Auawa baada ya kukataa kulipia gongo aliyokunywa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Auawa baada ya kukataa kulipia gongo aliyokunywa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FOE, Sep 27, 2009.

 1. F

  FOE Member

  #1
  Sep 27, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JESHI la polisi linamshikilia mwanamke wa Kitongoji cha Manyata Kijiji cha Nyichoka Kata ya Kyambahi wilayani hapa, kwa tuhuma za kumuua mteja wake kwa kumchoma kisu.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Lebaratus Barlow aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, mtuhumiwa huyo alimchoma kisu Mapinduzi, Thomasi Bisoti (32) na kufa papo hapo.

  Alisema tukio hilo lilitokea Septemba 21 mwaka huu, saa 4:00 usiku nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, ambako marehemu alikuwa akinywa pombe ya kienyeji aina ya gongo.

  Alisema chanzo cha mauaji hayo ni Bisoti, ambaye alifika kilabuni hapo akiambatana na mwanamke mmoja aliyedaiwa kuwa hawara yake, kunywa pombe na kugoma kulipa.

  “Kulitokea kutoelewana kati yao, kuhusu malipo ya Sh1,000 hali iliyopelekea mtuhumiwa huyo, ambaye alikuwa akiuuza gongo na aliyekiri kosa kumchoma kisu kifuani upande wa kushoto hadi kwenye moyo na kufa papo hapo,”alisema Kamanda.

  Kamanda alieleza kuwa baada ya tukio hilo wanywaji waliokuwepo walimkamata na kumfikisha polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazomkabili. source: Mwananchi 27/09/2009
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Maisha bora kwa watanzania
   
 3. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kinywaji sio cha halali, mke sio halali(hawara). Halafu hao waliompeleka mtuhumiwa polisi nao ilipaswa washikwe kwa kunywa pombe haram hiyo.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kazi kweli kweli
   
Loading...