Afadhali wao wana serikali lakini sisi wanatuibia bado pm wetu anasema nchi itayumba, huku wakifurahia maisha ukiinua mdomo tu unang'olewa meno na kucha kama sio kuuwawa kabisa. Huwa najiuliza hivi hawa tunaojiita viongozi wetu ni kweli vingozi au ni kikundi cha wahuni/mafia fulani?, kama si kundi la wahuni/mafia mbona hawaheshimu katiba na sheria zilizowekwa? Mbona wakiiba ndio wanazidi kupanda chati ndani ya chama na serikali? Na bado wapumbavu fulani (raia) wanawapigia upatu eti yule ana hela anafaa kuwa raisi, hivi kumuunga mkono jambazi sugu kuna fahari gani? Poleni sana wakara kwani hata mkiwa na sifa njema zote hamtachaguliwa, siku hizi sifa za kiongozi ni wizi, rushwa na kununua vyombo vya habari.