Kakende
JF-Expert Member
- Aug 18, 2012
- 2,741
- 1,233
Ndugu zangu Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu. Kwa muda sasa kumekuwa na viashiria kuwa nchi yetu Tanzania imekuwa ikinyemelewa na mabepari hasa baada ya kugundulika kuwa ina rasilimali nyingi kama vile madini, gesi, hifadhi za wanyama n.k. Nchi hii ina madini karibia kila kona ya nchi, Aliekuwa waziri wa nishati na madini aliwahi kusema kuwa madini yaliyochimbwa mpaka sasa hata asilimia 2 ya madini yote hayajaguswa.
Kumekuwa na taarifa kuwa katika tani 20 za madini yanayochimbwa Tanzania, ni tani 2 tu zinapitia kwenye njia sahihi za ukaguzi, hivyo tani 18 zinaibiwa. Kenya na South Africa ndiyo zinaongoza kwa kuuza TANZANITE duniani wakati madini haya yanapatikana Tanzania tu
Ndugu zangu, Rais wa CHINA alikuja hapa akaingia mikataba ya siri 29 na Serikali yetu. Huyo Rais pia aliahidi kujenga Bandari ya Bagamoyo, inasemekana ujenzi huo ni kutokana uwepo wa Gesi Mtwara. Kwanini Serikali imeingia mikataba ya gesi kwa siri bila kuwa na sheria wala sera ya GESI?
Pia kuna taarifa kuwa OBAMA anakuja na ujumbe wa watu 700 hapa Tanzania.Mimi binafsi siamini kama kuna taifa ambalo limejipanga kusaidia taifa lingine
Ndugu zangu swali la kujiuliza, Kwanini Clinton (X2) alikuja, kwanini Bush (X2) alikuja, kwanini Obama anakuja, kwanini Rais wa china alikuja?. Hapo kuna jambo maana mkono mtu mtupu haulambwi
Ndugu zangu sina shida na wawekezaji, lakini je Watanzania tumejipanga kushindana na hao wawekezaji?, au ndiyo yale mambo ya wao wanachukua asilimia 97 na sisi tunachukua aslimia 3?. Je tuna vijana ambao wana uzoefu na uchimbaji wa madini na gesi ambao wanaweza kuchukuwa pia zile top positions?, au watabaki kuwa vibarua wa kusogeza udongo wasijue hata madini yanapimwaje?. Kutokana na hali mbaya ya kielimu hapa Tanzania ninaamini kabisa madini yetu yataporwa bila sisi kujua
Vijana wenzangu. Tusipokuwa makini kupigania nchi yetu tutajikuta baada ya miaka kadhaa nchi yetu inabaki kama magofu huku madini yakienda kujenga uchumi wa nchi za watu. Tukae tukijua kuwa madini ni NONE RENEWABLE RESOURCES hivyo yakiisha yamekwisha. Madini si kama mpunga kwamba mwaka huu ukivuna na mwakani utalima na kuvuna tena.
MAONI YANGU.
-Vijana wa Tanzania tusikubali uporaji wa rasilimali zetu kirahisi, popote pale tukatae. Kama Tanzania ni nchi ya madini Serikali ilitakiwa ifanye uwezeshaji, ipeleke Vijana wengi sana nje wakasome mambo ya madini. Laa sivyo vizazi vyetu vitakuta TANZANITE IKIWA KWENYE MAJUMBA YA MAKUBUSHO (MUSEUM).
-Kwa kuwa sasa vijana ni wengi katika nchi hii, inabidi tuunde umoja wetu ambao utakuwa unahamua ni chama kipi tukiweke madarakani hasa kutokana na jinsi gani kitalinda Rasilimali za nchi.
-Serikali iende nchi za Kiarabu ijifunze wao wanaingiaje mikataba na wawekezaji
MKONO MTUPU HAULAMBWI, TANZANIA KUNA KITU NDIYO MAANA MABEPARI WANAKUJA KULAMBA NCHI YETU HUKU TUKIWA HATUNA ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU MADINI