Auawa na Mdogo wake Baada ya Kumfumania Akifanya Mapenzi na Mkewe

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,130
8,351
Mkazi wa Mahembo Manyanda Manyilizu (40) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mdogo wake baada ya kumfumania akiwa na mkewe.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Dismas Kisusi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Mawemilu.
“Manyilizu alimkuta mdogo wake akifanya mapenzi na mkewe, alivyomuhoji, mdogo wake alichukua kitu akampiga nacho kichwani hivyo alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu katika zahanati ya Kijiji cha Mawemilu,” alisema Kisusi.
Alidai mtuhumiwa na mwanamke walikimbia baada ya kufanya tukio hilo.
 
Hao walipanga mbinu kumuua mdogo mtu maana kama ni hivyo jamaa asingekimbia na mkewe maana kamfumania
 
HUYO mwanamke ni laana. Kawaua wote. Huyu aliekimbia ni maiti inayotembea kwisha habari yake. Kwani hawezi ishi mafichoni milele na hata jsuri ya pesa hana.
Walitakiwa wajue tatizo ni mwanamke. KWA NN KAWACHANGANYA MTU NA DOGO WAKE. Angesimama yote yasingetokea. Kama dogo alikuwa hawezi mchezo kwa nini alikubali kuolewa nae
 
Yaani hii kitu hii kitu hii kitu hii....
Ras Lion ft John Woka. Hakika tumezika wapendwa wetu wengi sana na pia tunaugua au kuuguza wapendwa wetu wengi chanzo kikiwa ni "Hii kitu hii kitu hii kitu hii...."
 
HUYO mwanamke ni laana. Kawaua wote. Huyu aliekimbia ni maiti inayotembea kwisha habari yake. Kwani hawezi ishi mafichoni milele na hata jeuri ya pesa hana.
Walitakiwa wajue tatizo ni mwanamke. KWA NN KAWACHANGANYA MTU NA DOGO WAKE. MWANAMKE Angesimama IMARA yote yasingetokea. Kama dogo alikuwa hawezi mchezo kwa nini alikubali kuolewa nae. MIE nikimfuma mwanake wangu nalia na yeye sio mwanaume. KWANZA KAMA UPO MAKINI UTAMGUNDUA MKEO TABIA ZAKE. Mpaka kuoana bado tu labda mwanaume ndio umekengeuka mpaka kufikia hapo. Usikute huyo demu zamani alikuwa wa kaka mtu sasa anakumbushia. Tatizo kwa nani hapa kama si muoaji
 
Back
Top Bottom