Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Yanasemwa mambo mbalimbali kumhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Ni juu ya hatma yake kama Mkuu wa Mkoa kufuatia sakata lake la makontena yanayoshikiliwa na TRA ambayo yatapigwa mnada kesho. Wapo wanaosema kuwa huu sasa ni mwisho wake kama mkuu wa mkoa na atatumbuliwa. Wapo wanaosema kuwa atabakia kuwa mkuu wa mkoa na atabakia alivyo.
Baada ya jana Mhe Rais kuvunja ukimya na kuweka nukta juu ya sakata hilo akiwa Wilaya ya Chato mkoani Geita, kila mwananchi aliyeweza kusema amesema lake. Wengi, lakini, wanatamani kuona mwisho wa Makonda ukifika. Wanachagiza mwisho wake na 'kashfa' zake mbalimbali mpya na za zamani kama kuwa na 'utajiri wa kutisha' na hata kumiliki Ardhi ya ukubwa wa viwanja 15 vya mpira mkoani Dodoma-kwa mujibu wa gazeti la Sauti Kubwa la jana.
Kiuhalisia na katika Maisha yetu ya kitanzania, ni nadra sana wananchi kutakiana laana au kuanguka. Mara nyingi, hata kinafiki, hutakiana mema na ya neema. Kutakiwa mabaya waziwazi si jambo la mchezo. Ni jambo la kuogofya na kutoa mafunzo kwa wananchi wote watakaobahatika kuwatumikia wengine. Inaonyesha jinsi wanachi walivyochoka na kuchoshwa na uwepo wa kiongozi katika nafasi aliyonayo.
Viongozi wetu wa Serikali na vyama tunawapenda na kuwaheshimu sana. Tunawapenda kwakuwa ndiyo Mungu aliotujaalia na kutubariki kuwa nao kwa muda husika. Tunawasikiliza na kuwafuata kutokana na wanachotuelekeza. Tunawapigania na kuwatetea; tunawaombea na kuwatakia mema kwa kiasi kikubwa. Lakini, kutokana na ubinaadamu wetu, kwa kiasi hichohicho huwatakia mabaya na kutamani kuona mwisho wao. Pale wanapotuonyesha kuwa hatukuwa tumepata ila tulipatikana.
Nasema, Makonda atoke au asitoke katika nafasi ya mkuu wa mkoa au nyingineyo, tunalo jambo kubwa la kujifunza. Viongozi, kama walivyo wananchi wao, wanapaswa kujinyenyekeza. Hata wakisema na kusema kwa staha, busara na hekima, mamlaka na madaraka yao hubakia na kuimarika. Kuheshimu na kujali unaowaongoza huongeza ulinzi, maombi, utetezi na baraka kupitia shukrani. Hata minara hujengwa kwa ukumbusho wa mema isipokuwa katika nchi za kidikteta kama kwa Marehemu Sadam Hussein wa Iraq