Atupwa jela miaka 25 kwa wizi cheti kidato 4

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,833
18,830
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miaka 23 mkazi wa kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26).

Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mshtakiwa kukiri kosa mahakamani.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Swai alisema mtuhumiwa amekutwa na hatia pasipo shaka hivyo anahukumiwa kwenda jela 23. Awali, Mwendesha Mashitaka, Baraka Hongoli alisema mshitakiwa alitenda makosa ya kuvunja na kuiba Mei 25 mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwa Veronica Crispin katika Kijiji cha Kalovye, Inyonga.

Alidai kwamba mshitakiwa alifika nyumbani hapo, akavunja na kisha kuiba nguo zenye thamani ya Sh 110,000 na cheti cha kidato cha nne cha Henreth Edward Kalamu, kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mwaka 2015.

Hongoli aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mtu huyo ili iwe fundisho kwa kuwa wizi wa aina hiyo ndio umesababisha usumbufu na watu kupoteza ajira zao serikalini na maeneo mengine pindi uhakiki wa vyeti unapofanyika.

Akijitetea, mshitakiwa aliiomba mahakama impatie muda ili aweze kwenda Dar es Salaam kumtafutia mtu huyo cheti kingine
 
Bashiteeeeeeeeeee! umeona hii? Mwenzio katangulia lupango nawe jiandae ila angalia ngongingo ulilonalo lisije kuleta maafa jela
 
Angeiba cha degree hakika angenyongwa, angeiba cha form six ni miaka 50, cha deploma ni maisha..

Ila nadhani hiyo adhabu haitokani tu na wizi wa cheti, kuna hiyo kuvunja sijui wanaita robbery au kitu kama hicho..
 
Ila kosa lililomfunga miaka hiyo 23/25 si kuiba cheti bali "kuvunja na kuiba". Title ya mada yako (au gazeti) inaleta impression kwamba kafungwa kwa kuiba cheti which is wrong!
 
Dunia haipo fair...huyu kaiba tu cheti cha form four jela miaka 25..mwingine yule alihonga nyumba za serikali kwa hawara zake yupo tu uraiani anapeta tena ckuhz ndo anajifafanya anauchungu na rasilimali zetu na kujifanya mungu mtu wa kuwatumbua wenzie
Tye teh teh teh teh eti anasema ana uchungu na Nchi! Kwanza ile mahakama ya mafisadi sijui ipo wapi maana aliyeaianzisha naye ni fisadi kuanzia ule mkangafu wa kwenda bagamoyo mpaka mijengo ya serikali
 
Mwandishi mwenyewe umeiba hii habari na hata hujaisoma.
Heading inasema miaka 25. Habari yako inasema 23.
Rekebisha Johnny Sack
 
Back
Top Bottom