Atm nyingi tz in mitumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atm nyingi tz in mitumba

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njowepo, Oct 10, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  ATM nyingi ni mtumba Send to a friend Friday, 08 October 2010 19:28 0diggsdigg

  Alvar Mwakyusa
  TEGEMEO la kupata fedha kwa haraka kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya ATM, linaweza kukwamishwa na maneno ya kuudhi yanayoandikwa kwenye mashine hiyo yakisema "tunasikitika huduma hii kwa sasa imesitishwa".

  Baada ya hapo, mteja anaweza kuzunguka kutoka mashine moja hadi nyingine bila ya mafanikio na kila sehemu anaweza kukutana na maneno hayo na inapotokea amebahatisha kukuta mashine moja inafanya kazi, basi atakumbana na msululu wa watu.
  Mwananchi inaweza kukuthibitishia kuwa tatizo hilo linatokana na mashine hizo za kuchukulia fedha zinazoitwa ATM kununuliwa zikiwa mitumba na hivyo kutoweza kufanya kazi kwa ufanisi.

  Baada ya uchunguzi uliofanywa kwa takriban wiki tatu na gazeti hili, imebainika kuwa mashine nyingi hununuliwa zikiwa kuukuu na hivyo kuharibika mara kwa mara au kupoteza mawasiliano na hivyo kushindwa kufanya kazi yake, hali ambayo husababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa huduma hiyo.

  Teknolojia ya ATM iliingia nchini mwanzoni mwaka 2000 ikiaminika kuwa itakuwa mkombozi wa wateja wa huduma za kibenki zinazopatikana ndani ya ofisi hizo, hasa kwa wateja ambao wanahitaji kuchukua fedha kidogo.
  Mageuzi makubwa yaliyojitokeza kwenye sekta ya fedha yalitaka mteja apate huduma kwa masaa 24 na hivyo kupunguza misululu kwenye benki au kusaidia wateja walio makazini kuwa na muda wa kuchukua fedha pindi watakpo kazini.
  Lakini takribani miaka kumi tangu kuingia kwa teknolojia hiyo, Mwananchi limebaini kuwa huduma hiyo imegeuka kuwa kero nyingine kwa wateja wa huduma za benki.
  Wateja wengi wamelalamika kuwa wanashindwa kupata fedha kwa muda mwafaka kutokana na mashine hizo kuharibika mara kwa mara na kushindwa kutoa fedha.

  Hali hiyo imefanya teknolojia hiyo isiwe ya kuaminika kwa wateja ambao wamekuwa wakilazimika kuzunguka ATM tofauti ili kupata fedha, hasa katika siku za mwisho wa juma na mwisho wa mwezi.
  Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika kutoka benki mbalimbali nchini, tatizo la uchakavu wa ATM ni kubwa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa zinazoingizwa nchini ni zile zilizokwishatumika katika nchini nyingine na hivyo kuingizwa nchini ili kuja kumalizia uhai wake, lakini benki hizo zimeamua kulifumbua macho suala hilo.

  “Tatizo ni kubwa sana na ni la nchi nzima… hata uongozi wa benki unalijua hilo ila umeamua kulifumbia macho. Wenye benki wanakimbilia zaidi faida kuliko kuboresha,” alisema mtoaji habari wetu kutoka moja ya benki kubwa nchini.
  Hata hivyo, vyanzo vingine vimehusisha huduma hiyo mbovu na uduni wa teknolojia ya mawasiliano unaotumiwa na benki hizo.
  Uduni wa teknolojia umeelezwa na baadhi ya vyanzo hivyo vya habari kuwa unachangia uhafifu wa huduma za ATM, hasa katika siku za mwisho wa juma na mwisho wa mwezi ambazo wateja huwa wengi na mahitaji ya fedha kuwa makubwa.
  “Tatizo siyo teknolojia bali ubahili wa benki katika kununua mashine mpya na kutoajiri wataalamu wa ATM wa kutosha aidha kutoka nje ya nchi au kuwapatia mafunzo Watanzania ili waweze kufanya kazi hiyo,” alisema mpashaji mwingine kutoka benki ya jijini Dar es salaam.

  Habari zaidi zimeeleza kuwa wataalamu wengi wa mashine za ATM hufanya kazi kama vibarua. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, watalaamu hao hawana ajira hali ambayo inawafanya wajihusishe zaidi na shughuli binafsi badala ya kushughulikia matatizo ya mashine hizo.
  Hata hivyo, maafisa wa baadhi ya benki hizo wamepinga taarifa kwamba matatizo hayo yanatokana na uhaba wa watalaamu na kubainisha kuwa tatizo ni ubovu wa miundombinu.
  Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NBC, Lawrence Mafuru alisema si kweli kwamba mashine zinazotumiwa na benki hizo ni chakavu.

  “Kwa mfano, benki yangu imefanya makerebisho makubwa katika mfumo wake kutoka mwezi Machi mwaka huu na teknolojia inayotumika ni mpya kabisa. Tatizo kubwa tunalokumbana nalo ni uduni wa mawasiliano,” alisema Mafuru.
  “Mfumo wa mawasilino unaotumika kwenye ATM ni sawa kabisa na ule unaotumiwa na mitandao ya simu… ni mara ngapi umewahi kupiga simu na ikakataa,” alihoji bosi huyo wa NBC.
  Alikiri, hata hivyo, kwamba baadhi ya benki zimekuwa zikitoa huduma zisizoridhisha kwa wateja wao.
  “Hivi karibuni tulifanya utafiti kwa kutumia taasisi huru ambayo imeonyesha kwamba ATM zetu zinafanya vizuri katika soko ikilinganishwa na nyingine,” alijigamba Mafuru.

  Aliongeza kuwa benki hizo hushindwa kukadiria kiasi cha fedha kinachohitajika na wateja kwa siku za mwisho wa juma na siku za mwisho wa mwezi, hivyo kusababisha usumbufu kwa wateja wao.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa CRDB, Esther Tully Mwambapa aliliambia gazeti hili kwamba benki yake hununua mashine mpya kutoka kampuni ya Kimarekani ya NCR ambao ni watengenezaji wakubwa wa mashine hizo duniani.
  “Si kweli kwamba mashine zetu ni mitumba japo inawezekana kuwa baadhi ya benki nchini ambazo ni kampuni tanzu za mabenki makubwa ya kigeni zinaweza kuwa na mashine ambazo ni mitumba kutoka kwa kampuni zao mama,” aliseme Mwambapa.
  Aliongeza kwamba benki yake ina zaidi ya mashine 100 za ATM nchi nzima.

  Kuhusu mawasiliano ya mtandao, Mwambapa alisema benki yake inatumia wasambazaji mbalimbali wa mtandao wa internet ili kuwa na uhakika wa mawasiliano kwa muda wote hasa pale panapotokea matatizo kwa msambazaji mmoja.
  “Katika sehemu nyingine za nchi tumeweka vifaa vyetu vya mawasiliano ambavyo vinawezesha mawasiliano,” alieleza.
  Alifafanua zaidi kwamba kwa mashine zilizo nje ya matawi ya benki (off-site ATMs) mabenki nchini yamepangiwa kiwango maalum ambacho wanaweza kuweka pesa katika mashine hizo.

  “Hili ni suala la kiusalama zaidi, kwa hivyo utakuta kwa siku za mwisho wa juma ambazo wateja huwa wengi, pesa zinaweza kwisha wakati kuna wateja wanahitaji fedha. Jukumu la benki ni kujaza pesa katika mashine mara zinapokwisha, lakini zinakwaminshwa na kiwango kilichowekwa pamoja na uwezo wa ATM husika,” alieleza.
  Kwa mujibu wa Mwambapa kukatika kwa umeme mara kwa mara pia ni tatizo kwa mashine hizo kwa kuwa huzifanya kuwaka na kuzima mara kwa mara na hivyo kuathiri utendaji wake.
  Mkurugenzi huyo wa masoko na utafiti wa CRDB alisema pia kwamba benki yake imeajiri wataalam wa ATM ambao hupatikana muda wote kurekebisha mashine hizo pale panapotokea tatizo.

  Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omari Yusufu Mzee alisema matatizo ya mashine hizo ni ya kawaida kutokana na kwamba kuna muda maalum wa kuweka pesa katika mashine na wala si ubovu.
  “Mashine za ATM zina uwezo wa kuchukua milioni 20 na hivyo ni kawaida pesa kuisha hasa kwa siku za mwisho wa juma. Kuna haja ya kuelimisha umma kwamba mashine hizo zinapokuwa zinashindwa kutoa pesa ni kwa sababu zinakuwa zimeisha na wala si ubovu na hivyo wawe na subira wakati maafisa wa benki wakishughulikia kujaza fedha nyingine,” alisema kwa njia ya simu.
  Kuhusu suala la mashine hizo kuwa mitumba, alisema: “Kwa sasa nina uhakika kwamba benki nchini zinanunua mashine mpya kabisa sijui kwa kipindi cha nyuma kwani sikuwa katika taasisi yeyote inayoshughulikia mambo ya fedha.”

  Hata hivyo, alisema serikali imekuwa ikiwahimiza wenye benki nchini kutumia mtandao mmoja wa ATM ili mteja anapokosa fedha katika mashine inayoendeshwa na benki moja aweze kwenda katika mashine nyingine ya benki tofauti.
  “Hii inawezekana kama wanavyofanya watu wa Umoja Switch au Visa cards ambazo mteja huweza kutumia kadi zao kuchukua fedha katika mashine za benki mbalimbali,” alisema naibu waziri huyo.
  Juhudi za Mwananchi kupata viongozi waandamizi wa Benki Kuu (BoT) kuzungumzia suala hilo katika siku tatu zilizopita hazikuzaa matunda.

  Gavana wa BoT, Prof Benno Ndulu aliliambia gazeti hili kwamba hangeweza kuzungumzia kwa kuwa alikuwa jijini Washington, Marekani ambako anahudhuria mikutano ya kila mwaka ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia (WB).
  “Naomba niandikie maswali yako unitumie kwa sms (akimaanisha ujumbe mfupi wa simu). Siwezi kuzungumza kwa sasa kwa kuwa niko katika mkutano,” alisema Gavana Ndulu.

  Hata hivyo pamoja na kuandika maswali hayo hakuwa ametoa majibu mpaka tunakwenda mitamboni.
  Maafisa wengine waandamizi wa benki hiyo, akiwemo mkurugenzi wa utafiti wa uchumi na sera, Dk Joseph Massawe pia alisema yuko mkutanoni Marekani na Gavana Ndulu hivyo hawakuweza kuzungumzia suala hilo.
  Mkurugenzi wa Mfumo wa Malipo wa BoT Lucy Kinunda aliomba muda mpaka Jumatatu ijayo ndipo atakapoweza kuzungumzia suala hilo
   
 2. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wadau, this could be time for wana JF kuanza kutatua matatizo ya jamii kwa kushirika ya Wabunifu USA (A California Nonprofit Public Benefit Corporation). Tutatumia technology kuleta ufumbuzi wa matatizo ya matumizi ya ATM kupitia serikalini. Naamini serikali hairidhiki na hiyo hali. Na kama inaridhika basi sawa, angalau malalamiko ya kulaum benki yatakwisha. Sisi hatulaum benki kwa sababu benki wanatangaza customer care na jinsi nilivosoma nakala yako, inaonyesha kua benki hawana ufumbuzi huo. Na sisi sote ni binAdam. Naomba ni PM contact zako kama unapongeza huu mswada wangu. Inatia huruma mtu kuhangaikia pesa zako baada ya kuzitolea Jasho. Toba!!! :)
   
 3. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mimi naweza kuwa kidogo against na wewe mkuu khs MASHINE kuwa mitumba,yaweza kuwa bank ndo tatizo maana mashine inapokuwa haina hela haiwezi andika maneno hayo I mean programmable mashine iwapo kuna hitirafu au upungufu wa hela ndo maneno yao...Bongo yetu mkuu unaijua na wafanyakazi bank wote wavivu na maana kwamba sijui wanafurahia kuwa na msululu cashier au niaje?

  VOTE FOR SLAA YOTE TUTAYAMALIZA....
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona CRDB wameanza install angalau ATM mpya so far nimeziona iringa,makambako na dsm.
  Personally nimezipenda
   
 5. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CRDB waliinvest kwenye business strategy zao nadhani. Walikuepo Marekani Kwenye DICOTA (DATA) ambayo ilifanyika Minessota mwka huu nadhani. Nafikiri kutoka walibadilishana mawazo na watu wengi. Ndio Uzuri wa kuhudhuria Trade Shows, Wabunifu inajaribu kutazama uwekano wa kufanya TRADE SHOW, kama Waliofanya DICOTA. Isipokua kua Wabunifu USA, watafanyia yao LOS ANGELES CONVENTION CENTERS. In the Middle of Down Town Los Angeles, next to Staple Centers and Nokia Thearters. I think Los Angeles can find a rooms to accomodate JF members. Yaani kwa tatizo la ATM ni kuzimwaga. si wateja wazitaka bana, tunaambiwa mteja ni kumridhisha. kwa sababu yeye ndio mwenye hela, ambayo ndio sababu ya benki kuingia biashara.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nadhani hoja ya msingi au tatizo sio umitumba wa ATM. bali ni huduma mbovu za benki. ATM hata kamani mtumba lie span yake ni kubwa tu. Mara nyingi ATM haziharibiki. tatizo kubwa kwenye ATM ni Kuishiwa Pesa .Na communication /network poblem kati ya ATM mashine na bank Account Database.

  Na mbaya zaidi ATM haziandiki matatizo haya yakitokea. Zinaandika mambo tofauti na hivyo kuwachanganya wateja.

  na zaidi ya ATM hata Magari,vifaa vya electronic kama majokofu etc.Tanzania ni Mitumba. Ni purchasing power yetu ndio ina determine bidhaa gani tutumie
   
Loading...