Auawa kwa risasi aliyetaka kuwaibia wapangaji ‘gesti’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Auawa kwa risasi aliyetaka kuwaibia wapangaji ‘gesti’

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 10, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WANANCHI wenye hasira wamemuua mtuhumiwa wa ujambazi aliyekuwa amepanga katika nyumba ya kulala wageni ya Inn’s lodge, iliyopo Kigogo wilayani Kinondoni na kuwajeruhi vibaya wengine watatu waliotaka kuwaibia wapangaji wa nyumba hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema mauaji hayo yalifanyika usiku wa kuamkia jana wakati mtuhumiwa huyo na wenzake watatu wakiwa katika harakati za kuwapora wapangaji wa nyumba hiyo.

  Alisema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye hajafahamika jina lake, alipanga katika nyumba hiyo kwa siku mbili mfululizo akiwa analala ndani bila kutoka nje na kuwataka wahudumu wampelekee kila kitu chumbani kwake.

  Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela ilipofika juzi saa 8 usiku, mtuhumiwa huyo aliwataka wahudumu wa nyumba hiyo kumfungulia mlango atokee nje kwa madai kwamba ana wageni wake anataka awaone lakini wahudumu wakamkatalia.

  Kamanda Kenyela akisema baada ya mabishano ya muda mrefu, wahudumu hao walilazimika kumfungulia mlango na ghafla waliingia watu watatu wakiwa na silaha na baruti.

  Alisema watu hao walianza kupita chumba kimoja baada ya kingine na kuwapora wapangaji ambao walipiga kelele na kuomba msaada kutoka kwa majirani.

  Kutokana na kelele hizo, mmoja wa wananchi wa eneo hilo akiwa na bastola yake alifika katika nyumba hiyo na kumfyatulia risasi mtuhumiwa huyo ambaye alikufa papo hapo na wengine watatu walijeruhiwa na hali zao ni mbaya.

  Katika tukio jingine, Polisi inamshikilia Alfonce Douglas (24), mkazi wa Kinondoni kwa kosa la kupatikana na gari la wizi aina ya Toyota Mark 11, iliyobandikwa namba bandia T 389 AKR.

  Uchunguzi wa awali uliofanywa na Polisi ulibaini kuwa namba halisi ya gari hilo ni T
  658 AVZ ambalo liliibwa Janauri 2, mwaka huu huko Masaki katika hoteli ya Sea Cliff.
   
Loading...