Aubin Kramo arejea Tanzania na kwenda Zanzibar fasta akitokea kwao Ivory Coast

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
Kiungo mshambuliaji fundi wa Simba aliyekuwa majeruhi, AUBIN KRAMO amerejea nchini akitokea Ivory Coast na fasta akapanda boti kwenda kuongeza mzuka kikosini mjini Unguja, Zanzibar. .

Kramo aliyekuwa Ivory Coast alikoenda kufanyiwa upasuaji wa goti, alitua jana Alfajiri na jioni yake alienda Zanzibar, huku akiweka bayana yupo fiti na kilichobaki ni kupiga kazi baada ya kushindwa kuitumikia timu hiyo tangu asajiliwe kutoka Asec Mimosas. .

Hata hivyo, daktari wa Simba, Edwin Kagabo alisema anasubiri kumuona nyota huyo kabla ya kutoa taarifa rasmi. Akizungumza baada ya kurejea, Kramo alisema ameimarika kiafya licha ya uwepo wa maumivu madogo na uzito kuongezeka kutokana na kutofanya mazoezi muda mrefu kwa sababu ya matibabu.

Nini maoni YAKo apewe Muda au aachwe dirisha hili dogo??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutibiwa ni jambo jema, ila klabu inatakiwa iondoe kiini Cha tatizo la sivyo wachezaji makini wataogopa kuja kuchezea klabu yenu.
Uko nje mmeanza kueleweka vibaya, Mambo ya kishirikina, viongozi kujihusisha na 10% Kuna i aibisha klabu.
 
Sio kila mchezaji anaamini katika ushirikina mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swala la kuamini ushirikina ni kitu kingine na kuwepo kwa ushirikina ni kitu kingine.

Klabu ambayo CAF wanaitambua kuwa ni kigogo katika ushirikina katika ngazi ya vilabu barani Afrika inakuaje isi msaidie mchezaji ambaye anatatizo lililo wazi.
Ni vigezo gani hivyo mkuu ambavyo CAF wanatumia Kujua hii club Ni kigogo kwenye ushirikina na vice versa ( kutokana na maelezo YAKo )

Natamani nijue Ni vizuri ukinijuza mkuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vigezo gani hivyo mkuu ambavyo CAF wanatumia Kujua hii club Ni kigogo kwenye ushirikina na vice versa ( kutokana na maelezo YAKo )

Natamani nijue Ni vizuri ukinijuza mkuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
Rejea kwenye waraka wa adhabu uliopelekea Simba kuadhibiwa na CAF kwa kufanya vitendo vya kishirikina katika mchezo wao uliofanyika kule south Africa.
Walifafanua vya kutosha.
 
Rejea kwenye waraka wa adhabu uliopelekea Simba kuadhibiwa na CAF kwa kufanya vitendo vya kishirikina katika mchezo wao uliofanyika kule south Africa.
Walifafanua vya kutosha.
We ni k
 
Back
Top Bottom