwanga. Lema anazidi kueleza kuwa Waziri wa mambo ya Ndani Mh Charles Kitwanga ni rafiki yake na kwamba baadhi ya mambo aliyoandika walijadili na Mh Kitwanga nyumbani kwake wakiwa wanakula ugali.

Mambo kadhaa aliyoandika kwenye hotuba hiyo ni yale ambayo serikali hawawezi kuyasema moja kwa moja hadharani.

Kama anakatazwa kuongea mambo ya msingi kama hayo basi kusoma hiyo hotuba haina maana.
Anamsihi Mh Kitwanga kuyajibu mambo aliyoandika kwenye hotuba yake kimkakati.

Mh Lema anamalizia kwa kusema ana-mmisi Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuwa alikuwa anasemwa sana bungeni lakini hakuingilia mwenendo wa Bunge.

 
Sio mpenzi wa siassa za Tanzania. Ila huwa nawapenda saaana wanasiasa kama wawakilishi ambao wanaongeaga mambo kwa ajili ya Taifa.
Huyu jamaa anachokiongea ni point kabisa. Jamaaa anaongea jambo la KiTAIFA zaidi na anachokiongea, mimi naona alikuwa na nia njema kabisa kwa waziri na jeshi la polisi na kuwataka kama kweli hawahusiki basi wajibu hoja kwa hoja na sio kumwambia aondoe mambo hayo katika hotuba yake.
Mengine siyafahamu ila kwa ufafanuzi alioutoa mwenyewe mi naona alikuwa na nia njema....
Big up kijana Lema naona wana ccm na uccm wao wameshindwa kukuelewa....
 
Back
Top Bottom