Atolewa utumbo kwa kugombania mwanamke

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Jamani huko Songea kuna mambo!

Atolewa utumbo kwa kugombania mwanamke
Na Joseph Mwambije,Songea
Saturday Apr 26, 2008

MKAZI wa kijiji cha Namanguli wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma ameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu tumboni na utumbo mkubwa kutoka nje katika ugomvi wa kugombea mwanamke.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Falhum Mshana amemtaja marehemu kwa jina la Majidu Chowo (60) na kwamba tukio hilo lilitokea Machi 20, mwaka huu katika Kijiji cha Namanguli wilayani humo.

Akifafanua kuhusu tukio hilo Kamanda Mshana alisema marehemu alikuwa na mke aliyekuwa akiishinaye aitwaye Asia Nchimbi (35). Alisema marehemu alizaa watoto kadhaa na mwanamke huyo na kwamba ukatokea ugomvi baina yao na kufikia kutengana. Hata hivyo alisema baada ya kutengana bado walikuwa wakitembeleana.

Alisema baada ya kutengana na mumewe Asia Nchimbi alimpata hawara aitwaye Nasibu Konde (26) ambaye alimwambia hana mume kwani aliyekuwanaye wameachana.

Mshana alisema siku ya tukio majira ya Saa 2:00 Usiku Hawara wa Nchimbi kijana Nasibu Ndonde alimtembelea mpenzi huyo na kumgongea na kufunguliwa mlango na Majidu Chowo na akamuhoji yeye ni nani aliyelala na mpenzi wake na akajibiwa kuwa huyu ni mke wake.

Katika majibizano hayo Kamanda alisema zikatokea ghasia kubwa ambapo Konde akachomoa kisu na kumchoma Chowo tumboni na kusababisha utumbo mkubwa kutoka nje.Mtuhumiwa wa mauaji hayo Nasibu Konde ameshafikishwa Mahakamani.

Source: Gazeti la Maisha
 
Kwa vile wewe uko karibu naye mpe pole sana mwenyezi mungu amuepushe hilo na mengine
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Falhum Mshana amemtaja marehemu kwa jina la Majidu Chowo (60) ...

... mke aliyekuwa akiishinaye aitwaye Asia Nchimbi (35)...

... Asia Nchimbi alimpata hawara aitwaye Nasibu Konde (26) ambaye alimwambia hana mume kwani aliyekuwanaye wameachana.

Masaibu mengine ni magumu kuepuka; hebu fikiria: mzee wa miaka 60 ana mke wa miaka 35, halafu huyu mama huenda hakuwa akitosheka na mzee huyu; akatafuta kijana wa miaka 26.

Wazee wenzangu msikate tamaa hata kama umri umesonga; nzi kufia kidondani siyo dhambi!
 
Back
Top Bottom